Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hii ni aibu kwa taifa la Tanzania na wananchi wake kuwa na tabaka la watu wenye Elimu na uelewa wa namna hii!. Je, ni kweli shule za Kata ndo chanzo cha yote haya!!!! au walimu wa VODA FASTA ndo chanzo cha haya! au zamani watu walikuwa wakiiba sana mitihani na mwaka huu wamezibitiwa wizi??? au morali ya waalimu haipo katika suala zima la ufundishaji kama ilivyokuwa enzi zile hasa kwa shule za Serikali????
Maswali haya na mengine yanahitaji majibu na ufumbuzi, Tutafute suluhisho la hili, Nini kifanyike kuondokana na tatizo hili???.
Hapo chini ni Matokeo hayo kwa kifupi yakionyesha Idadi kwa kila daraja na asilimia zake.
Daraja I - 5,363 1.5% Daraja la II 9,942 Asilimia 2.8% Daraja la III 25,083 Asilimia 7.1% Daraja la IV 136,633 Asilimia 38.9% Daraja la 0 174,193 Asilimia 49.6% na Jumla ya wanafunzi 351,214 walifanya mtihani huo.
NB: Kwa kifupi, Daraja la Kwanza hadi la Tatu ni asilimia 11.5 tu na madaraja ya Nne na la Zero (o) yanachukua asilimia 38.9 na aslimia 49.6 sawia. Hii inaashiria nini kwa Taifa la Tanzania?? na hata
Waziri wa elimu sijasikia akitoa tamko na wala Mhe. Dr. Dr. Jk yuko inje ya nchi wala hashitushwi na hali hii anaona ni kawaida tu! Kwani Maisha bora kwa kila Mtanzania yanawezekana kwa mfumo huu wa kuwa na tabaka la watu wa aina hii ambao watakuja kuwa Madaktari Mhimbili, Bugando, KCMC na watakuwa Specilist wa Ubongo na mifumo ya fahamu!!!!.
Inabidi shule binafsi zifutwe...
.....
ukiangalia shule za kata, project ile ilikuwa ni ya voda fasta, ili mafanikio yaonekane JK akiwa madarakani. hakuna kitu kama hicho. mafanikio ya kweli ya elimu yangeanza kuonekana kuanzia miaka 5 na kuendelea. yaani kama JK angekuwa serious katika elimu toka awamu ya kwanza, sasa hivi ndio tungeanza kuona matunda, kidogo kidogo. lakini yeye anataka matokeo palepale. sawa tu na katika mpira. badala ya kuleta mabadiliko ya kweli ya football kwa kuanzia kuwekeza kwa vijana wa umri mdogo, anatumia gharama kubwa sana kwa timu iliyopo sasa ili avune sifa zake.
Unashangaa JK yupo kimya? siku hizi amegundua ka mtindo. anaminya kimyaa. si umeona la Dowans?
Nakubaliana na wazo hilo badala ya kujenga mashule katika kila kata kungekua na shule kubwa na zenye madarasa ya kutosha katika kila wilaya au TARAFA hii ya kila kata naona kwa nchi yetu bado itasumbua sana hasa kwa suala la miundo mbinu upatikanaji wa waalimu pamoja na maabara na vifaa vya maabara pia fedha za kuziendeshea hizi shule kwasababu kutakua hakuna faida yeyote mmejenga shule nyingi halafu wanafunzi wanafeli kwa kuwa shule hazina waalimu na hazijitoshelezi kimiundombinu pia kipato cha waalimu ni kidogo na hawana nyumba za kuishi serikali ingekaa chini na kuliangalia upya hilo either wabadilishe mfumo kwenda kwenye tarafa au wilaya wajenge shule kwa level hiyo!Najiuliza sipati majibu
- Shule za kata zinasimamiwa na Wizara ya Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa
-Shule za zamani kama azania, tambaza, ilboru, msalato, etc the like, zinasimamiwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya ufundi stadi
-Baraza la mitihani linasimamiwa na wizara ya elimu
Kituko kingine
Mfano DAR ES SALAAM
-Shule za secondary za kata na zile rasmi za zamani (za o-level tu) nyingi mno. pengine zaidi ya 30- kupitia MEMM wamejenga shule nyingi sana za O-level, chanika almost kila street in shule ya kata.
-High school zilizopo ukiondoa Kibasila zote ni zile zile zilizoko eneo la upanga - Jangwani, Zanaki, Azania, Tambaza.
Katika hali hii, kama nilivyo wasikia watu wakihoji, Je baraza la mitihani linaweza kuwa fair katika kutoa alama kati ya shule za kata (zisizo na vifaa na walimu waliobobea na zilizo chini ya Tamisemi) na shule za secondary zilizo chini ya wizara ya elimu ilhali yenyewe iko chini ya wizara hiyo hiyo?
Kwa nini serikali isijenge angalau high school mbili au moja iliyokamilika kila wilaya?
Sababu za kufeli zipo nyingi kama walivyosema wenzetu. Lakini jambo moja la msingi ni kuwa hizo shule za KATA ambazo zimechangia sana kufeli HAZIKUWA NA WALIMU. Kuna baadhi ya maeneo tumepata taarifa za vyombo vya habari kuwa kulikuwa na mwalimu MMOJA, WAWILI, AU WATATU TU. Tulitegemea nini katika mazingira kama hayo? Jambo la pili ni kuwa hao walimu wa shule za kata walikuwa ni wale WASIO NA UJUZI. Wengi wao walipata mafunzo ya miezi mitatu ambayo hata English Course mwanafunzi angekuwa hajafaulu bado.
Matatizo hayo chanzo chake ni kwenye awamu ya TATU YA BWANA BEN. Ben alikuwa mpango wa MEM wa shule za msingi bila kujua kama shule hizo baadaye zitakuja kutoa wanafunzi wa SEKONDARI. Walimu walipaswa kuandaliwa na awamu ya Mkapa ili watumike kwenye serikali ya awamu ya NNE ya JK junior. Tunazalisha taifa la walioshindwa, taifa watu wasioweza na hilo ni JANGA jipya kwetu wenyewe maana tunaanda vijana watakao kuja kuleta matatizo kwenye jamii yetu. TUNAANDAA KUFELI KWA TAIFA ZIMA!
@ Tuko, Sioni kama hilo linaweza kuwa suluhisho! Mie hapa kwenye hoja yako hiyo kama shule za binafsi zinafaulisha kuliko serikali ni kwa nini?? je zinawaalimu ambao wako motivated!!, mazingira ya kusoma na kufundishia yako condusive, na mambo mengine kibao!. Lakini je Shule za Kata au Serikali zinawaalimu???, zina mazingira condusive kama ya shule za private???, au kama ni mishahara private wanapesa nyingi kuliko serikali!!???. Kufuta shule hizo hakuwazi kuwa suluhisho.
Kwani mkono wako ukijaa au ukashika mavi unaukata au unausafisha na kuendelea na kazi zake??
Hii ni aibu kwa taifa la Tanzania na wananchi wake kuwa na tabaka la watu wenye Elimu na uelewa wa namna hii!. Je, ni kweli shule za Kata ndo chanzo cha yote haya!!!! au walimu wa VODA FASTA ndo chanzo cha haya! au zamani watu walikuwa wakiiba sana mitihani na mwaka huu wamezibitiwa wizi??? au morali ya waalimu haipo katika suala zima la ufundishaji kama ilivyokuwa enzi zile hasa kwa shule za Serikali????
Maswali haya na mengine yanahitaji majibu na ufumbuzi, Tutafute suluhisho la hili, Nini kifanyike kuondokana na tatizo hili???.
Hapo chini ni Matokeo hayo kwa kifupi yakionyesha Idadi kwa kila daraja na asilimia zake.
Daraja I - 5,363 1.5% Daraja la II 9,942 Asilimia 2.8% Daraja la III 25,083 Asilimia 7.1% Daraja la IV 136,633 Asilimia 38.9% Daraja la 0 174,193 Asilimia 49.6% na Jumla ya wanafunzi 351,214 walifanya mtihani huo.
NB: Kwa kifupi, Daraja la Kwanza hadi la Tatu ni asilimia 11.5 tu na madaraja ya Nne na la Zero (o) yanachukua asilimia 38.9 na aslimia 49.6 sawia. Hii inaashiria nini kwa Taifa la Tanzania?? na hata
Waziri wa elimu sijasikia akitoa tamko na wala Mhe. Dr. Dr. Jk yuko inje ya nchi wala hashitushwi na hali hii anaona ni kawaida tu! Kwani Maisha bora kwa kila Mtanzania yanawezekana kwa mfumo huu wa kuwa na tabaka la watu wa aina hii ambao watakuja kuwa Madaktari Mhimbili, Bugando, KCMC na watakuwa Specilist wa Ubongo na mifumo ya fahamu!!!!.
Mtoto wa mwalimu anasoma private, mtoto wa mwenyekiti wa bodi ya shule anasoma private, mtoto wa diwani anasoma private, mtoto wa afisa mtendaji (kata) anasoma private, mtoto wa katibu tarafa anasoma private, mtoto wa afisa elimu, na wa mkuu wa wilaya, na wa mkurugenzi wanasoma private. Watoto wa wakurugenzi wote wizarani, wa katibu mkuu, wa makamishna, na wa waziri, wanasoma private.
Kikao kinafanywa na hawa 'wadau' wa elimu kuboresha shule za serikali. Unadhani zaidi ya kuongea, utekelezaji na ufuatiliaji utakuwepo hapo? Fikiria kuwa watoto wa 'wadau' hawa wangekuwa wanasoma kwenye hizi shule zisizo na madawati, vitabu wala walimu, huoni wangeguswa kidogo kuziboresha. Ongea na mwalimu yeyote wa primary au sekondari leo, anakuambia mi sina mda wa kufatafata mitoto ya watu, aandike asiandike, afaulu asifaulu, shauriyake. Ukimuuliza na mwanao je, anasema mwanangu anasoma St nini sijui. Uzalendo haupo. Shule za private zifutwe, tubanane humohumo. watoto wetu sisi walalahoi wakalie tofali moja na watoto wa waziri.
Short and Clear: TATIZO LA WANAFUNZI KUFELI NI CCM; NAMNA YA KUIONDOA TATIZO NI KUIONDOA CCM MADARAKANI
Haingii akilini CCM wanaondoa mtihani wa Form II the mtu anfika form four bila kufanya mtihani hat mmoja. mwisho wa siku unategemea nini?
Haingii akili kuona shule nyingi hazina waalimu na serikali ya CCM haitaki vijana waliomaliza vyou mwaka huu na kuwachukua wachache eti serikali haina Pesa, wana pesa za kugawa bure wakati wa uchagu na kulipa makampuni hewa ya mifukoni mwa watu kama Dowans n.k. ila hawana pesa za kuwlipa waalimu na kuwajengea manyumba.
Hii haiwezekani na hali hii ikiendelea kwa miaka kama miwili au mitatu watu wageuka na kuwa kam Tunisia