MATOKEO ya Kidato cha Nne a mjadala wa kuboresha Kufaulu

MATOKEO ya Kidato cha Nne a mjadala wa kuboresha Kufaulu

safi sana...na unakuwaje wewe ni great thinker? na wakati hata magreat thinkers hawakuleta udini wala vijembe ila walichallenge ili kuboresha ukweli ni uleule tuwasaidi kimawazo ili watoke kwenye pango la giza sio udini hapaaa.

Mie nimeonyesha tu kiu ya kujua Zaidi, tafadhali mwenye kuweza kunipatia analysis kama hio anisaidie, matokeo haya yanauma sana hasa ukizingatia 70% ya wadogo setu wana zero na four, tunawapeleka wapi? na mwakani wanakuja wengine tukae mkao wa kuwapokea.
Tujitahidi tuende mbali zaidi ya kufikiria dini hizi mbili, labda kama tuna hamu ya kubishana.
Mimi nadhani kuwa elimu ya ahera ni muhimu sana, na huwa nawaonea wivu wanaosoma KUIKWELI, sio wale wanaopotezewa muda kwenda kuimba kwenye kila maulidi mtaani.
Elimu ya duniani ni muhimu sana, lakini si rahisi kumpa mtu uungwana, utu, heshima, woga wa utu wa wenzake, maadili nk.

Tukirudi kwenye matokeo, Haijalishi dini zao wala makabila yao, wote hawa wanakuja kwenye soko la watu wazima Tanzania na ndio hawa watakuwa wabunge wetu, wezi wetu, wanamageuzi wetu madaktari na manesi wetu, walimu na madereva wetu, wakati sie wazee hatuwezi kuamua mambo, hawa ndio watakaokuwa nwanatuamulia, watatupeleka wapi?
Nikifikiria hii picha ya baadae naona ni kama jinamizi!!!
 
Kuna wito ambao umenivutia. Naomba kuwashirikisha wote. Nakubaliana na mtoa mada kwamba mass failure ya F4 inabidi kuangalia mfumo mzima kwa ujumla wake. Kuanzia mazingira shule za msingi na sekondari, wanafunzi wenyewe, waalimu, watunga mitihani, wasahihishaji na mtaala mzima wa elimu yetu.
 
Attachments

  • f4-wito.jpg
    f4-wito.jpg
    16.8 KB · Views: 160
Najiuliza sipati majibu
- Shule za kata zinasimamiwa na Wizara ya Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa
-Shule za zamani kama azania, tambaza, ilboru, msalato, etc the like, zinasimamiwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya ufundi stadi
-Baraza la mitihani linasimamiwa na wizara ya elimu

Kituko kingine
Mfano DAR ES SALAAM
-Shule za secondary za kata na zile rasmi za zamani (za o-level tu) nyingi mno. pengine zaidi ya 30- kupitia MEMM wamejenga shule nyingi sana za O-level, chanika almost kila street in shule ya kata.
-High school zilizopo ukiondoa Kibasila zote ni zile zile zilizoko eneo la upanga - Jangwani, Zanaki, Azania, Tambaza.

Katika hali hii, kama nilivyo wasikia watu wakihoji, Je baraza la mitihani linaweza kuwa fair katika kutoa alama kati ya shule za kata (zisizo na vifaa na walimu waliobobea na zilizo chini ya Tamisemi) na shule za secondary zilizo chini ya wizara ya elimu ilhali yenyewe iko chini ya wizara hiyo hiyo?

Kwa nini serikali isijenge angalau high school mbili au moja iliyokamilika kila wilaya?

Naomba nikusahihishe mkuu! hapo kwenye hiyo nyekundu, ni kwamba shule zote za sekondari kuanzia mwaka 2009 ziko chini ya TAMISEMI, chini ya uongozi wa afisa elimu wa secondari wa wilaya. Tofaut na zamani sasa kila wilaya ina afisa elimu wa secondary ambaye anashughughulikia mambo ya secondary tu. Kwa hiyo jukumu la wizara ya elimu kwa sasa ni kusimamia vyuo vya ualimu ngazi ya cheti na stashahada(diploma),
 
Kwa kuwa serikali inataka kufanya form 4 kuwa kiwango cha Chini cha kuanzia cha Elimu , isikifanye kiwe cha dharau Basi, itafute mbinu ya kuonyesha wanaomaliza wanauelewa, Wajaze vifaa vya kutosha kwani njia nyingi za kupata hela hizo zipo, Kwa wale wote walifeli form 4, wasidanganye Kabisa kwenye marudio kuufanya Upya kama PC kule kuna watu wana roho mbaya hawataki watu WASHINDE Mtihani HII kwani wanatunga Mitihani Migumu sana kupita kiasi,. ANGALIZO chukulia wewe umeshindwa MTIHANI wa form 4 kwa kupata 0 yaani 30 pointi unakutana na MTIHANI wa Form 6 eti unaitwa PC kweli hapo kuna UTU utasoma mpka macho yatatoka, hata usome vipi utaendelea kutoa hela kila mwaka ku-reset lakini hamna Mtu wa Kupata , angalia MIAKa hii Mitatu iliyopita walirudia wote wamefeli kuliko hata wa Zamani
 
Mimi natoa wito kwa serikali kwamba badala ya Kurudisha National Service ya kupigishana kwata, ni bora Wakaifanya kwa kuchukua vijana wetu waliopata division 1 mpaka 2 form six kuwatrain na kwenda kufundisha kwenye shule hizi mpya za kata japo kwa miezi Sita wakati wakisubiri kujiunga University hii iwe inafanyika kila mwaka , na wale waliopata division 3 mpaka 4 lakini wana pass nzuri za O-level wanaweza kwenda kujitolea kufundisha primary kwa kipindi cha muda kadhaa. kwa kufanya hivi serikali iwahakikishie mkopo wenye masharti nafuu wa kusoma katika vyuo mbali mbali, na ofcourse iwapatie vijisenti kadhaa vya kujikimu[ siyo full salary].
Utaratibu huu pia unaweza kusaidia katika shughuli mbali mbali za maendeleo kama kuhamasisha kilimokwanza, kupambana na ukimwi, kutoa elimu ya uraia n.k, wapo vijana vichwa vizuri tu wakipewa chaki kuwapigia wenzao mbona utawakubali, by the way mimi nimepitia TUITION, na waliokuwa wantupigia mbona ni vijana wenzetu(siyo walimu by profession), lakini mambo yakawa mazuri?

Veri kileva idea
 
Akina Mzee Mohd pale K'koo...hehe,maana Aza Boys wa kipindi kile wanatambua na kuheshimu mchango wake.
 
Sababu kubwa hapa ni mazingira ya kufanyia kazi pamoja na kusomea.
wanasiasa wamejiingiza sana kwenye elimu kiasi kwamba wanadhani kujenga vyumba vya madarasa vingi ndiyo kuboresha elimu (rejea tambo za CCM wakati wa kampeni - uchaguzi mkuu). Kazi ya elimu wangeachiwa wataalamu si wanasiasa, madhara yake tumeyaona na tutaendelea kuyafeel kama elimu wataachiwa wanasiasa.
Kuna baadhi ya shule zilizo pembezoni kabisa kuna walimu wawili tu, tutegemee wanafunzi wafaulu kimiujiza? Je huko pembezoni hatuna wawakilishi na hawayaoni haya? kwa nini kusiwe na hazard allowance kwenye maeneo kama hayo ili walimu wawe na moyo wa kwenda huko?
Wabunge wanawaza mishahara yao na ma allowance yao kibao huku elimu ikididimia.

KUNA HAJA YA KUTANGAZA HILI KUWA JANGA LA KITAIFA
 
Siasa imeingizwa kwenye mambo yasiyotaka siasa. Serikalini wanaona fahari kuandikisha idadi kubwa ya wanafunzi vs ubora wa elimu ipatikanayo. Haki elimu walipiga kelele sijui wako wapi tena au walipigwa vice maana ccm sio mchezo. Malengo ya serikali sio elimu bora ila idadi ya wanafunzi shuleni. Hata mtihani wa dar la 4 wameshusha pass mark ili wingi uendelee.
 
sababu za kufeli kidato cha nne hizi hapa:
1. Shule za kata
2. Hiki ndo kidato wakati kipo mwaka wa pili serikali ilifuta kufeli kidato cha pili, na kusema kila mwanafunzi atapita tu.

naomba kuicheka serikali nikiwa nimekasirika.

Hahahahahaha ! muda wenu umekwisha sasa upuuuuzi sasa basiiiiii ! tokeni

tuache siasa kwenye vitu vya msingi,watu shule tumeenda hakuna mkazo wa kimasomo utakuwepo mashuleni kama hakuna mitihani,kuondoa mitihani ya darasa la 4 na kidato cha 2 ni vichekesho!na bado athari hizi hazitaishia mwaka huu tu ni mpaka marekebisho ya dhati yatakapofanywa ikiwa ni pamoja na kurudisha hiyo mitihani hapo kweli tutakuwa na nia ya kuwakomboa watanzania,tatizo letu tunajali wingi si ubora ili watu wajisifie kuwa mwaka fulani walimaliza watu kadhaa,na bado si ajabu hata mtihani wa kidato cha 4 nao ukaondolewa!kwani watanzania hakika tumechoka kufikiri.
 
Sie kama sehemu ya Jamii na ambao tumepatwa na huu mkasa na tunafahamu chanzo cha Tatizo, tutafute SULUHISHO LAKE!! nini kifanyike???.

Simple; retain the brightest minds and heads as teachers but this will not be cost free. Its time to pay good salaries to these minds.

Mfano: Ukiweka standard kuwa mwalimu yeyote wa sekondari aliyepata madaraja ya kwanza katika form four and six mshahara kwa mwezi ni take home ya Tshs 2m. Kama atapata daraja la kwanza chuo cha ualimu mshahara ni take home Tshs 4m. Kama huyuhuyu atapata at least daraja la pili la juu(upper second) chuo kikuu mshahara ni take home ya Tshs 6m. Tutakuwa na walimu watakaokuwa tayari kutumia nguvu na akili zao zote kwa ajili ya kutoa elimu bora.

Unapowapa nafasi ya kufundisha walimu wa UPE halafu kutunga mitihani unawatumia brightest minds ni lazima kusiwe na compatibility kama matokeo yanavyoonesha.

Nchi za wenzetu walimu wanalipwa kutokana na standard zao kwetu sisi ni generalisability yaani division four na one unawaweka chungu kimoja linapokuja suala la ualimu. South Korea wanaitwa walimu ni Nation builders na wanapewa nafasi kubwa sana katika jamii. Sisi mishahara mikubwa na malupulupu yote tunalimbikiza kwa wanasiasa, wabunge tunasahau "front liners" na matokeo yake ni haya. Serikali inaposema haina pesa za kuwalipa walimu mshahara huo wakati wabunge wanalipwa mshahara wa mwezi mmoja unaowalipa walimu kumi ni kutokuwa na kipaumbele na ubinafsi wa wanasiasa.
 
sababu za kufeli kidato cha nne hizi hapa:
1. Shule za kata
2. Hiki ndo kidato wakati kipo mwaka wa pili serikali ilifuta kufeli kidato cha pili, na kusema kila mwanafunzi atapita tu.

naomba kuicheka serikali nikiwa nimekasirika.

Hahahahahaha ! muda wenu umekwisha sasa upuuuuzi sasa basiiiiii ! tokeni

Nilidhani nitaona substance,duh!
 
Kwa kuwa serikali inataka kufanya form 4 kuwa kiwango cha Chini cha kuanzia cha Elimu , isikifanye kiwe cha dharau Basi, itafute mbinu ya kuonyesha wanaomaliza wanauelewa, Wajaze vifaa vya kutosha kwani njia nyingi za kupata hela hizo zipo, Kwa wale wote walifeli form 4, wasidanganye Kabisa kwenye marudio kuufanya Upya kama PC kule kuna watu wana roho mbaya hawataki watu WASHINDE Mtihani HII kwani wanatunga Mitihani Migumu sana kupita kiasi,. ANGALIZO chukulia wewe umeshindwa MTIHANI wa form 4 kwa kupata 0 yaani 30 pointi unakutana na MTIHANI wa Form 6 eti unaitwa PC kweli hapo kuna UTU utasoma mpka macho yatatoka, hata usome vipi utaendelea kutoa hela kila mwaka ku-reset lakini hamna Mtu wa Kupata , angalia MIAKa hii Mitatu iliyopita walirudia wote wamefeli kuliko hata wa Zamani

Mkuu sahihisho kidogo.
Divion zero kwa O level inaanza na points 34, yaani kati ya masomo saba uliyafaulu vizuri wanayotumia kukokotoa daraja unakuwa umepata alama "D" katika somo moja tu the rest ni "F"
 
Serikali ya Tanzania inaongoza kwa kua na mipango hewa ila utekeleza hua hakuna hebu kumbuka mkwere na mikwara yake ya mkukuta, mara mkurabita, mara takukuru pamoja na unafiki kibao, kilimo kwanza, mem na mengineyo, ni lazima tuicheke serikali ya CCM kwa kicheko cha hasira kwani badala ya kuendelea wao wanazidi kuturudisha nyuma. kuna kila sababu ya kuilaani CCM na kuiombea kifo kibaya ili angalau na sisi tuweze kujivunia kua watanganyika, Nchi iliyobarikiwa na Mungu kuwa na mali nyingi lakini Viongozi mbumbumbu, walafi, wachoyo, mafisadi, wajinga kupitiliza kiasi na wanafiki walo jawa na hiayana pamoja na roho mbaya.
 
Mkuu si kweli kwamba matokeo mabaya ni kwasababu ya shule za KATA. La asha, sababu ni kuwa serikali haikupeleka vitu muhimu katika hizo shule yaani walimu, vitabu, maabara, Library na kujenga nyumba za walimu.

Tusiwe wagumu wa kusema ukweli, serikali inahusika na matokeo haya kwa 101%. Na kama yangekuwa mazuri basi kwa wenye akili wangehoji imekuwaje matokeo yakawa mazuri?????!

Hiyo ya kufuta mitihani ya form 2 ni sahihi kabisa, mitihani hiyo ilikuwa inawapa vijana uzoefu wa kufanya mitiahani ya taifa na kujua umuhimu wa juhudi katika masomo.

Usishangae kusikia wahitimu wengine wa form 4 hata hawajui kusoma na kuandika; si wote tunakumbuka yule mkuu wa sekondari aliyelalamika kupokea vijana wa form 1 wasiojua kusoma na kuandika!!!!!!!!!!!

Tanzania yetu kwa pamoja tutaijenga!

Mimi sijakuelewa. Unabisha! Unakataa! ama unakubaliana na sababu? Mi sikuelewi ati!
 
Sie kama sehemu ya Jamii na ambao tumepatwa na huu mkasa na tunafahamu chanzo cha Tatizo, tutafute SULUHISHO LAKE!! nini kifanyike???.
Wanataka kupunguza wasomi maana ndio wanaweza kuwatoa madarakani
 
mkuu si kweli kwamba matokeo mabaya ni kwasababu ya shule za kata. La asha, sababu ni kuwa serikali haikupeleka vitu muhimu katika hizo shule yaani walimu, vitabu, maabara, library na kujenga nyumba za walimu.

tusiwe wagumu wa kusema ukweli, serikali inahusika na matokeo haya kwa 101%. Na kama yangekuwa mazuri basi kwa wenye akili wangehoji imekuwaje matokeo yakawa mazuri?????!

hiyo ya kufuta mitihani ya form 2 ni sahihi kabisa, mitihani hiyo ilikuwa inawapa vijana uzoefu wa kufanya mitiahani ya taifa na kujua umuhimu wa juhudi katika masomo.

usishangae kusikia wahitimu wengine wa form 4 hata hawajui kusoma na kuandika; si wote tunakumbuka yule mkuu wa sekondari aliyelalamika kupokea vijana wa form 1 wasiojua kusoma na kuandika!!!!!!!!!!!

tanzania yetu kwa pamoja tutaijenga!

naunga mkono asilimia 100 na sasa hivi kuna mtiririko wa shule za privateambazo hazina viwango unakuta shhule ina a level hawana maabara na serekali inashindwa kuzuia sababu za serekali nazo hazina maabara.. Hivi alevel ya science subjects bila maabara ina wezekana?
 
Tumegundua wasomi hawatawaliki,na wazazi wengi wanataka watoto wao wasome,...kwa sababu hiyo tutatimiza malengo ya milenia kufurahisha ulimwengu (maana ndo wamuhimu wasije kukata misaada), kwa kuandikisha watoto wengi shule,ila matokeo yake ni kuzalisha mbumbumbu zaidi
 
Back
Top Bottom