safi sana...na unakuwaje wewe ni great thinker? na wakati hata magreat thinkers hawakuleta udini wala vijembe ila walichallenge ili kuboresha ukweli ni uleule tuwasaidi kimawazo ili watoke kwenye pango la giza sio udini hapaaa.
Mie nimeonyesha tu kiu ya kujua Zaidi, tafadhali mwenye kuweza kunipatia analysis kama hio anisaidie, matokeo haya yanauma sana hasa ukizingatia 70% ya wadogo setu wana zero na four, tunawapeleka wapi? na mwakani wanakuja wengine tukae mkao wa kuwapokea.
Tujitahidi tuende mbali zaidi ya kufikiria dini hizi mbili, labda kama tuna hamu ya kubishana.
Mimi nadhani kuwa elimu ya ahera ni muhimu sana, na huwa nawaonea wivu wanaosoma KUIKWELI, sio wale wanaopotezewa muda kwenda kuimba kwenye kila maulidi mtaani.
Elimu ya duniani ni muhimu sana, lakini si rahisi kumpa mtu uungwana, utu, heshima, woga wa utu wa wenzake, maadili nk.
Tukirudi kwenye matokeo, Haijalishi dini zao wala makabila yao, wote hawa wanakuja kwenye soko la watu wazima Tanzania na ndio hawa watakuwa wabunge wetu, wezi wetu, wanamageuzi wetu madaktari na manesi wetu, walimu na madereva wetu, wakati sie wazee hatuwezi kuamua mambo, hawa ndio watakaokuwa nwanatuamulia, watatupeleka wapi?
Nikifikiria hii picha ya baadae naona ni kama jinamizi!!!