MATOKEO ya Kidato cha Nne a mjadala wa kuboresha Kufaulu

MATOKEO ya Kidato cha Nne a mjadala wa kuboresha Kufaulu

Mbona matokeo bado yapo kwenye website ya NECTA na hata kwenye website ya wizara ya elimu www.moe.go.tz jamani jf tuwe objective tunapojadili issues tuache hadithi

Mkuu website ya necta was down jana na leo earlier on ! na hii issue ya voda tangazo ilikuwa linapita hapo hapo kwenye website ya necta ...hamna hadithi hapa.
 
Wasichana watesa form IV


Wa Kwanza: "Siamini kabisaa, ila Mungu alikuwa akiniona nikisoma kwa bidii. Nimepata nguvu kubwa ya kuendelea kusoma kidato cha tano na sita na chuo kikuu. Matarajio yangu ni kuwa daktari," alisema kwa furaha Lucylight.

Wa Pili:
"Siri ni ufuatiliaji wa karibu wa walimu na Meneja wa shule. Pia kujituma mimi mwenyewe, mazingira mazuri ya shule na uhamasishaji wa wazazi wangu, lakini pia siwezi nikasahau msaada wa sala,"� alisema Maria-Dorin.

Na Waandishi Wetu, Dar, Arusha

WASICHANA wameendelea kuonesha makali yao katika masomo dhidi ya wavulana baada ya
kushika nafasi nane bora kati ya 10 kitaifa kwenye matokeo ya mtihani wa kidato cha nne yaliyotangazwa jana.

Matokeo hayo yaliyotangazwa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), Dkt. Joyce Ndalichako jana Dar es Salaam, yanaonesha kuwa nafasi ya kwanza hadi ya sita zimechukuliwa na wasichana, wakifuatiwa na wavulana wawili (namba 7 na 8), kisha mabinti hayo kumalizia nambari tisa na 10.

Kutokana na matokeo hayo, wanafunzi wawili walioongoza kitaifa walielezea furaha hao walipozungumza na Majira kwa nyakati tofauti, wakisema siri ya mafanikio yao ni kujituma wenyewe, juhudi za walimu wao, mazingira mazuri ya shule pamoja na msukumo wa wazazi wao.

Akizungumza na Majira Tengeru mkoani Arusha, mwanafunzi wa kwanza kitaifa kutoka Shule ya Sekondari ya wasichana Marian, Bi. Lucylight Mallya alisema matokeo hayo yamempa moyo na kumjaza nguvu ya kuongeza bidii kwa masomo yanayokuja ya kidato cha tano na ya chuo kikuu.

Kwa upande wake Maria Dorin Shayo aliyeibuka wa pili, pia kutoka shule hiyo, ametoboa siri ya suhindi wake ni kuwa mazingira mazuri ya shule na kupata walimu wa kutosha na wenye sifa.

Pamoja na washidni hao watahiniwa wengine katika kumi bora kitaifa ni, Sherryen Mutoka wa Shule ya Sekondari ya wasichana ya Barbro-Johansson, (Dar es Salaam), Diana Matabwa, St. Francis Girls (Mbeya) na Neema Kafwimi, St. Francis Girls (Mbeya).

Wengine ni Beatrice Issara wa shule ya St. Mary Goreti (Kilimanjaro), Johnston Dedani Ilboru (Arusha) na Samweli Emmanuel wa Moshi Technical (Kilimanjaro), Bertha Sanga, Marian Girls (Pwani) na Bernadetha Kalluvya wa St. Mary Goret (Kilimanjaro).

Washindi hao ni miongoni mwa wasichana 216,084 sawa na asilimia 47.17 waliosajiliwa kufanya mtihani huo mwaka jana. Wavulana walikuwa 242,030 sawa na asilimia 52.83, jumla ya watahiniwa wote walikuwa 458,114.

Jumla ya watahiniwa wa shule 177,021 sawa na asilimia 50.40 ya waliofanya mtihani wa kidato cha nne 2010 wamefaulu , ambapo wasichana waliofaulu ni 69,996 sawa na asilimi 43.47 na wavulana 107,025 sawa na asilimia 56.28.

Idadi ya watahiniwa wa kujitegemea waliofaulu mtihani ni 46,064 sawa na asilimia 52.09 ya waliofanya mtihani.Wakati huo huo, NECTA imesitisha kutoa matokeo ya watahiniwa 1,448 waliofanya mtihani bila kulipa ada ya mtihani hadi hapo watakapolipa pamoja na faini katika kipindi cha miaka miwili, tangu tarehe ya matokeo kutangazwa rasmi.

Bi. Ndalichako alisema kuwa baada ya muda huo kumalizika matokeo yao yote yatafutwa kwa mujibu wa kifungu 52 (b) cha kanuni za mitihani.

Pia wanafunzi wenye namba S0358/ na S0243/0007 waliofanya mtihani wa kidato cha nne Oktoba mwaka jana kwa kutumia sifa zinazofanana hawatapatiwa matokeo yao hadi wakuu wa shule watakapowasilisha nyaraka zinazothibitisha uhalali wao.

Pia mwanafunzi mwenye namba S3484/0014 anayetuhumiwa kufanya mtihani kwa kutimia sifa za mtu mwingine, uamuzi kuhusu matokeo yake utatolewa baada ya kukamilika kwa uchunguzi unaofanyika kuhusu uhalali wa sifa zake.

NECTA pia imefuta matokeo na kuwaondoa katika usajili wa mtihani huo watahiniwa wenye namba S1461/0060 na S1461/0146 wa shule ya sekondari Kisaka na S2777/0033 na S2777/0083 wa shule ya sekondari Nguvu Mpya waliofanya mtihani kwa kutumia sifa za watahiniwa wengine.

"Wengine waliofutiwa matokeo na kuondolewa katika usajili ni watahiniwa 35 wa shule ya sekondari Bara, waliosajiliwa katika shule hiyo kwa kutumia majina ya watahiniwa ambao walichaguliwa kujiunga na shule hiyo lakini hawakwenda kuripoti," alisema.

Alimtaja mtahiniwa mwingine aliyefutiwa matokeo kuwa ni wa shule ya sekondari Ludewa aliyefanya mtihani kama mtahiniwa wa shule wakati hakuwa miongoni mwa waliosajili.

Bi Ndalichako alisema watahiniwa wanne wenye namba S 1457/0004, S1457/0006,S1457/0039 na S1457/0027 wa shule ya sekondari Ibanda nao wamefutiwa matokeo kutokana na kutokuwa wanafunzi halali wa shule hiyo.

"Wataniwa wengine 42 wamefutiwa matokeo ni kutoka shule za Ujenzi, Kahama Muslim, John's Seminary, Eckernford, Seuta, Jamhuri, Madanya New Vision na Mseru waliofanya mtihani wakati walikuwa wameondolewa katika usajili baada ya kubainika kuwa sifa za kidato cha pili walizowasilisha hazikuwa sahihi.

Aliwataja watainiwa wengine wanne wenye namba S3526/0066, S0545/0066, S0859/0116, P0328/262 wamefutiwa matokeo baada ya kuandika matusi katika kitabu cha majibu ya Biolojia Geografia, Historia na Kemia.

Bw. Ndalichako alisema NECTA pia imefuta usajili wa kituo cha watahiniwa wa kujitegemea P1189 Biafra Dar es Salaam kutokana na kukiuka taratibu za uendeshaji mtihani.




2 Maoni:


STARTIMES said... vipi KAYUMBA's secondars schools maendeleo yao...je zimeingia hata 100 bora?
January 26, 2011 7:59 PM
blank.gif

Anonymous said... Shule za serikali labda nazo zianzie na St........
January 26, 2011 9:13 PM
 
Kama watanzania wengi wenye ndugu ambao wamemaliza form 4. Kitu kimoja kimenishangaza sana kwanini taasisi ya serikali inaweka tangazo kwamba kama mwanafunzi anataka kuona majibu kwa njia ya simu ni lazma awe na line ya VODACOM ilI apate majibu hayo! Serikali kuweni makini hio kitu haina manufaa kwa jamii husika kwasabau mnajua kabisa kwamba watu wanatumia line tofauti.


Over and out

WAFANYAKAZI SERIKALINI KUWENI MAKINI NA MIKATABA YA KIJINGA MNAYOINGIA AMBAYO HAINA MANUFAA KWA WALENGWA.

Rostam Azizi anatafuna nchi mpaka kwenye sms

mtakoma.
 
Kazi kwelikweli. Hii imenikumbusha rafiki zangu furani wa karibu. Kulikuwa na kazi imetokea mahari nakofanyia, nikawaambia waombe. Wakaanza oohh wewe umesoma sana ndiyo maana ulipata huko. Sifa zilizokuwa zinatakiwa nilijua wanazo, pamoja na kuwashawishi waligoma. Ila sasa kila siku wewe bwana siyo mwenzetu mambo yako super. Tatizo huwa hawataki kuthubutu na hili pia linaonekana kwa upande wa elimu.
 
JAMANI KWELI INASIKITISHA SANA NDUGU ZANGU!!!!!!!! sielewi kwanini seminary zetu za kiislam zinafanya vibaya kiasi hiki..... si shule wala mwanafunzi wake aliye kwenye nafasi za juu
 
Hivi huwa hakuna programme ya kuexchange ujuzi na uzoefu kwenye mashule? Nadhani shule zilizo karibu na seminari wanaweza kwenda kujifunza namna ya kusoma na kufaulu. Through that tunaweza kupunguza aibu kwa baadhi ya shule za serikali hasa za kata.
 
Wana JF kutokana na trend ya perfomance ya shule za sekondari za serikali mi nafikiri tuzigeuze shule zote seminary kwa kuzikabidhi makanisa mi naona serikali imeshindwa kuziendesha( MA SHEKHEH TUUNGENI MKONO KWA HILI)

inawezekana ikawa solushenieeeeeeeeeeeee
 
6. Pande Darajani (Tanga),
7. Igawa (Morogoro),
8. Makata (Lindi),
9. Mbuyuni na 10. Naputa kutoka Mtwara


na huku ndio ccm ilishinda kwa kishindo

hivyo unataka kutwambia hapa walimu na wanafunzi wakuwa busy na uchakachuaji wa kura wakasahau kujiandaa na mitihani!! hahahahahahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!
 
Wadada wametia fora.

Wanafunzi kumi bora kitaifa

1. Lucylight Mallya,(Marian),
2. Maria –Dorin Shayo (Marian),
3. Sherryen Mutoka wa Barbro - Johansson,
4. Diana Matabwa (St Francis)
5. Neema Kafwimi (St Francis)
6. Beatrice Issara (Mary Goreti)
7. Johnston Dedani (Ilboru)
8. Samwel Emmanuel (Moshi Technical)
9. Bertha Sanga (Marian)
10.Bernadetha Kalluvya (St Francis).


Boys pull up your trousers, aaanghhh!!!
 
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani, Joyce Ndalichako, alisema shule kumi bora zilizokuwa na watahiniwa kuanzia 40 na zaidi,ni

1. Uru Seminari (Kilimanjaro),
2. Marian Wasichana (Pwani),
3. St Francis (Mbeya)
4. Canossa (Dar es Salaam).
5. Msolwa (Morogoro),
6. Feza Wavulana (Dar es Salaam),
7. St Mary Goreti (Kilimanjaro),
8. Abbey (Mtwara),
9. St Joseph’s Iterambogo (Kigoma)
10.Barbro - Johnson (Dar es Salaam).

Wanafunzi kumi bora kitaifa

1. Lucylight Mallya,(Marian),
2. Maria –Dorin Shayo (Marian),
3. Sherryen Mutoka wa Barbro - Johansson,
4. Diana Matabwa (St Francis)
5. Neema Kafwimi (St Francis)
6. Beatrice Issara (Mary Goreti)
7. Johnston Dedani (Ilboru)
8. Samwel Emmanuel (Moshi Technical)
9. Bertha Sanga (Marian)
10.Bernadetha Kalluvya (St Francis).

Shule kumi za mwisho zilizokuwa na watahiniwa 40 na zaidi ni

1. Changaa, 2. Kolo, 3. Kikore, 4. Hurui, 5. Thawi, zote kutoka Dodoma
6. Pande Darajani (Tanga),
7. Igawa (Morogoro),
8. Makata (Lindi),
9. Mbuyuni na 10. Naputa kutoka Mtwara.


My take: Mtanisamehe mbona sioni shule za ndugu zetu na wanafunzi wao wakiongoza au ile nusu kwa nusu hai apply kwenye uwezo wa elimu hadi kwenye vyeo, naogopa wasije kuanza kulalamika kuwa aliyetangaza matokeo kapendelea.

acha udini wako wewe..kwa hiyo unawacheka au..maake naona unaandika kishabiki shabiki..unaona raha eehh..hivi nyie watu hamjui machafuko ya dini yalivo eehh?? acheni choko choko zenu, nakuambieni siku yakilipuka hapa mtajuta..unaacha kuwapa ushauri wa maana unauliza maswali ya kishabiki shabiki...udini si mzuri,,,sie wote watanzania and that's all what matters!!
 
Tatizo ndugu zetu wanawakataza watoto wao kula "kitimoto", ile kitu inaongeza akili sana.
 
6. Pande Darajani (Tanga),
7. Igawa (Morogoro),
8. Makata (Lindi),
9. Mbuyuni na 10. Naputa kutoka Mtwara


na huku ndio ccm ilishinda kwa kishindo

Dah watakiona cha moto mpaka 2015 wapate mkombozi
 
Tatizo kwenye shule za serikali ni kuwa uwiano wa idadi ya mwanafunzi kwa kila mwalimu ni mkubwa sana kiasi cha mwalimu kushindwa kuwafikia wanafunzi wote. Kinachofanya seminari kufanya vizuri ni kuwa idadi ya wanafunzi kwa darasa ni ndogo kulinganisha na shule za serikali
 
Back
Top Bottom