At lest for now. Tusubiri huyo mdudu anayeitwa CC. Kuna dalili nyingi sana kuwa mafisadi branch of CCM wameimonopolize, inaweza kubadilisha mambo anytime.
Angediriki kugombea mwaka huu mtandao wangemmaliza, na sidhani kama CC ingekubaliana na hilo. Hapo angekuwa amejiweka mahali pabaya sana. Kama unakumbuka, Dr. Bilal alilaumiwa sana alipojitokeza kugombea mwaka 2005 na bado mwaka huu lilikuwa linaongelewa na baadhi ya wajumbe walitaka jina lake likatwe kabisa kwa kuwa eti alijitokeza 2005 kugombea.
Kilichompa ulaji Dr. Bilal ni mgawanyiko uliopo Zenji, kama NEC ya Zenji ndio wangepiga kura, Dr. Shein asingeona ndani. Sasa ili kuleta mshikamano ndani ya chama ndipo ikabidi jamaa apozwe kwa kupewa umakamu. Siasa za Zenji zinaongozwa na Bara na hasa linapokuja swala la kuteua mgombea urais wa Zenji.
Kwa hiyo turufu kama hiyo Mwandosya hawezi kuitumia huku bara na ndio ilibidi awe mpole. Bado Mwandosya ana nafasi ya kugombea, lakini uwezekano wa kushinda ni mdogo sana kwa kuwa yuko nje ya inner circle ya JK. Na kama angejitokeza mwaka huu ndiyo angewekwa mbali zaidi na kujiharibia kabisa. Subira huvuta heri, may be anaweza kupeperusha bendera ifikapo 2015.
Mkuu achana na haya mambo ya Mwakalinga.
Mwakyembe hakuwa na upinzani wowote zaidi ya kelele tu za kwenye JF, na ata akihamia Chadema na Dr Slaa ahamie Kyela kwa muda wote wa kampeni bado matokeo hayatakuwa tofauti sana na haya, Mwakyembe anakubalika sana Kyela kuliko unavyodhania.
Mwakalinga ni mtu safi lakini huu haukuwa wakati muafaka kwake kugombea Kyela.
Issues za Inner cyles hazikumpeleka JK ikulu. Hakuwa kwenye inner cycle ya Mkapa. Ni upepo tu wa kiuchaguzi na mkakati wa kimtandao. Kwa hiyo siku hizi suala si kuwa kwenye inner cycles, bali ni kwa kiwango gani umetengeneza mtandao wako na unajiamini vipi. Hilo linawezekana, kutoka 2005 mpaka 2015, Prof. anaweza kuendeleza kuimarisha mtandao wake. Na anaweza, kwani watu wa karibu sana ambao walikuwa wanaleta chokochoko, kama Mwakipesile et al. sasa wata-mute. Na hii inatuma ujumbe mzito kwa jamii kuwa,, ahaa kumbe huyu jamaa ni kiboko. Slowly network inakomaa.
Mhh,
Quinine sources zako nimeziheshimu.
Wewe ni kati ya watu wa kwanza kabisa kuleta matokeo hapa JF. Very good job mpiganaji.
Lakini watatakiwa wawe makini sana wakati wakifanya hayo madudu yao. Yanaweza kum-cost Muungwana na sidhani kama yuko tayari kubeba hiyo risk.
Ninakubaliana na wewe kwamba swala la inner circle linaweza lisiwe hoja, lakini naomba uelewe kwamba:
1. Kama JK hakuwa karibu na Mkapa, ilikuwaje Mkapa akachomoa mabilioni kutoka BoT kwenda kufadhili kampeni za JK kuanzia kwenye primaries? Hela za ufisadi zilianza kuchomolewa BoT tangu mwezi May kabla hata hawajaanza primaries na waliofaidika ni hao hao wana mtandao.
2. Kwanini watu kama akina Apson ambaye alikuwa boss wa TISS alikuwa upande wa JK na ilihali alikuwa ni DG wa TISS na hivyo anatakiwa ku-side na Mkapa?
3. Kwanini report ya Mangula kuhusu nominations za wagombea urais na rafu walizocheza iliwekwa kapuni?
4. Kama unakumbuka siku ya Mkutano Mkuu wa CCM pale Chimwaga, Mkapa aliwaambia wapiga kura kwamba chagueni kijana mwenzenu maana anajua matatizo yenu. Unajua kijana mwenzao ni nani?
Baada ya hayo maswali machache bado unaweza kusema kwamba JK alikuwa mbali na Mkapa? Mkapa huyu jeuri tunayemfahamu? Pamoja na mikakati ya mtandao, lakini walipewa access ya kutumia resources za umma kwa matumizi yao na hilo pekee linatoa opportunity kwa mgombea kujiandaa ipasavyo.
Wakati Salim anapakwa matope na magazeti kwamba ni mwarabu na mara sijui ni Hizbu, ulisikia serikali iking'aka? Sumaye alilishitaki gazeti moja kwa juhudi za kwake binafsi, lakini kwa wakati huo serikali ya Mkapa ilishaacha mambo yaende kama yalivyo na hiyo ndiyo kumwachia mtu ajifanyie apendavyo. Mpaka wanatumia Usalama wa Taifa kwa manufaa yao wenyewe, yet utasema hawakuwa kwenye inner circle?
2. Kwanini watu kama akina Apson ambaye alikuwa boss wa TISS alikuwa upande wa JK na ilihali alikuwa ni DG wa TISS na hivyo anatakiwa ku-side na Mkapa?
3. Kwanini report ya Mangula kuhusu nominations za wagombea urais na rafu walizocheza iliwekwa kapuni?
Anyway,tunamsubiri Afande aje atueleze ni wapi alipokuwa anaziokota habari zile zisizoeleza ukweli wa siasa ya Kyela hata chembe!
Mkapa ni chanzo cha matatizo ya mfumo wa sasa, ni mtu pekee aliyejua wazi kuwa ni wapi Tanzania inaelekea lakini alituzira watanzania na kutuacha tuvae mkenge. He knew from the start that JK was not the right choice for Tanzania, he knew all the way that JK alipelekwa mbele ya watanzania na watu ambao hawakluweza kujitokeza wao wenyewe kwa wakati ule kugombea urais, and he knew that will be remotely controlled by mtandao, lakini aliamua kutuzira watanzania.
Bado niko kimya kwa sababu posts za hapa zinategemea zaidi zimetolewa na nani, naye kazitoa wapi. Kwa mfano matokeo ya Kyela yanaweza kuwa na utata unless yamethibitishwa na Afande Samweli, na ndugu yangu Sikonge (huyu alihama kabisa toka kwetu Tabora na akaishia huko Mbeya na kuniacha mpweke nikihangaika na hawa akina Sitta (wote wawili), Selleli, Kigwangalla, na Kapuya na wengineo).
Matokeo mengine ni kwamba Rostam Aziz anaongoza (Igunga),Mohamed Dewji ameshinda (Singida Mjini),Aziz Aboud ameshinda (Morogoro mjini),Peter Serukamba anaongoza kwa margin kubwa (Kigoma kaskazini),Mpesya anaongoza kwa margin ndogo (Mbeya Mjini),Wilbert Lori ameshinda (Karatu),Celina Kombani ameshinda (Ulanga Mashariki),Abdul Mtegete ameshinda (Kilombero),Dr Lucy Nkya ameshinda (Morogoro Kusini).Idd Azzan ameshinda kwenye uteuzi wa Kinondoni.
Kuna Taarifa za Masahihisho kuwa Mama Shamsa Mwangunga ameshinda uteuzi wa Ubungo,hapo awali nilitaarifiwa kuwa Nape Nnauye alikuwa ameshinda,Tuwiane radhi kwa usumbufu wowote uliosababishwa na Taarifa ya awali.Kuna habari zisizothibitishwa kwamba matokeo ya Kawe yamefutwa kutokana na Utata uliotokea kwenye kitabu cha orodha ya uhakiki wa wapiga kura.
Hadi saa sita usiku matokeo yalikuwa Dr Harrison Mwakyembe 7,681; George Mwakalinga 574; Elias Mwanjala 512; Elius Mwakalinga 404 na Rhoda Mwamunyange 171.
Bado niko kimya kwa sababu posts za hapa zinategemea zaidi zimetolewa na nani, naye kazitoa wapi. Kwa mfano matokeo ya Kyela yanaweza kuwa na utata unless yamethibitishwa na Afande Samweli, na ndugu yangu Sikonge (huyu alihama kabisa toka kwetu Tabora na akaishia huko Mbeya na kuniacha mpweke nikihangaika na hawa akina Sitta (wote wawili), Selleli, Kigwangalla, na Kapuya na wengineo).
Kuna taarifa (zinasubiri uthibitisho tu) kuwa Mwakyusa kabwagwa vibaya na Richard Kasesela
That will be good news if transpires to be true. he was like a robbot, remoted by Sauli.