Matokeo mengine ni kwamba Rostam Aziz anaongoza (Igunga),Mohamed Dewji ameshinda (Singida Mjini),Aziz Aboud ameshinda (Morogoro mjini),Peter Serukamba anaongoza kwa margin kubwa (Kigoma kaskazini),Mpesya anaongoza kwa margin ndogo (Mbeya Mjini),Wilbert Lori ameshinda (Karatu),Celina Kombani ameshinda (Ulanga Mashariki),Abdul Mtegete ameshinda (Kilombero),Dr Lucy Nkya ameshinda (Morogoro Kusini).Idd Azzan ameshinda kwenye uteuzi wa Kinondoni.
Kuna Taarifa za Masahihisho kuwa Mama Shamsa Mwangunga ameshinda uteuzi wa Ubungo,hapo awali nilitaarifiwa kuwa Nape Nnauye alikuwa ameshinda,Tuwiane radhi kwa usumbufu wowote uliosababishwa na Taarifa ya awali.Kuna habari zisizothibitishwa kwamba matokeo ya Kawe yamefutwa kutokana na Utata uliotokea kwenye kitabu cha orodha ya uhakiki wa wapiga kura.