Elections 2010 MATOKEO ya kura za awali CCM August 1, 2010

Elections 2010 MATOKEO ya kura za awali CCM August 1, 2010

At lest for now. Tusubiri huyo mdudu anayeitwa CC. Kuna dalili nyingi sana kuwa mafisadi branch of CCM wameimonopolize, inaweza kubadilisha mambo anytime.

Lakini watatakiwa wawe makini sana wakati wakifanya hayo madudu yao. Yanaweza kum-cost Muungwana na sidhani kama yuko tayari kubeba hiyo risk.
 
Angediriki kugombea mwaka huu mtandao wangemmaliza, na sidhani kama CC ingekubaliana na hilo. Hapo angekuwa amejiweka mahali pabaya sana. Kama unakumbuka, Dr. Bilal alilaumiwa sana alipojitokeza kugombea mwaka 2005 na bado mwaka huu lilikuwa linaongelewa na baadhi ya wajumbe walitaka jina lake likatwe kabisa kwa kuwa eti alijitokeza 2005 kugombea.

Kilichompa ulaji Dr. Bilal ni mgawanyiko uliopo Zenji, kama NEC ya Zenji ndio wangepiga kura, Dr. Shein asingeona ndani. Sasa ili kuleta mshikamano ndani ya chama ndipo ikabidi jamaa apozwe kwa kupewa umakamu. Siasa za Zenji zinaongozwa na Bara na hasa linapokuja swala la kuteua mgombea urais wa Zenji.

Kwa hiyo turufu kama hiyo Mwandosya hawezi kuitumia huku bara na ndio ilibidi awe mpole. Bado Mwandosya ana nafasi ya kugombea, lakini uwezekano wa kushinda ni mdogo sana kwa kuwa yuko nje ya inner circle ya JK. Na kama angejitokeza mwaka huu ndiyo angewekwa mbali zaidi na kujiharibia kabisa. Subira huvuta heri, may be anaweza kupeperusha bendera ifikapo 2015.

Issues za Inner cyles hazikumpeleka JK ikulu. Hakuwa kwenye inner cycle ya Mkapa. Ni upepo tu wa kiuchaguzi na mkakati wa kimtandao. Kwa hiyo siku hizi suala si kuwa kwenye inner cycles, bali ni kwa kiwango gani umetengeneza mtandao wako na unajiamini vipi. Hilo linawezekana, kutoka 2005 mpaka 2015, Prof. anaweza kuendeleza kuimarisha mtandao wake. Na anaweza, kwani watu wa karibu sana ambao walikuwa wanaleta chokochoko, kama Mwakipesile et al. sasa wata-mute. Na hii inatuma ujumbe mzito kwa jamii kuwa,, ahaa kumbe huyu jamaa ni kiboko. Slowly network inakomaa.
 
Mkuu achana na haya mambo ya Mwakalinga.

Mwakyembe hakuwa na upinzani wowote zaidi ya kelele tu za kwenye JF, na ata akihamia Chadema na Dr Slaa ahamie Kyela kwa muda wote wa kampeni bado matokeo hayatakuwa tofauti sana na haya, Mwakyembe anakubalika sana Kyela kuliko unavyodhania.

Mwakalinga ni mtu safi lakini huu haukuwa wakati muafaka kwake kugombea Kyela.

Na kwa kweli nilikuwa sijui maneno yale Afande Samwel alikuwa anayatoa wapi;nguvu za Dr Mwakyembe ni kubwa sana Kyela,huwezi kumtoa kwa aina yeyote ile,na kama unakumbuka nilitabiri anaweza shinda hata kwa asilimia 80 kwa kura zote;lkn sasa likely atapata hadi zaidi ya asilimia 90!

Watu wapo mitaani Kyela wakishangilia ushindi wao,na afande Samwel lzm atuambie wana JF maneno yale kama Mwakalinga kambana kweli kweli Mwakyembe alikuwa anayatoa wapi?
 
Issues za Inner cyles hazikumpeleka JK ikulu. Hakuwa kwenye inner cycle ya Mkapa. Ni upepo tu wa kiuchaguzi na mkakati wa kimtandao. Kwa hiyo siku hizi suala si kuwa kwenye inner cycles, bali ni kwa kiwango gani umetengeneza mtandao wako na unajiamini vipi. Hilo linawezekana, kutoka 2005 mpaka 2015, Prof. anaweza kuendeleza kuimarisha mtandao wake. Na anaweza, kwani watu wa karibu sana ambao walikuwa wanaleta chokochoko, kama Mwakipesile et al. sasa wata-mute. Na hii inatuma ujumbe mzito kwa jamii kuwa,, ahaa kumbe huyu jamaa ni kiboko. Slowly network inakomaa.

Ninakubaliana na wewe kwamba swala la inner circle linaweza lisiwe hoja, lakini naomba uelewe kwamba:
1. Kama JK hakuwa karibu na Mkapa, ilikuwaje Mkapa akachomoa mabilioni kutoka BoT kwenda kufadhili kampeni za JK kuanzia kwenye primaries? Hela za ufisadi zilianza kuchomolewa BoT tangu mwezi May kabla hata hawajaanza primaries na waliofaidika ni hao hao wana mtandao.

2. Kwanini watu kama akina Apson ambaye alikuwa boss wa TISS alikuwa upande wa JK na ilihali alikuwa ni DG wa TISS na hivyo anatakiwa ku-side na Mkapa?

3. Kwanini report ya Mangula kuhusu nominations za wagombea urais na rafu walizocheza iliwekwa kapuni?

4. Kama unakumbuka siku ya Mkutano Mkuu wa CCM pale Chimwaga, Mkapa aliwaambia wapiga kura kwamba chagueni kijana mwenzenu maana anajua matatizo yenu. Unajua kijana mwenzao ni nani?

Baada ya hayo maswali machache bado unaweza kusema kwamba JK alikuwa mbali na Mkapa? Mkapa huyu jeuri tunayemfahamu? Pamoja na mikakati ya mtandao, lakini walipewa access ya kutumia resources za umma kwa matumizi yao na hilo pekee linatoa opportunity kwa mgombea kujiandaa ipasavyo.

Wakati Salim anapakwa matope na magazeti kwamba ni mwarabu na mara sijui ni Hizbu, ulisikia serikali iking'aka? Sumaye alilishitaki gazeti moja kwa juhudi za kwake binafsi, lakini kwa wakati huo serikali ya Mkapa ilishaacha mambo yaende kama yalivyo na hiyo ndiyo kumwachia mtu ajifanyie apendavyo. Mpaka wanatumia Usalama wa Taifa kwa manufaa yao wenyewe, yet utasema hawakuwa kwenye inner circle?
 
Mhh,

Quinine sources zako nimeziheshimu.

Wewe ni kati ya watu wa kwanza kabisa kuleta matokeo hapa JF. Very good job mpiganaji.

Mkuu David,kama unazifutailia siasa za Kyela wala hauwezi kuitwa genius kwa kusema Dr Mwakyembe atashinda,kilichokuwa hatukijui ni ushidi wa asilimia ngapi kati ya 70 hadi 90,ukweli ni kuwa aliwafunika sana wapinzani wake kwa kila kitu hata ikafikia pia kupata udiwani lzm uwe kambi yake!kati ya madiwani wote 23 ni mmoja tu Mzee Mujuni wa Kajunjumele ndiye kashinda ingawaje alikuwa timu tofauti na Dr Mwakyembe!

Niliandika wiki iliyopita kuwa Dr Mwakyembe atashinda kwa zaidi ya asilimia 75-80 lkn leo likely akashinda zaidi ya asilimia hiyo na watu Kyela toja mwezi January walikuwa wanajua kabisa kuwa Dr Mwakyembe atashinda kwa kishindo;sielewi maneno na takwimu za Samwel alikuwa anayatoa wapi!

Anyway,tunamsubiri Afande aje atueleze ni wapi alipokuwa anaziokota habari zile zisizoeleza ukweli wa siasa ya Kyela hata chembe!
 
Bado niko kimya kwa sababu posts za hapa zinategemea zaidi zimetolewa na nani, naye kazitoa wapi. Kwa mfano matokeo ya Kyela yanaweza kuwa na utata unless yamethibitishwa na Afande Samweli, na ndugu yangu Sikonge (huyu alihama kabisa toka kwetu Tabora na akaishia huko Mbeya na kuniacha mpweke nikihangaika na hawa akina Sitta (wote wawili), Selleli, Kigwangalla, na Kapuya na wengineo).
 
Lakini watatakiwa wawe makini sana wakati wakifanya hayo madudu yao. Yanaweza kum-cost Muungwana na sidhani kama yuko tayari kubeba hiyo risk.

Mkuu ukiangalia kwa undani Muungwana bado ana struggle ku establish authority ndani ya vikao vikubwa vya chama, hata uenyekiti wenyewe ni kama bado ni hot seat kwake. So anything can happen, i believe mtandao wanaweza kumzidi nguvu, well he is one of them anyway. Mafisadi bado ni formidable force ndani ya CC na NEC, unaweza kukumbuka jinsi walivyotaka ku-deal na Sitta, na still ni members wa NEC na CC ni walewale so you can not expect much from them. Am sure this time kunaweza kukawa na panga kwa baadhi ya wabunge kwa kisingizo cha umoja ndani ya Chama na kwa maslahi ya ushindi wa CCM.
 
Ninakubaliana na wewe kwamba swala la inner circle linaweza lisiwe hoja, lakini naomba uelewe kwamba:
1. Kama JK hakuwa karibu na Mkapa, ilikuwaje Mkapa akachomoa mabilioni kutoka BoT kwenda kufadhili kampeni za JK kuanzia kwenye primaries? Hela za ufisadi zilianza kuchomolewa BoT tangu mwezi May kabla hata hawajaanza primaries na waliofaidika ni hao hao wana mtandao.

2. Kwanini watu kama akina Apson ambaye alikuwa boss wa TISS alikuwa upande wa JK na ilihali alikuwa ni DG wa TISS na hivyo anatakiwa ku-side na Mkapa?

3. Kwanini report ya Mangula kuhusu nominations za wagombea urais na rafu walizocheza iliwekwa kapuni?

4. Kama unakumbuka siku ya Mkutano Mkuu wa CCM pale Chimwaga, Mkapa aliwaambia wapiga kura kwamba chagueni kijana mwenzenu maana anajua matatizo yenu. Unajua kijana mwenzao ni nani?

Baada ya hayo maswali machache bado unaweza kusema kwamba JK alikuwa mbali na Mkapa? Mkapa huyu jeuri tunayemfahamu? Pamoja na mikakati ya mtandao, lakini walipewa access ya kutumia resources za umma kwa matumizi yao na hilo pekee linatoa opportunity kwa mgombea kujiandaa ipasavyo.

Wakati Salim anapakwa matope na magazeti kwamba ni mwarabu na mara sijui ni Hizbu, ulisikia serikali iking'aka? Sumaye alilishitaki gazeti moja kwa juhudi za kwake binafsi, lakini kwa wakati huo serikali ya Mkapa ilishaacha mambo yaende kama yalivyo na hiyo ndiyo kumwachia mtu ajifanyie apendavyo. Mpaka wanatumia Usalama wa Taifa kwa manufaa yao wenyewe, yet utasema hawakuwa kwenye inner circle?

Kwa kuongezea, Mkapa ndiye aliyeondoa jina la Malecela kwa mabavu kutoka kwenye listi ya wagombeaji kwa vile alijua fika kuwa JK asingefurukuta mbele Malecela, kwa hiyo Mkapa ndiye alimnusuru JK asiangamizwe na makucha ya Malecela ndni ya CCM.
 
2. Kwanini watu kama akina Apson ambaye alikuwa boss wa TISS alikuwa upande wa JK na ilihali alikuwa ni DG wa TISS na hivyo anatakiwa ku-side na Mkapa?

3. Kwanini report ya Mangula kuhusu nominations za wagombea urais na rafu walizocheza iliwekwa kapuni?

Mkapa ni chanzo cha matatizo ya mfumo wa sasa, ni mtu pekee aliyejua wazi kuwa ni wapi Tanzania inaelekea lakini alituzira watanzania na kutuacha tuvae mkenge. He knew from the start that JK was not the right choice for Tanzania, he knew all the way that JK alipelekwa mbele ya watanzania na watu ambao hawakluweza kujitokeza wao wenyewe kwa wakati ule kugombea urais, and he knew that will be remotely controlled by mtandao, lakini aliamua kutuzira watanzania. Na excuse yake ni kuwa hataki na hawezi siasa za kiswahili na kihuni. Hata alipokuwa anampigia JK kampeni you could see from his eyes that he knew where we were heading to. it is being said Chagua lake lilikuwa ni mmoja wa watu wake mahiri kwenye mambo ya uchumi, na yeye alifayiwa zengewe zito pale Dodoma karibu azimie.

haha Mangula report and Mangula story most interesting. Actaully i am happy yamemkuta. Kila alipoambiwa ufisadi, ulaghai na ujanja kwenye uteuzi wa wagombea ndani ya CCM alikuwa anakejeli watu. Ripoiti yake was too late, na ipo wenye kabati ya mtu. Na Mtandao wamefanya kila wanaloweza kuhakaikisha kuwa hata ujumbe wa nyumba kumi hapati, jaribu kufuatilia nafasi zote alizogombea uangalie matokeo yake ngazi ya taifa, ngazi ya mkoa, ngazi ya wilaya hata lowest level ameshindwa. Matokeo yakienda tu CC, kuna mtu alikuwa na kazi ya kumanipulate. Na hii system ni yeye mwenyewe aliipigia debe alipokuwa katibu Mkuu, so anastahili kutafunwa na system aliyoiruhsu iwatafune wengine alipokuwa madarakani. And that will be the case hadi awamu ya nne itakapoondoka madarakani.
 
Anyway,tunamsubiri Afande aje atueleze ni wapi alipokuwa anaziokota habari zile zisizoeleza ukweli wa siasa ya Kyela hata chembe!

Mkuu Malafyale,

Kwanza naomba nikukubali kwa analysis yako maana nilikuwa ninafuatilia post zako zote katika mada zile mbili ambazo sijui zilikufilia wapi. Ni zile za mada za Kadi fake 10,000 na Mwakalinga kukamatwa na TAKUKURU. Bahati mbaya mada hizo hazipo tena, lakini kile ulichokiandika ndio hicho ambacho umekirudia tena leo na matokeo ya kura yanaunga mkono analysis yako ya awali.

Sina hakika kama tutamuona tena Afande Samwel, maana alirusha maneno ya ajabu sana na mengine aliyaelekeza kwako kwamba analysis yako ilikuwa based kwenye maongezi ya simu, lakini yeye yuko kwenye uwanja wa mapambano jimboni Kyela. Sasa ukweli umepatikana, next time tukipata watu kama Afande Samwel itabidi kuwa makini.

Huu ushabiki mwingine ambao hauna kichwa wala miguu hauna maana kabisa, na ninakubaliana na wale waliombatiza jina la Comical Ali a.k.a Al-Sahaf aliyekuwa msemaji wa Marehemu Serikali ya Sadam Hussein, maana huyo waziri alikuwa anaona makombora yanashuka lakini bado anadai kwamba wamarekani wanapigwa. Ku-admit kushindwa sio kosa, bali mapungufu ya kimkakati.
 
Mkapa ni chanzo cha matatizo ya mfumo wa sasa, ni mtu pekee aliyejua wazi kuwa ni wapi Tanzania inaelekea lakini alituzira watanzania na kutuacha tuvae mkenge. He knew from the start that JK was not the right choice for Tanzania, he knew all the way that JK alipelekwa mbele ya watanzania na watu ambao hawakluweza kujitokeza wao wenyewe kwa wakati ule kugombea urais, and he knew that will be remotely controlled by mtandao, lakini aliamua kutuzira watanzania.

Mkuu sina ushahidi na hili lakini that is what I have alwayz believed, na kama kuna ishu ambayo Mkapa inabidi alaumiwe vizazi na vizazi ni kutushushia watanzania hili garasha.
 
Bado niko kimya kwa sababu posts za hapa zinategemea zaidi zimetolewa na nani, naye kazitoa wapi. Kwa mfano matokeo ya Kyela yanaweza kuwa na utata unless yamethibitishwa na Afande Samweli, na ndugu yangu Sikonge (huyu alihama kabisa toka kwetu Tabora na akaishia huko Mbeya na kuniacha mpweke nikihangaika na hawa akina Sitta (wote wawili), Selleli, Kigwangalla, na Kapuya na wengineo).

Mkuu Kichuguu,

ha ha ha ha ha ha .... Afande Samwel sijui kama utamuona soon, kama matokeo yangekuwa mazuri (kwamba Mwakalinga ameshinda) basi saa hizi angekuwa hapa anajaza post na maneno ya kejeri.

Sikonge naona ameishampongeza Dr. Mwekyembe, japo sina hakika kama amempongeza baada ya kupata information from a reliable source au kwa kusoma mabandiko hapa jukwaani.

Mpaka kesho mchana watu watakuwa na taarifa kamili za matokeo. Kwa hiyo tuvute subira, japo matokeo siyo final maana NEC na CC bado wanaweza kuyapindua kulingana na mapenzi yao.
 
Hadi saa sita usiku matokeo yalikuwa Dr Harrison Mwakyembe 7,681; George Mwakalinga 574; Elias Mwanjala 512; Elius Mwakalinga 404 na Rhoda Mwamunyange 171.

Afande Samwel hawezi kuja hapa leo kwani wametimka mara baada ya kupata matokeo vituo vichache vya mwanzo. Mtu kama Mwanjala majira ya saa nne usiku tayari alikuwa keshapita Mbeya.

Mwakalinga tulimuonya kutoendekeza wapambe wa jamvini, akatuita wapambe wa Mwakyembe, lakini ukweli ni kwamba hata kuendelea na kampeni hadi mwisho walikuwa na mioyo sugu kwani wananchi waliwakataa, kwenye mikutano ilikuwa Dr Mwakyembe akimaliza kuongea wananchi wanatawanyika, ni pale tu alipowekwa wa mwisho.

Kwenye mkutano wamwisho pale mjini, waliimbiwa nyimbo wakiitwa mafisadi.

Tatizo walijionyesha wazi kuwa wametumwa na kina EL na RA kwani walijinadi kwa kumsifia RC. John Mwakipesile na kueleza wazi kuwa ndiye wanayeshirikiana na ye na kwamba Mwakyembe ni morofi ndio maana hapatani na viongozi akiwemo RC.

Wote wanne hawakusoma mawazo ya wananchi,walishindwa kuelewa kuwa ndugu zao wanampenda kiongozi mwenye misimamo mikali, na kwamba kitendo cha Mwakyembe kuongoza Kamati iliyosababisha Waziri Mkuu kuachia ngazi inafurahiwa na wananchi wa Kyela.

Mwakalinga siasa haiwezi, nimemsikiliza sana ni mtu mwenye jazba, hasira za haraka haraka na kuonyesha chuki kwa mtu anayetofautiana naye.
 
Matokeo mengine ni kwamba Rostam Aziz anaongoza (Igunga),Mohamed Dewji ameshinda (Singida Mjini),Aziz Aboud ameshinda (Morogoro mjini),Peter Serukamba anaongoza kwa margin kubwa (Kigoma kaskazini),Mpesya anaongoza kwa margin ndogo (Mbeya Mjini),Wilbert Lori ameshinda (Karatu),Celina Kombani ameshinda (Ulanga Mashariki),Abdul Mtegete ameshinda (Kilombero),Dr Lucy Nkya ameshinda (Morogoro Kusini).Idd Azzan ameshinda kwenye uteuzi wa Kinondoni.
Kuna Taarifa za Masahihisho kuwa Mama Shamsa Mwangunga ameshinda uteuzi wa Ubungo,hapo awali nilitaarifiwa kuwa Nape Nnauye alikuwa ameshinda,Tuwiane radhi kwa usumbufu wowote uliosababishwa na Taarifa ya awali.Kuna habari zisizothibitishwa kwamba matokeo ya Kawe yamefutwa kutokana na Utata uliotokea kwenye kitabu cha orodha ya uhakiki wa wapiga kura.
 
Yule demu vipi; nasikia alimkwida mtu ili kuimarisha wingi wa kura zake?
 
Yaani kuna wagombea wa CCM nikisikia wameshinda napata faraja sana maana hii itawasadia CHADEMA kushinda kiulaini kama watasimamaisha wagombea wanaokubalika.
 
Hadi saa sita usiku matokeo yalikuwa Dr Harrison Mwakyembe 7,681; George Mwakalinga 574; Elias Mwanjala 512; Elius Mwakalinga 404 na Rhoda Mwamunyange 171.

Kama taarifa hizi ni sahihi, mbona wilaya/jimbo la Kyela lina wanachama wachache sana? Sasa hao wanachama milioni 4 ambao CCM huwa inatutambia kila siku wako wapi?

Margin ni kubwa sana! Hapo hata kama CC wana kinyongo na mshindi sioni kama wanaweza kuwa na jeuri ya kukata jina la mshindi aliyeongoza.

Rafiki yangu Mwakalinga kama ana nia ya kujaribu tena 2015 anahitaji kuanza mikakati ya ushindi kuanzia mwakani mwezi Januari.

Nimekubali maneno ya Dr. Mwakyembe aliyoyasema siku anahojiwa na Mwanakijiji kuhusu juhudi za Lowassa kujisafisha. Alisema kwamba watu wataaibika, kama huo ndio ushindi wenyewe basi alikuwa na haki ya kutamka hivyo.
 
Bado niko kimya kwa sababu posts za hapa zinategemea zaidi zimetolewa na nani, naye kazitoa wapi. Kwa mfano matokeo ya Kyela yanaweza kuwa na utata unless yamethibitishwa na Afande Samweli, na ndugu yangu Sikonge (huyu alihama kabisa toka kwetu Tabora na akaishia huko Mbeya na kuniacha mpweke nikihangaika na hawa akina Sitta (wote wawili), Selleli, Kigwangalla, na Kapuya na wengineo).

ahaaaaaaaaaaaaa Afande Samweli bado kuonekana hapa labda ana fight kubadili matokeo si unajua chama cha majambazi .Si mesikia yaliyo jiri Dar watu wanachana majina ya wapiga kura wengine wana fight back kuzuia upigaji wa kura .
Chadema kuna mambo ya kujifunza hapa CCM will come up swinging you gotta know how to fight "whatever works"
 
Kuna taarifa (zinasubiri uthibitisho tu) kuwa Mwakyusa kabwagwa vibaya na Richard Kasesela

Hizi habari mnazipata wapi Jamani? For your information, Prof. Mwakyusa ameshinda kwa kura nyingi tu. Subiri official news in a few hours time.
 
Back
Top Bottom