Kama taarifa hizi ni sahihi, mbona wilaya/jimbo la Kyela lina wanachama wachache sana? Sasa hao wanachama milioni 4 ambao CCM huwa inatutambia kila siku wako wapi?
Margin ni kubwa sana! Hapo hata kama CC wana kinyongo na mshindi sioni kama wanaweza kuwa na jeuri ya kukata jina la mshindi aliyeongoza.
Rafiki yangu Mwakalinga kama ana nia ya kujaribu tena 2015 anahitaji kuanza mikakati ya ushindi kuanzia mwakani mwezi Januari.
Nimekubali maneno ya Dr. Mwakyembe aliyoyasema siku anahojiwa na Mwanakijiji kuhusu juhudi za Lowassa kujisafisha. Alisema kwamba watu wataaibika, kama huo ndio ushindi wenyewe basi alikuwa na haki ya kutamka hivyo.
Kama msajili wa vyama angekuwa anahakiki wanachama idadi kamili ingejulikana wazi, unaweza kuta CHADEMA, CUF wana wanachama sawa na CCM au hata kuizidi tena kwa mbali