Elections 2010 MATOKEO ya kura za awali CCM August 1, 2010

Elections 2010 MATOKEO ya kura za awali CCM August 1, 2010

Mwakalinga angelishinda bana, ila sema tu Kanda2 alimuahidi LAPUTOPU, na yeye akawaahidi Wanakyela. Sasa mwisho muda umefika, Kanda2 kapotea na Wanakyela wanadai LAPUTOPU, Mwakalinga hana. Kanda2 ndiyo kamponza Mwakalinga. Mtu Mzuri sana wa Mwakyembe huyu.

kanda2 itabidi aseme kwa nini akupeleka laputopu, hizi ni hujuma dhidi ya mwakalinga
 
whatever happened:

Karamagi atarudi kugombea:

Kamala atarudi kugombea:

Chiligati atarudi kugombea:

Naambiwa hawa nimiongoni mwa wenye Chama,
Hata fweza nazo huwa wanajitutumua kukipiga tafu chama.
 
Ha ha haa! This is good news that Mwakyembe has excelled at last.

I am waiting for Mwakalinga to join us here in the forum to say something.
 
Mie Mnyamwezi wa Sikonge weee Kibwengu. Huko Kyela nakusikia tu. Kama huamini basi ngoja nikupe Kinyamwezi cha kwetu Sikonge.

Lilingange, milomo kiti ka Mpaninga kahurumzya.
Lilingange, nda kiti Kabwa kabukalile....... Want more? Kale uvimbe.
Ungelitamani sana niwe mtu wa Kyela, heheheeee!!! Uliye tu.
Hii ni dhahabu ya Sikonge. Au vipi Elnino wa Kukaya?

hh, jana niliwasiliana na Afande Samuel. Jamaa alikuwa kavunjika sana Moyo na ni kweli msimtegemee hapa hivi karibuni. Wako kwenye kuhakiki majina ya waliopiga kura na watu kwenye daftari maana kuna tarakimu zinakataa kulingana ikiwa na maana huenda zile kadi zetu zimeingia mtaani na kutumika jana. Matokeo ya Kyela ni kweli yatajulikana pale Mwakalinga mwenyewe atakaposema kuwa KAJITOWA na kakubali KUSHINDWA na yameisha.

Hiloooooo linaona haya hilooooo

Wewe unayejifanya Sikonge ndiye huyo huyo Afande Sele matusi kwenu ni kama chai sikushangai.

Mwakalinga asimlaumu mtu mchawi wake ni nyie ndugu zake mmemwangusha hamjui siasa zinavyoendeshwa badala ya kujikita jimboni mkabaki kutukana watu na kuwatungia CV za uongo.

Nilimwambia kaka yenu atausikia ubunge kwenye redio kipindi cha bungeni leo mwambieni arudi kubeba mabox sijui aliomba likizo au alitoroka alikwina.
 
Huko Mkoani Kagera kuna Taarifa kuwa Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Nkenge Nazir Karamagi ameshindwa katika uchaguzi wa mwanzo wa kumtafuta Mgombea wa CCM wa Jimbo hilo,pia Waziri anayeshughulikia Masuala ya Afrika Mashariki Dr. Deodorus Kamala amepoteza kiti chake, Mama Asumptha Mshama ameshinda kwenye Jimbo hilo la Misenyi.Huko Iringa Mjini aliyekuwa Katibu Mkuu wa TFF Bwana Fredrick Mwakalebela amemshinda aliyekuwa Mbunge Mama Monica Mbega.

Katika Kinyang'anyiro cha mwaka huu ni Wabunge Wanne tu ambao wamepita bila kuwa na Wapinzani,Wabunge hao wa CCM ni Mizengo Pinda,Benard Membe,Aggrey Mwanri na Ezekiel Maige.

Karamagi anagombea jimbo la Bukoba (V) na siyo Nkenge. Nkenge ni kwa Kamala ambaye tayari kulingana na matokeo rasmi ameshika nafasi ya tatu, hivyo awamu hii ya kura za maoni yuko mbali sana na ushindi wa kupeperusha bendera ya chama chake.

Kwa Karamagi pia si kama matokeo yote tayari yamejumlishwa, la hasha! Kila hila ili/inatumika kumnusuru. Ilikuwa imebaki kete MOJA TU! nayo imetumika jana kuhailisha upigaji kura katika Kata ya Katoro amabo utafanyika leo. Katoro ni eneo wanakotoka Waislam wengi wenye msimamo thabiti na ni karibu na Kwao Karamagi.

Katoro iliachwa kama tairi ya akiba kubadili ushindi mwishoni mwa mchezo lakini morali ya wapigakura ilivyo na wigo uliopo mpaka sasa Karamagi ni sawa na kuku anayejiona kakimbia kifo kwa kuondoka bila shingo!

Ma Tibaijuka (Waziri wa Mambo ya Nje na ......) kakamilisha mchakato wa awali kama taratibu zinavyopaswa kufuatwa wakati Lucy Msafiri kashindwa katika awamu hii. kiujumla Kagera inakuja na sura mpya za wagombea kupitia CCM.

Lingine la muhimu, pamoja na wagombea Ubunge Bukoba (Mjini) kumpunguzia kazi Kagasheki kwa kumaliza mambo mezani na kujitoa, kwa namna ya ajabu uteuzi na kisha ujio wa Dr. Slaa hapa Bukoba unaanza kubadilisha upepo kufanya utabiri wa ushindi wa Kinyang'anyiro cha kiti cha ubunge kuwa mgumu. Awali ilionekana Kagasheki atapeta kwa upinzani wa kadri kutoka kwa Rwakatare lakini sasa Upinzani unaonekana kuzidi kuongezeka na kuimarika.
 
Naam waungwana, matokeo rasmi ya jimbo la nzega kwa wagombea wawili waliokuwa wakichuana sana ni kaam nilivyoandika hapo juu, japo najua kwa kufanya hivi nitaporomoshewa matusi ya kumwaga ila ukweli ndio huo nami binafsi nimeongoza kwa kishindo kura za maoni nafasi ya udiwani
 
hapa mafia mbunge abdulakarim shah buji kamshinda kwa taabu sana mtoto wa mbunge wazamani Omari Kimbau. matokeo ya mwisho ni Buji 1,848 kimbau 1,764 Hafsa 789 na Kipanga 567. Huko kibaha vijijini ibrahim msabaha anapumulia mashine hali mbaya sana taaaaban. na huko mkuranga mh adama malima kwa ulaaaiiini kama ananawa anawagaragaza ulega na kiame
 
Prof Mark Mwandosya kapata kura 4490, Mwakajumulo kura 240.
Katika jimbo la uchaguzi Rungwe Mashariki amemgaragaza vibaya mgombea aliyekuwa anafikiriwa kuwa pandikizi,Mwakajumulo.
Maji yalipomfika shingoni wiki iliyopita Mwakajumulo alisikika akijitetea kuwa safari hii ilikuwa ni kujifunza tu.
Hongera Prof Mwndosya, quite,slow but sure man.
 
Mkapa ni chanzo cha matatizo ya mfumo wa sasa, ni mtu pekee aliyejua wazi kuwa ni wapi Tanzania inaelekea lakini alituzira watanzania na kutuacha tuvae mkenge. He knew from the start that JK was not the right choice for Tanzania, he knew all the way that JK alipelekwa mbele ya watanzania na watu ambao hawakluweza kujitokeza wao wenyewe kwa wakati ule kugombea urais, and he knew that will be remotely controlled by mtandao, lakini aliamua kutuzira watanzania. Na excuse yake ni kuwa hataki na hawezi siasa za kiswahili na kihuni. Hata alipokuwa anampigia JK kampeni you could see from his eyes that he knew where we were heading to. it is being said Chagua lake lilikuwa ni mmoja wa watu wake mahiri kwenye mambo ya uchumi, na yeye alifayiwa zengewe zito pale Dodoma karibu azimie.

Mnamwonea tu Mkapa ndugu zangu. Kumbukeni kwamba Mkapa ndiye aliyemshawishi Salim A Salim agombee Urais, kwakuwa Mkapa alimuaandaa huyo. Lakini akina Mwinyi wakaingilia kati. Na katika mambo ambayo yanamgharimu sana Mangula hivi sasa ni ile attempt yake ya kutaka kumnyima Kikwete form ya kugombea Urais. Jambo ambalo pia liliingiliwa kati na Mwinyi. Na zaidi ya yote, wananchi wengi walikuwa wanampenda Kikwete, kwa hiyo namna pekee ya kumzuia Kikwete asiingie ilikuwa ni kumnyima form, jambo ambalo Mwinyi alilipinga vikali akiwataka CCM waache Kikwete akakataliwe na wananchi. Kitendo cha Kikwete kuingia kwenye NEC tu lilikuwa kosa tayari, kwa kuwa wenye uelewa finyu walimuona Kikwete kuwa ni kiongozi mzuri. Lakini ukweli ni kwamba Mangula na Mkapa walijua fika udhaifu wa Kikwete. I happened to talk personally na mmoja wa viongozi wa juu wa CCM those days akasema wazi kabisa kwamba Kikwete hakuwa chaguo la Mkapa. Lakini kama kiongozi, unatakiwa kusikiliza na kuangalia watu wanataka nini. Kama Mkapa angelazimisha kumuweka Salim si ajabu leo hii tungekuwa tunamlaumu kwamba alituchagulia tusiye mtaka, na pengine yangeweza kutokea machafuko. Na zaidi sana inasemekana kwamba mtandao wa Kikwete ulishapanga kwamba akitoswa tu akimbilie upinzani (more likely CHADEMA). Na wapo waliokuwa wanasema kwamba Nyerere alimuahidi hiyo nafasi Kikwete, hivyo ni lazima apewe. So hakuna sababu ya mtu kumlaumu Mkapa badala yake tujilaumu wenyewe. Mkapa alijali mahitaji yetu.
 
Pole sana mzee shelukindo,naamini kijana ataendelea kukuheshimu na kama atapata kiti hicho cha ubunge basi udhoefu wa muda mrefu ulioupata miaka yote ya utumishi wako selikarini utasaidia kupeleka watu wa bumbuli mbele.
 
Washindi katika baadhi ya majimbo
Mwakyembe (Kyela),Makongoro Mahanga (Ukonga?),Mary Nagu(Hanang?),Ole Medeye (Arumeru),Masha (Nyamagana),January Makamba (Bumbuli),Anthony Diallo (Mwanza?),Mathayo (Musoma),Ole Sendeka (Simanjiro),Richard Kasesera (Rungwe Mashariki),Hussein Bashe (Nzega),Ntukamazina (Ngara),Dr.Batilda (Arusha Mjini),Kimaro (Vunjo),Prof.Mwandosya (Rungwe Magh),Anne Kilango (Same),Nape Nnauye (Ubungo).

Wabunge Maarufu waliokwishapoteza ni Malecela (Mtera),Prof.Mwakyusa (Rungwe Mashariki),Lembeli,Mama Mwangunga na Selelii.

Asafali Shamsa kadondoka, sio msikivu huyu! Huku Moshi, taarifa nilizonazo ni kuwa Moshi mjini kapeta Mhs Buni na huko Moshi Vijijini Mhs Syril Chami kambwaga aliyetumwa na wazee Bwn Mmassy. Taarifa zaidi kufuata.
 
Mijitu ya rosti tamu la azizi utaijua tu
naam waungwana, matokeo rasmi ya jimbo la nzega kwa wagombea wawili waliokuwa wakichuana sana ni kaam nilivyoandika hapo juu, japo najua kwa kufanya hivi nitaporomoshewa matusi ya kumwaga ila ukweli ndio huo nami binafsi nimeongoza kwa kishindo kura za maoni nafasi ya udiwani
 
mchuano mkali haukuwepo basi! ..............
 
Sitegemei kuna mtu atashindana na Mwandosya kule kwa sasa, hata wapinzani wanakiri Mwandosya ni maji marefu. Ni sawa na kutaka kushindana na Magufuli jimboni kwake, unatakiwa kufanya miujiza. Mwandosya japo yuko DSM karibu kila mwezi anapita jimboni kwake kuhimiza maendeleo na anajitolea sana. Sio msemaji sana lakini ni mtendaji mahiri, sayansi kweli anaitumia vizuri.
 
Taarifa za muda huo nimezipata hapa Shigongo kashindwa vibaya sana na Dr. Tizeba


Ila habari kamili ni tarehe 14 ,so hapo ndipo nitakaposema Mengi zaidi..
 
Back
Top Bottom