Elections 2010 MATOKEO ya kura za awali CCM August 1, 2010

Elections 2010 MATOKEO ya kura za awali CCM August 1, 2010

Ndo alianzisha kuita wenzake vuvuzela utadhani kondakta wa daladala. na mara ya mwisho nimemsikia akichangia mjadala wa sheria utadhani anasoma mashairi. OUT!

Sijui kama Mungu atasikia ombi langu la kumuondoa Sita? Ndo kundi linalopigania maisha bora ya wabunge badala ya wananchi. Akipita basi, lakini nitamuombea Lowasa achukuwe kiti cha spika.

Unamwombe mtoto usafi kwa kumwogesha tope?
 
Vipi matokeo ya jimbo la Mwibara, Mh Kajege na Tabora vijini Mh Msekela wamepumua? Ingawaje nyepesi nyepesi wanadai Msekela ambaye ni RC Dodoma alikuwa anapumlia kwenye mashine.
 
Vipi Shigongo? Zile taka taka zake zilikuwa zinaandika upupu kilasiku. Ningekuwa waziri wa habari ningeanza kufungia vile vijarida!
 
Ndo alianzisha kuita wenzake vuvuzela utadhani kondakta wa daladala. na mara ya mwisho nimemsikia akichangia mjadala wa sheria utadhani anasoma mashairi. OUT!

Sijui kama Mungu atasikia ombi langu la kumuondoa Sita? Ndo kundi linalopigania maisha bora ya wabunge badala ya wananchi. Akipita basi, lakini nitamuombea Lowasa achukuwe kiti cha spika.

pole sana!
 
Unashauriwa kuweka jina halafu unauchun, Kama vijembe pelek katika thread nyingine
 
Nasikia Rostam kapita khaaaaaaaaaaaaaaaaaa,ivi waliompigia wanamjua?Au kulikuwa na mapandizi?
Naona nabii amekubalika kwao,uchelewi kukuta ata Chenge kapita

Wasipopita hao unadhani CHADEMA itadondosha nani? Acha ccm ya mafisadi ipite ili isubiri hukumu ya mwisho Oct 31. Acha ngano na magugu vikue pamoja kwani bwana wa mavuno yuko njiani kutenga ngano na magugu.

Oktoba 31!!!!
 
Vipi matokeo ya jimbo la Mwibara, Mh Kajege na Tabora vijini Mh Msekela wamepumua? Ingawaje nyepesi nyepesi wanadai Msekela ambaye ni RC Dodoma alikuwa anapumlia kwenye mashine.

Msekela hana shida, akianguka jamaa atmchagua tena, labda ashindwe na Slaa
 
Duh! kumbe yote yanawezekana iwapo kila mmoja anachukua nafasi yake na kutimiza wajibu. Kumbe kweli tunaweza kulala kuzika huzuni zetu tarehe 31 Oct, 2010 na kuamka next day tunashangilia Tanzania iliyokombolewa! Furaha iliyoje jamani:

Karamagi-out
Masilingi-out
Kamala-out
Lucy Msafiri-out

Haya yote yametendeka Kagera. Na ukigeuka Mbeya nako furaha tele. Sijui Mkoa wa Mara nao itakuwaje?
 
Huko Mwanga, Babati na Hai nako hali imekwenda je?
 
Na January Makamba ameshinda for 85&....Lau Masha ameshinda pia...hahaha C.C.M!....
 
Mwakalebela Iringa,na Kandoro Kalenga

HAPANA MKUU. MATOKEO IRINGA NI KAMA IFUATAVYO;
1. KALENGA. DR. MGIMWA - PRICIPAL WA BANK INSTITUTE MWANZA.
2. NJOMBE KUSINI - ANNE MAKINDA NAIBU SPIKA
3. NJOMBE KASKAZINI - DEO SANGA AU JAH PEOPLE - MKITI WA CCM MKOA WA IRINGA
4. NJOMBE MAGHARIBI - THOMAS NYIMBO MBUNGE WA ZAMANI WA JIMBO HILO NA MFANYABIASHARA.
5. MUFINDI KASKAZINI - MAHMOUD MGIMWA INGAWA J.J. MUNGAI HAKUBALI ANATAKA MATOKEO YASITISHWE NA MAJINA YAHAKIKIWE UPYA. UBUNGE MTAMU.
6. MUFINDI KUSINI- CYPRIAN TWEVE- MWEKA HAZINA WA CCM WILAYA YA MUFINDI.
7. KILOLO - PROF. PETER MSOLLA
8. MAKETE -DR. BINILLITH MAHENGE MBUNGE WA ZAMANI
9. IRINGA MJINI- MWAKALEBELA KATIBU MKUU WA TFF
10. ISMANI- WIILIAM LUKUVI - MKUU WA MKOA WA DSM
11. LUDEWA- DEO FILIKUNJOMBE.

MENGINEYO:

Dr. Slaa atakuwa Iringa kesho saa 4.00 asubuhi. Yatakayojiri mtaarifiwa. Zaidi tutaelekea Mbeya na Ruvuma kuwaletea habari zaidi.
 
You are joking about Shigongo right? Hivi nani anampigia kura mtu kama Shigongo?
Lakini inawezekana ni hapa JF tu ndio undani wa watu kama Shigongo unajulikana.

Mimi, kwa mfano, Shigongo nimemjulia hapa JF. Majarida ya udaku na burudani huwa kwa kweli sisomi zaidi ya mara moja moja kusoma shujaa wangu wa utotoni Madenge na kina Lodi Lofa kwenye Sani. Najitahidi sana kununua magazeti mengine ya kawaida na sijawahi kuona kina Shigongo wa dunia wakijadiliwa vibaya, hata vizuri. Najitahidi kusikiliza runinga na redio ambapo bahati mbaya maskini wachambuzi wetu ndio Marina Hassan na Ephraim Kibonde wa dunia, yani vibonde kweli kweli, huwezi sikia wakijadili vitu kama tabia na hulka za mgombea kinaga ubaga. Na ndio vyanzo vya uchambuzi vya Tanzania ( au sahihi zaidi niseme Dar-es-Salaam, ninapopaelewa zaidi, ambapo ndio Mecca ya habari nchini). Zaidi ya hapo ndio mtandao tena. Sasa Watanzania wangapi wanasoma JF?

Wewe na mimi na wana JF ndio tunajua Shigongo wa dunia ni kina nani.
 
Mramba tena..? :shock:
Usishangae tena kuwa atakuwa waziri. Tena akapewa wizara nyeti, kila mtu anajua kuwa ana kesi, katika hali ya kawaida hakutakiwa kugombea. kama Chadema watakuwa makini, ni vizuri wamwache tu ateuliwe kugombea kwa tkt ya CCM, kwenye kinyang'anyiro cha ubunge anawekewa pingamizi la maana tu.
 
he!!!! si nilisikia kwamba kawe wamebatili matokeo?

Kippi kachukua

@Lembe Kippi hawezi kuitwa fisadi kwa sababu siyo fisadi, kama hamjui Kippi basi omba wadau wakueleze...jamaa ni mpiganaji mwenye msimamo...ndiyo maana wanamtandao hawakumbeba, unlike some of the sponsored wgombea!
 
Kippi kachukua

@Lembe Kippi hawezi kuitwa fisadi kwa sababu siyo fisadi, kama hamjui Kippi basi omba wadau wakueleze...jamaa ni mpiganaji mwenye msimamo...ndiyo maana wanamtandao hawakumbeba, unlike some of the sponsored wgombea!


Mkuu unaweza kufafanua kidogo sponsored wagombea, hasa hawa new blood??
 
Hivi Kippi amefanya nini na anamjua nani na ameishi lini Kawe?

Kippi amejenga nyumba nzuri pale Ununio na anaishi na mke na watoto

Kama hujuai amefanya nini then it's time you started attending those rallies
 
Hatimaye Muiran Rostam Aziz ametimiza kiapo chake alichoapa cha kuhakikisha aliyekuwa Mbunge wa Nzega Lucas Seleli anang'oka na kumsimika Msomali Hussein Bashe. Taarifa za kuaminika zinasema pamoja na kuapa kwa Miungu yake kufaniksha hili, Muiran huyu alitenga zaidi ya mil 500 kufanikisha hili. Na katika siku za mwisho mwisho alikuwa anakwenda mwenyewe au Lowassa jimboni Nzega kusimamia kampeni. Ilifikia hatua hadi maofisa wa Takukuru/Hosea nao kumtumikia RA kwani hata malalamiko ya wagombea kuhusu taarifa ya pesa kuingizwa Nzega siku za mwisho za kampeni yalifumbiwa macho. Pesa hizi ni kama zilimnunua kila mhusika ktk mchakato wa kura za maoni kuanzia Mwenyekiti wa CCM wilaya hadi mhudumu wa CCM wilayani Nzega.

Kuna baadhi ya vituo ambavyo vina matokeo very interesting. Mfano unaambiwa baadhi ya vituo Bashe ana kura 200 na Seleli 0. Ikiwa ina maana hata mawakala wake Seleli nao hawakumpigia. Lingine ambalo ni interesting ni kuwa kila mtu Nzega anajua kuwa Bashe ni kibaraka wa muirani na Lowassa. Iko wazi kuwa ni fate tu ndiyo iliyowakutanisha watatu hawa kwani backgrounds zao ni tofauti sana. Wakati ambapo bashe alikuwa akiutaka ubunge wa Nzega by hooks and crooks, Lowassa na Muiran walikuwa wanakitaka kichwa cha Seleli kwa vyovyote vile tangu Richmond. Sasa baada ya Utatu huu kufanikisha malengo yake kuna uwezekano Bashe akatelekezwa kwani kilichowaunganisha kitakuwa kimekwisha. Wana Nzega inabidi waombe Mungu Rostam/Lowassa asimsahau mbunge/kibaraka wao mtarajiwa kwani vinginevyo aliyoahidi Bashe majukwaani hayatekelezeki na kilio chao kitauzidi msiba. Baada ya Muiran huyu ''kutuchagulia'' Rais watanzania (kwa malengo yake). Safari hii kawakumbuka wana Nzega nao kwa kuwapa Mbunge ''kijana'' (kwa malengo yake). Nadhani sasa anajiandaa ''kutupa'' Spika wa Bunge. Yetu macho!

Hatimaye mkoa wa Tabora umekuwa mkoa pekee wenye wabunge wengi wenye uraia/asili tata. A rainbow ''nation''.

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom