Matokeo ya Maalim Seif Kumtambua Karume

HAYA HAPA MANENO YAKE MWENYEWE MAALIM SEIF SHARIFF HAMAD,WAKATI AKIWAHUTUBIA WANACHAMA WA CUF KATIKA MKUTANO MKUBWA WA HADHARA. ULIOFANYIKA JANA KIBANDA MAITI,MKOA WA MJINI MAGHARIBI,KAMA YALIVYONUKULIWA....
....................................................
"Tulikuwa na mazungumzo na Mheshimiwa Karume naomba mnisikilize vizuri sana hii ni nchi yetu ya Zanzibar kwa zaidi ya karne imekuwa katika misukosuko na huku nyuma wazee wetu wanatwambia walikuwa walikuwa wakiishi vizuri lakini sasa tumekuwa tunaishi roho juu hasa kukikaribia chaguzi" alisema Maalim Seif huku wananchi wakiwa kimya sana.
Alisema baada ya kurejeshwa mfumo wa vyama vingi huko nyuma kulikuwa na mivutano hadi watu kuuawa na kila kukikaribia uchaguzi watu wanakufa, watu wanaumia na enzi zile za siasa za 1961 watu 68 waliuawa na kutokea ghasia na kukafanyika uchaguzi ambao haukuleta matokeo mazuri na jambo ambalo lilisababisha watu kadhaa kupoteza maisha na vitu kuharibiwa.
Alisema kwamba licha ya juhudi za hapa na pale na mataifa ya nje kuingilia hali hiyo haijatengemaa hasa kwa kuwa mazungumzo hayo yote huwa yanafanywa na watu wan je lakini watu wa ndani huwa hawashirikishi bali huambiwa tu lakini sasa watu wenywe wameamua kukaa pamoja na kujadiliana kuweka hali ya usalama nchini.
"Baada ya kuona haya yaliotokea yameshatokea na juzi tulipokutana ikulu tumeulizana hali hii itaendelea hadi lini kuuawa wenyewe kwa wenyewe kudhuriana kwani tumeshapigana vya kutosha tumeshagombana vya kutosha lakini sasa tumesema basi tunataka kuijenga nchi yetu kwa pamoja" alisema Maalim Seif.
Akizungumzia suala hilo Maalim Seif alisema kwa kuogopa dhima mbele ya Mwenyeenzi Mungu wameamua kukaa pamoja na kuleta suluhu ya kudumu hapa Zanzibar kwa kuwa wananchi wamekuwa wakiumia kila ifikapo uchaguzi wamekuwa wakipigwa na kuonewa bila ya kiasi.
"Sisi viongozi wenu mimi na mheshimiwa karume tumekaa na kukubaliana kwamba hali hii itaendelea mpaka lini jamani? tumeona tunadhani njia tunayopita siyo tumeona kwamba tunadhima kubwa mbele ya Mwenyeenzi Mungu na tutakuja kuulizwa kwa kuwaadhibu wazanzibari" alisema Maalim Seif huku akipigiwa makofi kabla kauli iliyowaparaganya wananchi hao haijatolewa.
Hata hivyo alisema hakuna kitu kisichowezekana hasa kwa kuwa kauli za viongozi wa CCM bara walikwishasema suala hilo linaweza kumalizwa na wenyewe wananzibari hivyo hakuna haja ya kuendelea na malumbano yasiokuwa na tija kwa jamii na kuwataka watu wote kukubaliana kukaa pamoja na kuijenga nchi yao.
Huko Pemba mkutano kama huo umefnayika ukiwa na usalama huku wananchi wakiwa wamempokea kwa shangwe kubwa Katibu Mkuu huyo kutokana na uamuzi wa kuingia katika mazungumzo kati yake na Rais Amani.
Wiki hii Maalim Seif Sharif Hamad na Rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume walikutana Ikulu Mjini Zanzibar kwa lengo la kusahau tofauti zao za kisiasa na kujenga mahusiano mema kwa maslahi ya wananchi wote wa Visiwa vya Unguja na Pemba.
Katika mazungumzo hayo ambayo yalichukua takribani sasa mbili wawili hao yaligusia mambo mbali mbali ikiwa ni pamoja na haja ya kudumisha amani na utulivu nchini na maelewano na mashirikiano kati ya wananchi wote.
Viongozi hao wamezingatia haja ya kuzika tofauti zilizopo ambazo zinachangia kuwatenganisha Wazanzibari na kutoa wito kwa viongozi wa vyama vyote vya siasa na wananchi kwa jumla kushirikiana katika kujenga nchi bila ya kujali itikadi zao za kisiasa.
Viongozi hao walifafanua kuwa wananchi wakishirikiana na kujenga nchi kwa pamoja, watapiga hatua kubwa zaidi za maendeleo.Katika mazungumzo hayo, viongozi hao walihusisha umuhimu wa mchakato wa mazungumzo endelevu baina yao na vyama vyao kwa jumla.
SOURCE:ZANZIBAR YETU WEB BLOG.
 
Zitto,

Thats changamoto, nitaitafuta. Ila mie binafsi siamini viongozi wengi wa TZ. Mfano wapinzani kwanini hawaachiani majimbo ya uchaguzi ?, kwanini hawashirikiani? ubinafsi wao unanipa mashaka kaka.

Thats all and Maalim is no exception!


Maalim is an exception!

However upo sahihi na ubinafsi wa wanasiasa wa upinzani bongo. Unajua mwaka 2005 tulipoteza majimbo 48 kwa kutoshirikiana? hebu fikiria tulipoteza zaidi ya viti tulivyonavyo sasa kwa ubinafsi wa kijinga kabisa. Mwalimu aliita hii - stupidity of the highest order
 
Mjengo Mpya Chukwani kule

Good luck mkuu, naona utaendeleza kutimiza usemi wa miafrika ndivyo tulivyo - most of time tunaishi kama vinyonga (kuchukua rangi ya chochote tunachokisogelea karibu).
 


Zitto,

Bahati mbaya au nzuri hatujawahi kukutana. Nipo CCM kama mwanachama, ila sipendi nchi inavyoendelea nina marafiki Chadema na CCM kwetu, ila kweli mnanichanganya nyie wapinzani. Kuna moves ambazo naziona ni right lakini hamfanyi.

Maalim is no exception kwa sababu angalau angeonyesha kufanya hayo.

Sasa believe me kwenye hili la Muafaka kuna kitu kinakuja.

Subiri
 
Nipo bize Mkuu najiandaa kuingia mjengoni 2010 inshallah

Mbona tunajiandaa wengi? ila wananchi watatuelewa bila Takrima? mie nimejipanga kwenda kuwapa ukweli kwanini hawana maendeleo. Kama hawata nikubali poa tu. ila rushwa siwapi.
 
Good luck mkuu, naona utaendeleza kutimiza usemi wa miafrika ndivyo tulivyo - most of time tunaishi kama vinyonga (kuchukua rangi ya chochote tunachokisogelea karibu).
La hasha sikuchagua mwenywe,ni wazee...cant deny them.
Mbona tunajiandaa wengi? ila wananchi watatuelewa bila Takrima? mie nimejipanga kwenda kuwapa ukweli kwanini hawana maendeleo. Kama hawata nikubali poa tu. ila rushwa siwapi.
Mkuu mi napokea kijiti niendeleze mbio...na wazee wakikuita kukupa utumwa wao...ukubali...kwa kuwa mkataa wengi mchawi.
 
La hasha sikuchagua mwenywe,ni wazee...cant deny them.

Mkuu mi napokea kijiti niendeleze mbio...na wazee wakikuita kukupa utumwa wao...ukubali...kwa kuwa mkataa wengi mchawi.

Teh teh teh,

Wazee gani hao waliokupa kijiti? wale wa lumumba au wa wete?
 
Teh teh teh,

Wazee gani hao waliokupa kijiti? wale wa lumumba au wa wete?
Mkuu,nimekudokolea tu,unataka yote,kuna watu weshashtuka...naona vimeseji hapa...nshawambia nawatania tu..he?
LOL kaka haya heri wewe uliyeteuliwa
Mkuu usitowe hata senti tano...uongozi wa kununuwa ni wa kiwoga na kutojiamini...wakiwa na shida watakwita tu.
 
Kwangu kuna ushindani na wananchi hawaelewi, nina kimeo kikubwa kaka
 
Kwangu kuna ushindani na wananchi hawaelewi, nina kimeo kikubwa kaka
Mkuu,usije kuyatoa "mafao ya kustaafu" hayo, watu wako wanaonyesha dalilii za virusi hatari vya H1N1 vya ufisadi...he tutafika kweli?
 
Mkuu,nimekudokolea tu,unataka yote,kuna watu weshashtuka...naona vimeseji hapa...nshawambia nawatania tu..he?

Ukisikia kutojiamini mkuu ndio huku.

Kutegemea vimeseji ili kufanya maamuzi inazidi kuweka sakafu kwenye mtizamo wako na muelekeo wako.
 
Siye twasema Maalim Seif na Prof. Lipumba wametusaliti na kwa hakika hatutokubali kushirikiana na CCM mpaka yale madai yetu ya msingi yametafutiwa ufumbuzi. Hivyo wale wanaodhani CUF tumesalimu amri nawaambia wanaota ndoto za mchana. Mkakati wetu kwa sasa ni kuwang'oa hao vibaraka na kuwa na viongozi wenye nia ya kudai haki zetu.

"HAKI SAWA KWA WOTE"
 
UKWELI HII GOLDEN OPPORTUNITY KWA UPINZANI KUSIMISHA MGOMBEA MMOJA NA KUIANGUSHA CCM .
Fununu zilizopo ni Kuwa PR Lipumba Kamfuata Spika na kutaka agombee Urais kwa kupitia Chama hicho mwaka ujao ila nasikia Spika hajatoa jibu l;olote mapaka mda juu huu ni mpasuko utakao iokoa Tanzania kwa ujumla kwani CCM wamejisahau na kuiharibu nchi yetu.
pia nimeona namna Maalim Seif alivyoyumia karata zake kukijenge jina chama chake katika international community na pia kuweka mazingira bora ya kuingia kwenye uchaguzi ujao hasa ikizingatiwa kuwa CCM iko taabani
Nawapongeza Wazanzibari kwa kuleta peace kwa kujenga nchi yao.

http://dirayetu.blogspot.com/2009/11/maalim-seif-tuiokoe-zanzibar-yetu.html
 
Ukisikia kutojiamini mkuu ndio huku.

Kutegemea vimeseji ili kufanya maamuzi inazidi kuweka sakafu kwenye mtizamo wako na muelekeo wako.
Mkuu mbona mm najiamini tu,sitaki kuwatia hofu wapinzani wangu...mm wa kuumeni bwana,ndo maana wakanitoa huku ninakopata "kikia cha mbuzi" kwa wiki...nikijuwa kumbe wapo 'siriaz'
 
Mkuu, usiwe na munkari utaelewa tu...kila mtu kaumia na utawala wa kimapinduzi zanzibar...Kuanzia Maalim Seif ambaye amefungwa jela na SMZ bila ya kisa chochote, kuja kwa Mzee Ali Haji Pandu...aliyefukuzwa ujaji kwa kusema tu kuwa Maalim Seif hakuwa na kesi ya kujibu, kuja kwa Marehemu Maulid Makame Abdallah aliyehasimishwa na ndugu zake kwa sababu tu ya kukubali haki itendeke...kuja kwa Marehemu Shabaani Khamis Mloo aliyefukuzwa serikalini kwasababu ya kujitenga na batili ya SMZ...kuja kwa akina Machano Khamis Ali na wenzake...waliowekwa ndani miaka zaidi ya miwili na nusu kwa kesi ya kubambikiziwa ya uhaini usio kichwa wala miguu...na kejeli za Salmini Amour juu yao akidai kuwa atawaweka ndani mpaka washike adabu zao na kuwa wao si mapapai kama wataoza huko...kuja mauwaji ya Januari 26/27/01 yaliyoongozwa na aliyekuwa Amri jeshi mkuu wa Tanzania wakati huo Mh. Benjamin Willium Mkapa akisaidiwa na IGP wake ngunguri Omar Mahita kwa wananchi wasio na hatia kwa sababu tu ya kutumia uhuru wao wa kikatiba wa kujieleza na kujikusanya...kufikia na mateso mbalimbali kwa wananchi wa Zanzibar ambao walifanywa kuwa wakimbizi ndani ya nchi yao na nje yake...baada ya kupora haki ya uchaguzi wao...yote haya na mengine ni gharama za demokrasia...Mkuu mpaka USA imekuwa super power leo walipitia katika kipindi kigumu cha historia ya kujenga umoja na mshikamano wa taifa lao ktoka vita vya ukombozi mpaka vita vya wenyewe kwa wenyewe, vita vya haki za kinchi za raia weusi...mpaka hivi walivyo sasa wanajivunia kuwa na taifa lenye nguvu na fahari kubwa za kilimwengu...hayo yote yamejengwa kwa muhanga wa watu waliokubali siku hizo kuachana na siasa za ubinafsi na kujipendelea kuja katika siasa za kupendeleana kama taifa. Leo Maalim Seif kuna watu wanamlaumu kwa hatua hiyo...lakini maneno yake aliyosema yataandikwa kaitka madaftari ya historia kuwa at one time aliwapendelea watu kile alichokipendelea nafsi yake,nafkiri unanielewa hapa,licha ya madhila na manyanyaso aliyopata kwa watawala bado katoa nafasi ya kuvumiliana na kujenga umoja na mshikamano kwa watu wote...kama kisasi yeye anastahili kabisa kulipa kwa uhuni aliofanyiwa na SMZ kuliko yeyote Zanzibar...mbali na kufungwa jela na kufukuzwa nchini na vitisho vya kuwawa,na masimango kwa watu wake,kuna bugdha,dharau hata kwa familia yake,unakumbuka mwaka ule Mkewe Maalim Seif alipouguwa na kupelekwa Hospitali ya SMZ, ya Mnazi moja,masimbulizi aliyopata katika hali yake ya ugonjwa na kukejeliwa mpaka katika vyombo vya habari kisa mumewe mpinzani wa serikali hiyo hiyo ambayo mkewe amekwenda kupatiwa matibabu,kama vile si mwananchi,mlipa kodi,mwenye haki kama raia wengine wa nchi...Mkuu mengi yamepita hayeshi...hapa tunaomba Mungu baada ya muda watu wakishakaa sawa..baada ya kuunda tume ya muwafaka...tuwe na tume ya ukweli na maridhiano...watu wasafiane nia...tusonge mbele...huku tukiwatafutia watoto wetu mambo mengine ya kuwarithisha na si haya ambayo sisi wazee wao kwa miaka zaidi ya 40 tunaendelea nayo...muda wake umepita...tusongeni mbele at least kwa ajili yao...nakubali dosari zipo hapa na pale, hasa katika mambo ya daftari wapiga kura lakini hatua za awali ndo hizo...Tuombe mungu tu Mkuu atuvushe salama katika hatua hii ngumu kidogo kulingana na hali na upepo unavyovuma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…