Junius
JF-Expert Member
- Mar 11, 2009
- 3,181
- 144
HAYA HAPA MANENO YAKE MWENYEWE MAALIM SEIF SHARIFF HAMAD,WAKATI AKIWAHUTUBIA WANACHAMA WA CUF KATIKA MKUTANO MKUBWA WA HADHARA. ULIOFANYIKA JANA KIBANDA MAITI,MKOA WA MJINI MAGHARIBI,KAMA YALIVYONUKULIWA....
....................................................
"Tulikuwa na mazungumzo na Mheshimiwa Karume naomba mnisikilize vizuri sana hii ni nchi yetu ya Zanzibar kwa zaidi ya karne imekuwa katika misukosuko na huku nyuma wazee wetu wanatwambia walikuwa walikuwa wakiishi vizuri lakini sasa tumekuwa tunaishi roho juu hasa kukikaribia chaguzi" alisema Maalim Seif huku wananchi wakiwa kimya sana.
Alisema baada ya kurejeshwa mfumo wa vyama vingi huko nyuma kulikuwa na mivutano hadi watu kuuawa na kila kukikaribia uchaguzi watu wanakufa, watu wanaumia na enzi zile za siasa za 1961 watu 68 waliuawa na kutokea ghasia na kukafanyika uchaguzi ambao haukuleta matokeo mazuri na jambo ambalo lilisababisha watu kadhaa kupoteza maisha na vitu kuharibiwa.
Alisema kwamba licha ya juhudi za hapa na pale na mataifa ya nje kuingilia hali hiyo haijatengemaa hasa kwa kuwa mazungumzo hayo yote huwa yanafanywa na watu wan je lakini watu wa ndani huwa hawashirikishi bali huambiwa tu lakini sasa watu wenywe wameamua kukaa pamoja na kujadiliana kuweka hali ya usalama nchini.
"Baada ya kuona haya yaliotokea yameshatokea na juzi tulipokutana ikulu tumeulizana hali hii itaendelea hadi lini kuuawa wenyewe kwa wenyewe kudhuriana kwani tumeshapigana vya kutosha tumeshagombana vya kutosha lakini sasa tumesema basi tunataka kuijenga nchi yetu kwa pamoja" alisema Maalim Seif.
Akizungumzia suala hilo Maalim Seif alisema kwa kuogopa dhima mbele ya Mwenyeenzi Mungu wameamua kukaa pamoja na kuleta suluhu ya kudumu hapa Zanzibar kwa kuwa wananchi wamekuwa wakiumia kila ifikapo uchaguzi wamekuwa wakipigwa na kuonewa bila ya kiasi.
"Sisi viongozi wenu mimi na mheshimiwa karume tumekaa na kukubaliana kwamba hali hii itaendelea mpaka lini jamani? tumeona tunadhani njia tunayopita siyo tumeona kwamba tunadhima kubwa mbele ya Mwenyeenzi Mungu na tutakuja kuulizwa kwa kuwaadhibu wazanzibari" alisema Maalim Seif huku akipigiwa makofi kabla kauli iliyowaparaganya wananchi hao haijatolewa.
Hata hivyo alisema hakuna kitu kisichowezekana hasa kwa kuwa kauli za viongozi wa CCM bara walikwishasema suala hilo linaweza kumalizwa na wenyewe wananzibari hivyo hakuna haja ya kuendelea na malumbano yasiokuwa na tija kwa jamii na kuwataka watu wote kukubaliana kukaa pamoja na kuijenga nchi yao.
Huko Pemba mkutano kama huo umefnayika ukiwa na usalama huku wananchi wakiwa wamempokea kwa shangwe kubwa Katibu Mkuu huyo kutokana na uamuzi wa kuingia katika mazungumzo kati yake na Rais Amani.
Wiki hii Maalim Seif Sharif Hamad na Rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume walikutana Ikulu Mjini Zanzibar kwa lengo la kusahau tofauti zao za kisiasa na kujenga mahusiano mema kwa maslahi ya wananchi wote wa Visiwa vya Unguja na Pemba.
Katika mazungumzo hayo ambayo yalichukua takribani sasa mbili wawili hao yaligusia mambo mbali mbali ikiwa ni pamoja na haja ya kudumisha amani na utulivu nchini na maelewano na mashirikiano kati ya wananchi wote.
Viongozi hao wamezingatia haja ya kuzika tofauti zilizopo ambazo zinachangia kuwatenganisha Wazanzibari na kutoa wito kwa viongozi wa vyama vyote vya siasa na wananchi kwa jumla kushirikiana katika kujenga nchi bila ya kujali itikadi zao za kisiasa.
Viongozi hao walifafanua kuwa wananchi wakishirikiana na kujenga nchi kwa pamoja, watapiga hatua kubwa zaidi za maendeleo.Katika mazungumzo hayo, viongozi hao walihusisha umuhimu wa mchakato wa mazungumzo endelevu baina yao na vyama vyao kwa jumla.
SOURCE:ZANZIBAR YETU WEB BLOG.