Matokeo ya Maalim Seif Kumtambua Karume

Matokeo ya Maalim Seif Kumtambua Karume

Heeee heeee heeh! Sidhani kama wana nia ya kumvote out! Hali hii inaonyesha kuanza kuamini kuwa hapakuwepo na mpango wa kuwaibia kura zao, kama ilivyokuwa ikitangazwa na wanasiasa wao.

Kibunango, mpango huo bado upo na nitakuletea utekelezaji wake.
 
Licha ya Maalim Seif Kumtambua Karume kama rais halali wa Serikali ya Mapinduzi, Zanzibar, mambo niliyoyashuhudia hapa Pemba kwenye muendelezo wa zoezi la uboreshaji daftari la kudumu la wapiga kura linaloendelea kisiwani hapa, kuna kamchezo makini kanaendelea, na kakikamilika kama kalivyo pangwa, CUF itaangukia pua kwa kupoteza baadhi ya majimbo kisiwani Pemba na kuufuta ule msemo kuwa Pemba ni ngome kuu ya CUF.

Kamchezo kenyewe ni haka...

1. Sheria ya Uchaguzi Zanzibar, inataka lazima uwe na kitambulisho cha ukaazi ili kuandikishwa kupiga kura.
2. Ili kupata kitambulusho cha ukaazi, lazima uwe umeishi mahali husika kwa kipindi kisichopungua miezi 36, kwa lugha nyingine, miaka 3 na Sheha ndiye anayetakiwa kulithibitisha hilo.
3.Sheria hiyo hiyo imetoa mwanya kwa Wafanyakazi, depandants na wajeshi, polisi na vikosi vya SMS kupewa vitambulisho hivyo muda wowote watakapo kuwepo eneo husika bila kuzingatia kipengele cha miezi 36.
4. Wakuu wa polisi, majeshi, wafanyakazi na depandants wanahaki ya kupata vitambulisho vya ukaazi bila kuthibitishwa na masheha wala kuzingatia kipengele cha muda gani.
5. Katika zoezi la uboreshaji daftari unaoendelea sasa, makundi ya watu wengi wao vijana, wanasombwa kwa malozi na kupelekwa vituo vya mbali ili kuandikishwa ambako masheha na mawakala wa maeneo husika hawafahamu, ila wamekuja na barua kuwa wao ni watu wa vikosi vya KMKM na wamekuja piga kambi eneo husika.
6.Sheria ya Uchaguzi Zanzibar unamlazimisha msisimazi kuwaandikisha watu wate atakaotajiwa ni ni polisi au askari wa KMKM hata kama ndio wameingia leo na haim[i mamlaka msimamizi kuuliza idadi halisi ya wajeshi hao, yeye ni kuwapokea tuu, sheha hawawajui, mawakala hawawatambui ali muradi hawajavunja sheria yoyote.
7. Kufuatia hali hii, yale majimbo ya CUF kisiwani Pemba ambako marjin ya ushindi ni ndogo, wameletewa wapiga kura mamluki kwa kisingizio ni wajeshi ili 2010 kusawazisha ile slim difference ya kura za CUF na CCM hivyo CCM kujishindia kiulani.
8. Pia kuna uthibitisho usio mashaka, viongozi wa CUF waliwahamasisha wafuasi wao kususia kujiandikisha na kuleta fuja za kila aina ili kudororesha zoezi zima la uandikishaji kisiwani Pemba na serikali ikiwachukulia hatua, wapeleke kilio chao kwa jumuiya ya kimataifa kuwa uchaguzi sio huru na haki.
9. Wakati CUF wao wakisusa, wenzao CCM wao wala vichwa, kwa kuwahamasisha wafuasi wake kujiandikisha kwa wingi, hivyo uchaguzi ukiitishwa leo, CUF wataangukia pua.
10. Baada ya Maalim kumtambua Karume, wana CUF sasa wanajutia kisuso chao kutaka zoezi lirudiwe. Hata hivyo kwa Seif kumtambua tuu Karume, haitoshi, analazimika kuwa muwazi kwa wana CUF mazungumzo yao ya siri yalihusu nini ili hii michezo michafu inayoendelea kwenye uboreshwaji imalizike rasmi na zoezi liendelezwe kwa uwazi, amani na utulivu.
 
Sioni impact yoyote ya kumtambua Rais ikiwa imebaki mwaka mmoja uchaguzi kufanyika. Karume hawi Rais kwasababu CUF imesema inamtambua. Karume alikuwa Rais pale tume ya uchaguzi ilipomtangaza kama mshindi wa uraisi huko Zanzibar. Sasa Maalim kusema leo anamtambua naona kama ni kichekesho na wastage of time. Angeendelea na msimamo wake tu wa miaka yote minne.
 
'O' issue sio Seif kumtambua Karume, alichofanya Seif ni kumtangaza tuu kumtambua Karume, the really issue ni Seif amezungumza nini Karume?. Kumtangaza ni outcome, what was the motive behind?. Hiki ndicho kinachowaduwaza na fundamentalist wa CUF, lazima aje to the open aseme deal ni nini otherwise moto utamuwakia.
 
Watu wamekifia chama, Maalim anadharau damu zao. Mianasiasa bana aaaaaaghhhhhhhhhhhhhhhhhhhhrrrrrrrrrrrrrrrrrr!!!!
 
Hakuna mapya kati ya hao yanayo tendeka hivi sasa tumeshaona mengi kabla Dr Amani kuwa Rais ,Dr salim Amour( kamando)wakati ule wa muafaka akasema mengi pale ikulu huku akijifuta jasho kwa kihangachifu chake kumaliza tu zile hutuba yule Aduwi wa Mmungu Abdala Rashid akaendelea kuwabomolea watu majumba ,kufukuzw makazini huku akiwadhibu leo sijuwi hata anaishi masha gani,Mmungu anatwambia hatoikataa Dua ya Mwenye kudhulumiwa ,ijapokuwa sisi binadamu tunaharaka hutaka mambo yatokee hapo kwa papo, sasa na haya ya Amani ni sawa na kujambia majini ,masikini Maali seif ameizidi kugeuzwa KARAGOSI ,au naweza kusema amegeuzwa Gari la Ngombe sukani puwa,nafikiri amesahau kauli kubwa za watu wawili wenye Nguvu ndani ya chama na serekali waliosema kuwa Mungu akitaka asitake CCM maisha na yule mmoja aliyesema kuwa Hata Mmungu hana Uwezo wakuijenga Zanzibar kwa siku mia.
 
Kwa kuweka kumbukumbu sawa, uvunjaji wa majumba ulifanyika mara baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 1995. Uvunjaji huu pengine ulisukumwa sana na vujo zilizotokea baada ya matokeo kutangazwa rasmi na tume ya uchaguzi, wacha yale yaliyotangazwa na redio mbao ambayo yalichangia kwa baadhi ya watendaji wakuu wa SMZ kujikuta hawana kazi.

Kulipuliwa kwa Kidatu, kulilifuatiwa na opereshini kubwa ya kuvunja nyumba zote zilizokuwepo karibu na mtambo huo wa umeme(Mtoni Kidatu). Hata nyumba ya Maalim Seif iliponea chupuchupu kukumbwa na bomoa bomoa hiyo.

Baada ya kusafisha eneo hilo, zoezi lilihamia kwa wale wote waliojenga kwenye buffer zone ya umeme wa kidatu, kabla ya kuhamia kwa wale waliojenga kwenye vyanzo vya maji na jirani na kambi za jeshi(JWTZ).

Hawa wote waliorodheshwa na kupatiwa viwanja vya kupimwa kati ya Welezo na Mwera.

Aidha operesheni nyingine ambayo ilihusu zaidi usalama ya wananchi ni ile ya kuondoa watu katika majumba mabovu ya mji mkongwe. Hata hivyo baada ya mafanikio makubwa ya operesheni hii, iligeuzwa kuwa ni ya kisiasa.

Mwaka 2002, Rais Karume aliunda tume ya kuchunguza waliovunjiwa nyumba zao katika eneo la Mtoni Kidatu, hata hivyo matokeo ya tume hiyo sikuweza kuyapata. Na nina hakika hakiweza kuwa na chochote kwani waliovunjiwa katika eneo hilo walipatiwa maeneo mengine yaliyopimwa kisheria.
 
Mwiba yuko wapi? tunahitaji mawazo yako kuhusu hii ishu ya Maalim na Karume!
 
mimi naona liko jambo kubwa na sio hivi hivi tu seif kukutana na karume inamaana seif kurudi 2 ulaya kaenda kwa karume bila ya taarifa au kuna mtu kati ndie alowaunganisha wakutane ihii ishu naona haijazuka hivi hivi lazima umeunda zamani sana ukiangalia karume hendi kwenye sherehe yoyote ya muungano na wala vikao mimi naona ni mapema mno kusema kitu tuangalie tu imani yangu kubwa lipo jambo litatokea muda sio mrefu natabiri kuwa muda si mrefu karume anavunja baraza la mawiziri sinazaidi
 
MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, amewaambia wanachama wa chama hicho mjini hapa kuwa uamuzi wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ( SMZ), Abeid Amani Karume, kukutana na Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad, usiwavunje moyo wa kukipigania chama hicho.

Alisema kukutana huko ni maamuzi yaliyotolewa na Wazanzibari wenyewe kutokana na vurugu za kisiasa zinazotokea kila wakati wa uchaguzi.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini hapa, Profesa Lipumba alisisitiza kuwa chama hicho hakipendi kuona maisha ya wananchi wake yakipotea kila wakati wa uchaguzi kutokana na vurugu na kwamba kimepania kuandika historia.

“Lengo letu ni kuhakikisha amani inakuwepo Zanzibar bila kujali chama gani tumeshirikiana nacho,” alisema Lipumba, “Ndugu zangu wa CUF, tuache kulumbana kuhusiana na uamuzi wa Maalim Seif kukutana na Karume, tujipange kupinga kutawaliwa na mafisadi na walevi wa CCM,” alisema.
 
Tujipange kupinga kutawaliwa na mafisadi na walevi wa CCM hapo hapo na Katibu wako anakutana na hao mafisadi..mbona unachanganya wananchi..we need more explanation??
 
Tujipange kupinga kutawaliwa na mafisadi na walevi wa CCM hapo hapo na Katibu wako anakutana na hao mafisadi..mbona unachanganya wananchi..we need more explanation??

Tulichoweka mbele hapa ni maslahi ya wananchi wa Zanzibar kwanza...Uchaguzi wa vurumai hautatupeleka popote zaidi ya kuwaumiza wananchi wetu wasio na hatia...Angalau najua mimi siwezi kushambuliwa, lakini mwananchi wakawaida atapambanishwa na dola bila hata kufanya hatia, na ataishia kukimbia makazi yake!

Tukishaweka sawa hili, ndipo dhana ya kupinga kutawaliwa na Mafisadi inaanza kufanyiwa kazi...Sijui kama umenielewa...Ahsante.
 
Uko very postimistic na hiyo move..lakini CCM hawatafanya uchaguzi usio na vurumai kama matokeo yanaoonyesha kuwa wao wanaweza ko-lose! lazima walete askari wauua wachukue nchi ..that much we need for decades...
Cha kufanya si kuzungumza na mwizi, mwizi dawa yake ni kumzibiti hata ikibidi kwa kufa watu wake..au yeye mwenyewe ndio atakuwa na adabu..so sera ya jino kwa jino was very right for this scenario..hilo mimi nasema ni kanyaboa!
 
Move ni nzuri ya kuleta amani ya kweli na ya kujivunia! CUF wakiachana na lugha ya "ngangari", "jino kwa jino", "damu itamwagika CUF ikishindwa", nk angalau kitapata kiti kimoja cha ubunge Bara na angalau Marekani na nchi za Magharibi wataacha kusema "uchaguzi ulikuwa huru na haki" baada ya kupewa somo na CCM kwamba CUF ni chama cha kigaidi!
 
Buchanan,
ww U-CCM, unakereketwa nao hasa...somo gani wametowa kwa CUF mafisadi hawa...si wangejipa somo wao wenyewe kwanza kwa kuacha kuwaibia watanzania wanyonge na masikini....kuhusu maelewano hayo, the move was initiated by the Zanzibaris themselves.
 
Back
Top Bottom