Matokeo ya mchujo TAKUKURU: Let's be honest with each other

Matokeo ya mchujo TAKUKURU: Let's be honest with each other

Nafasi nyingi za vyombo vya usalama huwa wanagawana kabla.Zinazobaki ndiyo wanawapa wengine.

Mnakumbuka ule usaili wa TAKUKURU waliofanyia uwanja wa Taifa?Yale majina mliyaona hadi wakatangaza kufuta?Majina yote yalikuwa ya watoto wao na ndugu zao.

Sent from my SM-G950F using JamiiForums mobile app
Mkuu sijaelewa hapo ilikuaje hadi kutangaza kufuta?
 
Yes, kama ni mshahara ule ghafi ukiweka makato, PSSF, NHIF, PAYE mshahara utaobakia mkononi utacheza hapo hapo. Sijui nani anadanganya kuwa hawa watu wanalipwa vizuri. Nina watu wapo huko PCCB ni njaa kali tu. Mkifika kazini ndio mtaaona.
Bongo nyosooo ngoja niendelee kufanya kazi kwa wahindi tu
 
Naanza kwa kusema, poleni mliokosa na hongereni mlioona majina.

Ila tukisema tuangalie uhalisia, naweza sema TAKUKURU haijawatendea haki waliofanya usaili ule. To be fair, why wasingetoa majina na marks kila mmoja alizopata, huku wakiainisha cut-off points?

Tuachane na lile swala la baadhi ya majina kujirudia zaidi ya mara moja, hivi, how can we measure the transparency of the process?

Wametumia muda mwingi kuandaa haya majina, ila bado wamechemka pakubwa, maana mpangilio sio mzuri na unamakosa kibao.

Jumanne ya tarehe 04/01/2022 kuna dogo aliniombaga ushauri juu ya hizi application. Kilichokuwa kinamsumbua ni kwamba kuna mzee alimwambia mpaka kufikia ile siku (jumanne), nafasi zilizokuwa zimebaki wazi for everyone zilikuwa 10 out of 200 ( upande wa afisa uchunguzi).

So aliambiwa na yule Mzee atoe around 4 million ili aweze kupatiwa nafasi, na alikuwa guaranteed kupata as long as jina lake lilikuwepo kwenye list ya walioitwa kufanya mtihani hata kama hatoenda Dom kwenye pepa ya mchujo. Me nilichomshauri ni kwamba asitoe hiyo hela, aende tu kufanya mtihani wa mchujo.

Ila am sure now atakuwa anajilaumu kuniskiliza, maana ile hela uwezo wa kulipa alikuwa nao. Even kwa upande wangu baada ya kuona namna results zilivyorudi, napata hisia kuna possibility yule Mzee alikuwa anajua anachokiongea, something is smelling fishy here.

Anyway, kuna 3 questions ninazo:

1. Nasikia kwenye paper waliandika number, why takukuru wametumia nguvu kubwa kuconvert numbers into majina, wakati ilikuwa simple kurudisha results kwa number?

2. Cut-off point ilikuwa ngapi na ufaulu ulikuwaje?

3. Why hawaja-display attained marks za participants wote?
Mh mkuu kama una ushahidi wa ilo la rushwa ya 4 M kwann msi file case ili mchakato urudiwe
 
Sio kuita kazini,ni kuita kwenda Mafunzoni (Depo) CCP Moshi,lakini uzuri ukienda Depo unakuwa unalipwa Posho mwisho wa mwezi nadhani Laki 200,000 au 300,000,vijana mtakaoenda mkapige mchakamchaka na kwata vizuri mmalize m-pass out salama mje muijenge Nchi.
Salary ya investigation officer ni how much?
 
Sio kuita kazini,ni kuita kwenda Mafunzoni (Depo) CCP Moshi,lakini uzuri ukienda Depo unakuwa unalipwa Posho mwisho wa mwezi nadhani Laki 200,000 au 300,000,vijana mtakaoenda mkapige mchakamchaka na kwata vizuri mmalize m-pass out salama mje muijenge Nchi.
-hao makanjanja tu, na ndiyo maana Takukuru wanashindwa kesi nyingi Sana kutokana hawaajiri kwa merits,
 
Haya majina baana Kuna jamaa yangu nimememuona mpaka nimecheka, form four alipata div 4 ya point 32 tulimaliza nae shule 2011, lakini alipita njia za certificate mpaka akawa na degree ya Sheria, Mzumbe Mbeya kwa uwezo wake ule wakuunga unga nahakika kwenye mtihani uliokua umejaa hesabu zaidi ya 50% asingeweza kupita maana hesabu alikua na F , lakini mzee wake alikua RPC Miaka ya nyuma nashangaa kumuona hapo. Poleni ndugu Zangu mliochoma nauli, karibuni kwenye ujasiliamali unalipa sana, kuliko huko TAKUKURU
mzee kuteleza sio kuanguka, kuna watu waliyumba na baadae wakakaza wakatoboa fresh tu. nimeona watu ambao hawakuwa na ufaulu mzuri sekondari lakini chuo wakatoka na gpa nzuri tu na kuna watu walifaulu vizuri sana sekondari afu chuo wakatoka deki. Vitu hubadilika
 
Back
Top Bottom