Matokeo ya mchujo TAKUKURU: Let's be honest with each other

Matokeo ya mchujo TAKUKURU: Let's be honest with each other

Mungu anasema mali na vyote vijazavyo Nchi ni mali yangu na anasema nijarubuni kwa matoleo yenu muone kama sitawanyeshea mvua ya Baraka. Mungu hajawahi kuniacha hata katikati ya simba wakali mimi nikiwa kondoo nilitoboa...Asante Yesu
Ulitoboa kivipi mkuu?
 
Nakumbuka kuna dada nilikuwa nachat naye telegram siku moja kabla ya usaili aliniambia vitu kama hivi
Alisema yeye ameapply na ameitwa kwenye aptitude test ila hawezi kuja kwa sababu kuna mtoto mmoja wa kigogo fulani (yeye anamjua) tayari ana nafasi yake licha ya kutofika kwenye usaili so hawezi Kupoteza nauli kwakuwa ameshaona kuna viashiria vya kuwepo kwa majina yaliyoandaliwa kabla ya usaili
Duuuuuh inaumiza sana.
 
Tafuta mali uwe na connection then ndo uzae watoto baadae uje wafanyia connection waishi vizuri waache wale mema wazazi wao na connection zao zinafanya kazi
Asilimia kubwa ya watu wanaouawa vifo vya kikatili ukifuatilia utagundua nao waliwahi kuua hapo kabla. Kwa nje huonewa huruma na watu wengi kuwa wamekufa vifo vibaya, ila on back side wamepata malipo yao. Hakuna kitokeacho kwa bahati! Huu mfano ukitumia akili utauelewa. Nice day!
 
Hao TISS watu wanawasifia tu ila wana maisha ya kawaida sana, nje ya safari ni weupe sana kwa mwezi wanapata kama 1.1M inclusive everything.

Kuna kipindi nilidate na watu wa huko kusema ukweli nilimsaidia vitu vingi maana ikifika katikati ya mwezi hana kitu yaani mweupe pyee kama karatasi

Same applies to PCCB officer baada ya makato yote anapokea kama laki saba hivi.
We' uli date na mgambo sio TISS, koma.
 
Sio tu vita bali ajira yenye maslahi mazuri. Kwa level za mishahara ofisi inayolipa 1.7m au zaidi maslahi ni mazuri. Humo kuna hata wafanyakazi wengine wamekimbilia humo kuhonga ili wapate chance imagine unatoka ofisi unayolipwa laki 7 gross mpaka ofisi ya kulipwa 2.2m kwanini usipambane?

Wazazi wanaumiza vichwa sana mtoto umemsomesha anazeekea nyumbani hata kuoa hataweza maana hata kazi ya maana ya kulisha mke hana. Kwanini usihonge kama inawezekana mwanao apate kazi
Hapa nimekuelewa kaka.
 
mishahara ya takukuru imekaaje kwa wachunguzi ?
 
CARDLESS tumia busara,sio suala la wote kuitwa,inachotakiwa ni HAKI,si sawa watoto wa maskini watumie gharama kusafiri kutoka makwao mpaka Dodoma,gharama za malazi na chakula halafu nafasi wapewe watoto wa wakubwa ambao hata kuhudhuria Usaili hawakuhudhuria,hii si sawa. Chombo kama TAKUKURU kikiwa KICHAFU wakati kipo Kisheria kupambana na mambo MACHAFU ni aibu
mi naamini haki ipo hadi
 
Majina ya watakaofanya oral ya pccb yalitoka yakiwa na changamoto kadhaa ikiwemo watu kurudiwa rudiwa mara mbili ,hilo walikuja wakalitolea majibu ,tunaomba pia mtolee majibu na hili kwa mtu ambae hakuitwa Written Interview Ila jina lake limetoka kwenye Oral interview ?View attachment 2120090View attachment 2120091
mbona hao wote unao wataja hawapo kwenye list ya walio itwa oral au umeamua kupotosha umma
 
Back
Top Bottom