Black billionaire
JF-Expert Member
- Oct 16, 2018
- 455
- 526
Nitafatilia kijana ,Shikamoo Mkurugenzi Mkuu Salum Hamduni
Mimi ni kijana niliyekuwa miongoni mwa vijana tuliofanya Usaili tarehe 8 January, 2022 na majibu yametoka juzi. Ulitokea mkanganyiko ambapo jina langu lilitoka kwenye list ya WACHUNGUZI WACHUNGUZI (waombaji wenye Degree) wakati mimi niliomba nafasi ya WACHUNGUZI WASAIDIZI (maana nina Diploma).
Kutokana na mkanganyiko huo,niliambiwa na Wasimamizi nifanye Mtihani wa Wachunguzi Wasaidizi lakini nikitumia namba ya Mtihani niliyopewa kwenye list ya WACHUNGUZI.
Na kwa kuwa sikuwa peke yangu niliochanganywa nafasi, tuliambiwa na Wasimamizi kwamba Mitihani yetu itawekwa Pending kusubiri maelekezo mengine.
Licha ya kuamini kwamba nilifanya vizuri Mtihani ule, jina langu halijatoka pamoja na majina ya wengine wote tuliokumbwa na kadhia ya kuchanganywa nafasi tulizoomba, hivyo tunaamini mkanganyiko uliojitokeza ndio uliosababisha majina yetu yasitoke.
Kwa HESHIMA NA TAADHIMA, tunakuomba Mkurugenzi Mkuu ufuatilie suala hilo.
Ubarikiwe sana
Pole sana.