Matokeo ya sensa 2022 yanaonesha kila mwaka Watanzania wanaongezeka watu 1,800,000 kuanzia mwaka 2012

Matokeo ya sensa 2022 yanaonesha kila mwaka Watanzania wanaongezeka watu 1,800,000 kuanzia mwaka 2012

peno hasegawa

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2016
Posts
14,255
Reaction score
23,949
Sensa ya wayu na makazi ya mwaka 2012 Tanzania ilikuwa na watu 44 milioni ambapo sensa ya mwaka 2022 watanzania wamehesabiwa na kupatikana watu 62 milion.

Kwa hesabu hii, inaonyesha 62m ~ 44m = 18m
18,000,000/miaka 10 = 1,800,000

Kwa mantiki hii kila mwaka kuanzia mwaka 2012 hadi 2022 wanazaliwa watanzania 1,800,000 pamoja na kuwepo kwa janga la covid -19 na matatizo mengine ya kimaisha.

Tujadili idadi hii ya ongezeko la watu kila mwaka kama ni ndogo au ni kubwa kwa mwaka.
 
Hiyo idadi ni kubwa. Mafanikio pekee ya CCM toka tupate uhuru ni hayo maana maeneo mengine yote wameshindwa.
 
Ongezeko Hilo ni kubwa Sana Mkuu, kwa hesabu yako ukiileta kwa lisaa inaonesha tangu 2012 kwa saa moja wanazaliwa watoto 60.
 
Ukikokotoa hesabu za kuzaliwa kwa watanzania kuanzia mwaka 2012 hadi 2022, Ninahisi matokeo ya sensa 2022 yanafanana na matokeo ya uchaguzi mkuu 2020.
 
Katika kipindi cha Dakika 45 kinachorushwa na chanel ya ITV tarehe 16 May, 2022, Kamisaa wa Sensa Anna Makinda alihojiwa kuhusu zoezi la sensa, na moja ya kitu alichoelezea ni bajeti ya Sensa, ambapo alisema bajeti ya Sensa kwa mwaka 2022 ni Tsh bilioni 629.

Kimahesabu Watanzania kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 wapo watu 61,748,120 watu hawa walihesabiwa kwa gharama ya Tsh 629 bilion kwa wote.

Kwa maana hiyo Tsh 629,000,000,000 gawanya kwa watanzania 61,748,120 = 10,186

Maana yake kila mtanxania alihesabiwa kwa gharama ya Tsh 10,186.

Tujadili tafadhali
 
Haraka ya nini? Subiri analysis. Aidha kumbuka ni kama mtu alipita kwenu 2012 akakuta watu 5 wakazaliwa 3 wakahamia 5 wakafa 2 wakaolewa 4 akarudi tena 2022 akahesabu na kusema nyumba hii tangu mwaka 2012 ameongezeka watu wawili tu. Hii ni sawa?
 
Haraka ya nini? Subiri analysis. Aidha kumbuka ni kama mtu alipita kwenu 2012 akakuta watu 5 wakazaliwa 3 wakahamia 5 wakafa 2 wakaolewa 4 akarudi tena 2022 akahesabu na kusema nyumba hii tangu mwaka 2012 ameongezeka watu wawili tu. Hii ni sawa?
Subiri analysis tangu 23 August, 2022 hadi leo 1 Nov, 2022?

Tuambieni pia kiasi cha fedha za sensa ya watu na makazi zilibaki kiasi gani au kama ziliisha zote ni sawa tu ila nilitarajia Rais akitangaza matokeo ya sensa angetangaza kiasi cha fedha zilizotumika na zilizobaki ili zifanye kazi zingine.

Yeye kasoma idadi ya watu na kumaliza mambo. Sensa watu walipiga fedha sana saba
 
Ukichukua gharama ya kumuhesabu kila mtanzania ukagawa kwa idadi ya maswali yaliyoulizwa kwenye zile fomu za usahili utajua kila swali limeghalimu kiasi gani.

Sasa ukilinganisha na ughali wa teknolojia iliyotumika unaweza kujua kama hivi kuna haja ya kutumia teknolojia iliyotumika ama laa?

Pia, wastani wa gharama ya kila swali inaweza kutumika kama bei elekezi kwa vijana au watu wanaoulizwa maswali mbalimbali na watu wengine kwa kazi au kuwaelekeza mambo mbalimbali.

Mfano, nielekeze kwa fulani ni wapi au hivi wewe umeoa au bado, hivi asha leo utakuja au hauji, au wanasiasa wanapouliza hivi mtanichagua?

Maswali yote haya na mengine ya namna hiyo yanaweza kuanza kulipiwa ili kupunguza usumbufu na kuongeza tija kwasababu bei elekezi tayari itakuwepo.
 
Subiri analysis tangu 23 August, 2022 hadi leo 1 Nov, 2022...
Una wazimu si bure!!!! Uliza matokeo ya sensa hutumia muda gani hadi kupata idadi ya watu (Total Population). Hii imekuwa ya kwanza (uliza UNECA watakueleza ndo maana Chinganya jana alikuwa Dodoma kufifia kazi nzuri iliyofanyika na kugharamiwa na serikali kwa zaidi ya asilimia 90, ni rekodi katika Africa). Unadhani kazi ya takwimu ni rahisi kama ufikiriavyo? Kwa sensa hii, Samia (binafsi) ameupiga mwingi!
 
Back
Top Bottom