Katika kipindi cha Dakika 45 kinachorushwa na chanel ya ITV tarehe 16 May, 2022, Kamisaa wa Sensa Anna Makinda alihojiwa kuhusu zoezi la sensa, na moja ya kitu alichoelezea ni bajeti ya Sensa, ambapo alisema bajeti ya Sensa kwa mwaka 2022 ni Tsh bilioni 629.
Kimahesabu Watanzania kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 wapo watu 61,748,120 watu hawa walihesabiwa kwa gharama ya Tsh 629 bilion kwa wote.
Kwa maana hiyo Tsh 629,000,000,000 gawanya kwa watanzania 61,748,120 = 10,186
Maana yake kila mtanxania alihesabiwa kwa gharama ya Tsh 10,186.
Tujadili tafadhali