Matokeo ya Stars Kocha katuchomesha

Kamgomoli

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2018
Posts
1,896
Reaction score
4,058
Ndani ya dk 90 Kocha bora anapimwa kwa upangaji wa kikosi,kusoma vzri mbinu za timu pinzani na kufanya mabadiliko sahihi( Substitution).

Kocha wetu alianza kulikoroga kwenye kupanga kikosi cha kwanza. Sielewi kwanini aliamua kuwapanga Bacca na Novatus kucheza kati. Japo walicheza vzr lakini ni hatari kufanya mabadiliko ya kiuchezaji hasa eneo muhimu la kati kwa wachezaji ambao hawajawahi ku-pair na kuchezaji kwa pamoja.

2. Kosa jingine.Nilitegemea baada ya Shabalala kutoka ( aliumia) basi angeingia Mwamnyeto ili arudi acheze na Bacca aafu Nova angeenda kushoto. Cha ajabu akamuingiza Luhende ambae kusema ukweli mechi ilimuelemea. Uganda walikua fiti sana hasa kipindi cha pili.

3. Kosa la tatu.Baada ya Himid Mao kuumia na kutoka, aliamua kumpeleka Job eneo la kati km kiungo mkabaji wakati sikumbuki ni lini job amewahi cheza hiyo nafasi hata akiwa Yanga. Pamoja na ubora wa Job huwezi kujaribisha wachezaji kwenye mechi ngumu na nzito ya Uganga.

4 Akaendelea kufanya Sub mbovu tena. Akamtoa Mzamiru na kumuingiza Fei ambae hana mechi "fitness" tena akampa jukumu la kukaba.

5.Na mwisho akaharibu kabisa kwa kumtoa Samata. Watu wengi hawajui umuhimu wa Samata uwanjani. Uwepo Samata ulikuwa unawafanya mabeki wa Uganda kua na tahadhari muda wote. Ndio maana hawakuwa wakipanda kwenda mbele.Baada ya Mbwana kutoka kocha wa Uganda alipunguza kiungo akaongeza washambuliaji. Hapo ikawa ndo turning point ya mchezo.

Nafahamu Watanzania huwa tunamaneno yetu Ooh Uganda hatuwawezi,Sisi hatuna wachezaji,Mara wanasiasa wametuharibia timu sawa kila mtu ana uhuru wa kusema anachodhani, Ila kwa jana mimi binafsi naona kocha katuchomesha kwa kiasi kikubwa. Alifanya mabadiliko mengi ya nafasi za kiuchezaji bila sababu za maana. Kocha yeyote duniani huwa habadilishi ovyo timu ya ushindi( Winning team). Mfano mzuri ni Simba ukimtoa Chama tu mambo huwa yanabadilika.

Kuna mechi za kujaribisha wachezaji lakini si mechi na Uganda inayotafuta matokeo ya hali na mali.

Sasa tumejiweka kwenye hali ngumu mno kwenda Afcon. Kwa jinsi mechi zilivyo naona Uganda akitoboa.Hakika Tumelikoroga! Kwenu wachambuzi wenzangu wa mchongo[emoji1]
 
Atleast angeena norvatus ni mido heavy duty
 
Mbona ninyi mlishinda jama, kufungwa ni mchezo pia.Halafu wanasiasa wakishajiingiza tu kwenye timu huwa inafungwa sijui kwanini hamjifunzi.
Hapo hutowaona tena wanasiasa wakiendelea kuisapoti starz,,,ikifanyaga vizuri huwaga kila mwanasiasa anaibuka kutengeneza jina na ahadi kedekede,,,Na hapo ndipo tunapokoseaga sana kwenye swala la michezo kuingiza siasa za kipuuzi puuzi!!!
 
Hapo hutowaona tena wanasiasa wakiendelea kuisapoti starz,,,ikifanyaga vizuri huwaga kila mwanasiasa anaibuka kutengeneza jina na ahadi kedekede,,,Na hapo ndipo tunapokoseaga sana kwenye swala la michezo kuingiza siasa za kipuuzi puuzi!!!
Kocha kapanga kikosi vizuri mara ya kwanza walipoingia wakamweka kapombe mara tshabalala.Kama waliokuwepo hawakushinda mwanzoni.Ujinga ujinga.
 
Haujui mpira wewe
Pair ya Nova na Bacca imecheza vizuri almost mechi nzima
Mwamnyeto alikua na kadi mbili za njano
Coach ndo anaekua uwanja wa mazoezi anawaona wachezaji wake
Ni kweli walicheza vzr ila madadiliko aliyoyafanya nadhani kubalansi team basi ni bora Job angerudi katikati aafu kulia angecheza kapombe. Nova angeweza kusogea kiungo au kwenda pembeni kushoto. Angalau timu ingekaa vzr.
 
Angalau wewe umongea points tupu bila dharau au kuwatukana wachezaji wetu
 
TFF na kocha wao, wote ni wahuni tu. Na kwa pamoja wanahudika kwenye kuihujumu timu yetu ya Taifa.

Kwanza Fei toto hakustahili kabisa kuitwa timu ya Taifa. Unawaacha akina Sure Boy, unamuacha nje Sospeter Bajana! Unamchezesha mchezaji ambaye hana hata timu anayochezea!! Ujinha wa ajabu kabisa huu.
 
Wanasiasa wa Tanzania ni watu fulani wa hovyo sana tena sana tu. Wameshindwa kujishughulisha na maswala muhimu ya maendeleo na sasa wanakuja kuvuruga mpira.

Uchumi kila siku unazidi kuporomoka lkn wanakwepa na kujificha kwenye mpira ambapo pia hamna wanachofanya ila ni kuharibu tu, ina maana wachezaji hawajui jukumu lao uwanjani ni nini mpaka wahahidiwe pesa na hizo pesa zimepitishwa katika bajeti gani?

Wanasiasa waache kujitafutia umaarufu wa kijinga kwenye mpira baada ya kushindwa kushughulikia matatizo muhimu ya nchi.

Very hopeless political opportunists masquerading for leaders.
 
Kwa forward ile ambayo kila aliyekuwa akipata mpira anaangalia chini na kuanza kukimbia na mpira bila kuangalia wenzake, tusingepata ushindi hata tungeendelea kucheza mpaka asubuhi hii.

Mechi zote mbili tulicheza kwa kukamia ila bila mbinu ya maana ya ushindi. Pia ingetusaidia zaidi kuwapunguzia pressure wachezaji kwa kuicheza mechi kule kule Misri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…