Kamgomoli
JF-Expert Member
- May 3, 2018
- 1,896
- 4,058
Ndani ya dk 90 Kocha bora anapimwa kwa upangaji wa kikosi,kusoma vzri mbinu za timu pinzani na kufanya mabadiliko sahihi( Substitution).
Kocha wetu alianza kulikoroga kwenye kupanga kikosi cha kwanza. Sielewi kwanini aliamua kuwapanga Bacca na Novatus kucheza kati. Japo walicheza vzr lakini ni hatari kufanya mabadiliko ya kiuchezaji hasa eneo muhimu la kati kwa wachezaji ambao hawajawahi ku-pair na kuchezaji kwa pamoja.
2. Kosa jingine.Nilitegemea baada ya Shabalala kutoka ( aliumia) basi angeingia Mwamnyeto ili arudi acheze na Bacca aafu Nova angeenda kushoto. Cha ajabu akamuingiza Luhende ambae kusema ukweli mechi ilimuelemea. Uganda walikua fiti sana hasa kipindi cha pili.
3. Kosa la tatu.Baada ya Himid Mao kuumia na kutoka, aliamua kumpeleka Job eneo la kati km kiungo mkabaji wakati sikumbuki ni lini job amewahi cheza hiyo nafasi hata akiwa Yanga. Pamoja na ubora wa Job huwezi kujaribisha wachezaji kwenye mechi ngumu na nzito ya Uganga.
4 Akaendelea kufanya Sub mbovu tena. Akamtoa Mzamiru na kumuingiza Fei ambae hana mechi "fitness" tena akampa jukumu la kukaba.
5.Na mwisho akaharibu kabisa kwa kumtoa Samata. Watu wengi hawajui umuhimu wa Samata uwanjani. Uwepo Samata ulikuwa unawafanya mabeki wa Uganda kua na tahadhari muda wote. Ndio maana hawakuwa wakipanda kwenda mbele.Baada ya Mbwana kutoka kocha wa Uganda alipunguza kiungo akaongeza washambuliaji. Hapo ikawa ndo turning point ya mchezo.
Nafahamu Watanzania huwa tunamaneno yetu Ooh Uganda hatuwawezi,Sisi hatuna wachezaji,Mara wanasiasa wametuharibia timu sawa kila mtu ana uhuru wa kusema anachodhani, Ila kwa jana mimi binafsi naona kocha katuchomesha kwa kiasi kikubwa. Alifanya mabadiliko mengi ya nafasi za kiuchezaji bila sababu za maana. Kocha yeyote duniani huwa habadilishi ovyo timu ya ushindi( Winning team). Mfano mzuri ni Simba ukimtoa Chama tu mambo huwa yanabadilika.
Kuna mechi za kujaribisha wachezaji lakini si mechi na Uganda inayotafuta matokeo ya hali na mali.
Sasa tumejiweka kwenye hali ngumu mno kwenda Afcon. Kwa jinsi mechi zilivyo naona Uganda akitoboa.Hakika Tumelikoroga! Kwenu wachambuzi wenzangu wa mchongo[emoji1]