Matokeo ya 'supplementary' DIT, wengi wamefeli

Matokeo ya 'supplementary' DIT, wengi wamefeli

A JUSTMAN

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
439
Reaction score
555
Matokeo ya mitihani kwa supplementary ya Dar es salaam istitute of technology yametoka jana tarehe 17, kwa idara zote matokeo yamekua mabaya sana maana kwa diploma wengi wanarudia mwaka "retake" na discontinued.

Wale wa shahada ya uhandisi wengi wamecarry na discontinued nyingi pia. Mfano diploma ya computer engineering first year, pass ni 60, retake 8, abscond 16, disco 18 hapo walianza pamoja ni 102. Information technology pass 26, retake 3, abscond 20, disco 14, kutoka 63.

Karibuni kwa maoni
 
Nashukuru Mungu nimechomoka na nimemalizana nao.

Electronics and Telecommunication Engineering (ETE).
 
Hapo kwenu Tele perfomance imekuaje toa takwimu tuone pia

Niliingia pale stationary nikaangalia namba yangu nikaona matokeo yamekuwa poa nikaondoka nikaendelea na mambo yangu mengine town.
 
Next time kama huna cha maana usini-Quote.

Sihitaji hongera yako.

Kaa mbali na mimi. Utanitafutia ban bure.

We nani hata hivo uliulizwa ndo swali shauo nyingine bwana change ua attitude usisingizie ban kupongrzwa dhambi acha shauzi
 
Hivi bado ile lugha ya "JUCHE" inatumika hapo DIT?. Ha ha ha...Chuo langu hilo bana!.
 
Matokeo ya mitihani kwa supplementary ya Dar es salaam istitute of technology yametoka jana tarehe 17, kwa idara zote matokeo yamekua mabaya sana maana kwa diploma wengi wanarudia mwaka "retake" na discontinued. Wale wa shahada ya uhandisi wengi wamecarry na discontinued nyingi pia. Mfano diploma ya computer engineering first year, pass ni 60, retake 8, abscond 16, disco 18 hapo walianza pamoja ni 102. Information technology pass 26, retake 3, abscond 20, disco 14, kutoka 63.Karibuni kwa maoni

Hivi kwanini vyuo vya elimu ya juu Tanzania failures zinakuwa nyingi sana? Kama selection ya kujiunga na chuo ilifanyika vizuri, darasa lenye watu 63 pass ni 26 tu ina maana tatizo liko kwenye ufundishaji.

HAIWEZEKANI uwe na percentage kubwa namna hii ya failures kama ufundishaji unaeleweka na mtihani ni fair.

Halfu basi bado hata hao walio-pass uwezo wao bado ni majanga.
 
Vyuo vya kibongo mwanafunzi ukifeli ndio malecture wanafurahi wanajiona wapo vizuri kitaaluma.

Poleni wahanga lakini pia juhudi binafsi zinahitajika ili kufanya vyema kwenye masomo.
 
Hivi bado ile lugha ya "JUCHE" inatumika hapo DIT?. Ha ha ha...Chuo langu hilo bana!.

Itakuwepo tu. Vipi block 5 au 1? Ha ha ha! Kuna president mmoja wa DITSO wakati ule miaka ya 1999/2000 Eng Richard Ojendo jamaa alikuwa kichwa sana. Itakumbukwa miaka hiyo hela za wanafunzi wa elimu ya juu zilikuwa zinatolewa na Wizara ya Sayansi Teknolojia na Elimu ya Juu.

Nakumbuka yeye na wenzake wa kutoka UDSM walidokeza wanavyuo kote nchini kuwa kuna kitu kinaandaliwa kinaitwa Cost sharing.

Wengi hatukuelewa nini maana yake. Jambo hilo lilisababisha mgomo wa vyuo vyote vikubwa vya Elimu ya Juu nchi nzima mwaka 2000/2001.

Wengi wa viongozi wa serikali za wanafunzi walisimamishwa vyuoni kwao.

Nilikuja kugundua huyu jamaa alikuwa kichwa ambapo wengi hatukumuelewa ilipofika mwaka 2005 ilipoanzishwa Loan Baord ambayo ndo ile Sera ya Cost Sharing.

Ninachokusudia hapa ni kuelezea ni huyu jembe Richard Ojendo( P Eng- Civil) , ni moja ya jembe lililotoka pale DIT. Huyu kwa sasa ni miongoni mwa Local ambae ni Top Menejiment ya Geita Gold Mine.

Comments zake na mijadala anayoitoa kuhusu Uhandisi utakubali kuwa jamaa ni jembe.

Hongera EX DITSO President Eng Richard Ojendo. Eng Dr Richard Masika ambae alikuwa ni Director of Studies ( kwa sasa ni mkuu wa TCA- Arusha) na Prof Kondoro wanamjua Ojendo mwanaharakati hodari kabisa pale DIT.
 
Matokeo ya mitihani kwa supplementary ya Dar es salaam istitute of technology yametoka jana tarehe 17, kwa idara zote matokeo yamekua mabaya sana maana kwa diploma wengi wanarudia mwaka "retake" na discontinued.

Wale wa shahada ya uhandisi wengi wamecarry na discontinued nyingi pia. Mfano diploma ya computer engineering first year, pass ni 60, retake 8, abscond 16, disco 18 hapo walianza pamoja ni 102. Information technology pass 26, retake 3, abscond 20, disco 14, kutoka 63.Karibuni kwa maoni

Muda Mwingi Mnazurura Tu Barabarani Na Mnajifanya Wanaharakati Na Tunagongana Sana ktk Nyumba Za Kulala Wageni MKIGEGEDANA Je Mtafaulu Vipi Na Huwa Mnasoma Saa Ngapi?

Hizo Kozi Zenu Zinataka Umakini Mkubwa Sana Na Siyo UPOPOMA.
 
Matokeo ya mitihani kwa supplementary ya Dar es salaam istitute of technology yametoka jana tarehe 17, kwa idara zote matokeo yamekua mabaya sana maana kwa diploma wengi wanarudia mwaka "retake" na discontinued.

Wale wa shahada ya uhandisi wengi wamecarry na discontinued nyingi pia. Mfano diploma ya computer engineering first year, pass ni 60, retake 8, abscond 16, disco 18 hapo walianza pamoja ni 102. Information technology pass 26, retake 3, abscond 20, disco 14, kutoka 63.Karibuni kwa maoni

Abscond=Disco=Incomplete
 
Muda Mwingi Mnazurura Tu Barabarani Na Mnajifanya Wanaharakati Na Tunagongana Sana ktk Nyumba Za Kulala Wageni MKIGEGEDANA Je Mtafaulu Vipi Na Huwa Mnasoma Saa Ngapi? Hizo Kozi Zenu Zinataka Umakini Mkubwa Sana Na Siyo UPOPOMA.

Hivi harakati katika kudai haki yako ni jinai mkuu?
 
Back
Top Bottom