Matokeo ya uchaguzi CCM chipukizi: Mtoto wa msanii Shetta na Mwigulu Nchemba wang'ara

Matokeo ya uchaguzi CCM chipukizi: Mtoto wa msanii Shetta na Mwigulu Nchemba wang'ara

Huu ni ufalme na umwinyi tuukate na kuhakikisha CCM inangashushwa, pamoja na vyama vyote vya upinzani, tunahitaji mapinduzi katika ulimwengu wa siasa.
 
Hiki kizazi kinachokuja ni tofauti na chetu mkuu.

Jamaa wanajiamini na wanauliza almost kila jambo, hawatakubali kuburuzwa.

Haya unayoyaona sasa yataishia kizazi hiki ila trust me huo ujinga hautakuwepo huko mbeleni.
wajuaji ndio hao wanaandaliwa na kujengewa msingi wa kujizatiti uongozini kwa kupewa mbinu za mapema za kuongoza, waburuzwaji kama kawaida hawana habari hata kidogo, wametulia tuli nadhani wanaandaliwa kulalamika kama wazazi wao,

Hata ivo wakati huo hawatajua hata wanalalamikia nini
 
CCM kutolewa madarakani ni kazi sana mkuu, jamaa wana mipango miaka 30 mbeleni.
Wataondoka tu hizi ni mbwembwe , na ni bahati mbaya watoto kama hawa wanaalibiwa future zao wakifikili ccm itakua pale, wenda mbele wangekuja fanya maamuzi sahii kwa chama ambacho kitakua madarakani, ni kilaza pekee anaweza kuexpose mwanao kwa umri huu kwenye siasa,

Na wanaoangaika ni wajinga wa chini huko, hivi wanafikili kikwete, Mkapa , Mwinyi senior, Mwl Nyerere hawana wajukuu?
Na kama wapo lini umewasikia wakijiusisha na ujinga wa namna hii, watoto wapo huko wanapiga vitabu, nakupata connection za dunia, kama ni Uongozi siku ikifika wataingia kwenye ulingo kupambana
CCM kutolewa madarakani ni kazi sana mkuu, jamaa wana mipango miaka 30 mbeleni.
 
CCM kuitoa bila machafuko nchini ni ngumu. Yani bila wananchi kuamua kumwaga damu ili kizaliwe chama kipya kitachofuata misingi mipya kikatiba tutaendelea kuwa hivi hivi for foreseeable future😂
Inatakiwa akili na si kumwaga dam.mbona nchi zilizoendelea wanatoana madarakani na hawamwagi dam?tunahitaji kuwa wastaarabu tu.anaetwala awe mstaarabu,vyombo vinavyosimamia Haki wawe wastaarabu basi.tatizo cc waafrika ustaarabu bado sana.ndo mana mzungu aliita bara hili DARK CONTINENT kwa SABABU ya matendo YETU,hatuna TOFAUTI NA wanyama Pori.
 
Hiki kizazi kinachokuja ni tofauti na chetu mkuu.

Jamaa wanajiamini na wanauliza almost kila jambo, hawatakubali kuburuzwa.

Haya unayoyaona sasa yataishia kizazi hiki ila trust me huo ujinga hautakuwepo huko mbeleni.
Hiviiii, vyama vingine tofauti na CCM, vinaruhusiwa kufanya haya wafanyayo CCM, kuhusiana na watoto? Jana, wamewakusanya watoto mpaka zaidi ya saa tano usiku!
Na Nchi hii, inaruhusu watoto kujihusisha na siasa?
 
Kukaa mpaka saa tano kuna taarifa yoyote ya maafa uliisikia?
 
Nzuri sana. Lkn sisi waislam tusisahau kuwasimamia watoto mafunzo ya kiislam ili waweze kujitambua na kujielewa wao ni nani na kwanini wakaumbwa na baada ya kufa nini kitafata. Haya mengine ukifumba jicho tu hakuna tena msaada.
Kitu kizuri kumuachia mtoto ilmu ya dini yake.
LEO NI HAYO. AU NAKOSEA WADAU?
Umeongea point
Ugomvi wangu tu kufumbia kosa kwa kumlinda wa dini yako.
Hiyo ni mbaya. Kemea ubaya bila kubagua aliyefanya ni nani.
Kama ambavyo tunakemea mauaji ya pande zote tena ya wasio na hatia ule mgogoro kule basi tukemee hata tunaowaunga mkono wanapokosea. Wala si kujitweza bali kuonyesha ustaarabu. Kuendelea kujaribu kutetea kwa kupindisha mambo inaleta ukakasi
 
CCM Watolewe madarakani na nani?, au CCM itoke halafu aje nani? kwasababu Tanzania hatuna upinzani makini!. Hiki Chuma kilipoingia tuu, tukawauliza watu humu Je, Kasi ya Magufuli itaua Upinzani Uchwara na Kuimarisha Upinzani Makini? - Prof. Kitila Mkumbo kisha tukawauliza tena Upinzani wa Tanzania ni Upinzani Makini wa Kweli, au ni Upinzani Uchwala?. Kasi ya JPM Itaua Upinzani Uchwala na Kuibua Upinzani Makini wa Kweli Au..? jibu likawa ni Tanzania hatuna upinzani wowote makini na wa maana wa kuing'oa CCM, hivyo tukawaeleza watu ukweli halisi wa kitu kilichopo ni CCM only and only CCM hivyo Kupata maendeleo ya kweli, Watanzania ni lazima tujifunze kuukubali ukweli!. Hili la CCM kutawala milele ni kweli!. kwasababu CCM sio tu ni chama tawala, bali pia ni chama Dola! na kufuatia members wengi humu wamejiunga juzi juzi, angalieni hili la CCM kutawala milele, tumeanza kulizungumza lini Watch TBC Live!. " William Malecela na Ndoto ya CCM Kutawala Miaka 50!. na Wenye Matumaini na Upinzani Kushika Dola! Sahauni! CCM Inajiandaa Kuua Kabisa na Kuuzika Jumla Chuma kilipoingia utekelezaji wa hili ulifanyika The Economist: Rais Magufuli ametangaza kufuta Upinzani ifikapo 2020 na kuirudisha Tanzania kuwa Nchi ya chama Kimoja watu walikuwa na mategemeo sana na Chadema, tukawaeleza ukweli kuwa Chadema hakuna kitu pale Je, CHADEMA inaweza kushinda 2020? Is it serious, credible & mature enough opposition?, kama vitu vidogo tuu kama Handling of Serious Security Issues: Kama CHADEMA Takes Things For Granted Kwa Uzembe Hivi!, Jee Ikulu Yetu Wangeiweza?.

Ila pia msikate tamaa kabisa, uchaguzi Mkuu wa 2030 bado kuna fursa Uchaguzi mkuu wa mwaka 2030, ndio mwanzo wa mwisho wa CCM! Wajinga karibu wote watakuwa wamemalizika!
P
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] tayari umeshakujaa, yaan huchelewii wee.
Mzee. Khaaaah
 
Nzuri sana. Lkn sisi waislam tusisahau kuwasimamia watoto mafunzo ya kiislam ili waweze kujitambua na kujielewa wao ni nani na kwanini wakaumbwa na baada ya kufa nini kitafata. Haya mengine ukifumba jicho tu hakuna tena msaada.
Kitu kizuri kumuachia mtoto ilmu ya dini yake.
LEO NI HAYO. AU NAKOSEA WADAU?
Na sie tutawafunza kula kitimoto na bia
 
Qayllah Nurdin Bilal, ambaye ni mtoto wa msanii wa Bongofleva, Shetta (Hutaniwa wamefanana na Kova), amechaguliwa kwa kishindo kuwa Mwenyekiti wa Chipukizi Taifa katika Chama cha Mapinduzi (CCM) leo Dodoma.Qayllah amepata kura 303 kati ya kura halali 429 zilizopigwa

View attachment 2848650

Isack Mwigulu Nchemba ambaye ni mtoto wa Waziri wa Fedha Dkt Mwigulu Nchemba is ametangazwa kuwa mshindi wa Ujumbe wa Baraza Kuu La UVCCM Taifa

View attachment 2848651
Upuuzi tu
 
Nzuri sana. Lkn sisi waislam tusisahau kuwasimamia watoto mafunzo ya kiislam ili waweze kujitambua na kujielewa wao ni nani na kwanini wakaumbwa na baada ya kufa nini kitafata. Haya mengine ukifumba jicho tu hakuna tena msaada.
Kitu kizuri kumuachia mtoto ilmu ya dini yake.
LEO NI HAYO. AU NAKOSEA WADAU?
Elimu ya dini NI yakipumbavu na kudumaza akili hii Elimu ya kijamii ndiyo muhimu mara 1000 kwa vijana wetu
 
Back
Top Bottom