Jamani tafadhali!...
Unajua kuna uongo unaokaribia ukweli kiasi kwamba hata sisi huku tulo mbali tunaweza kukubaliana nao..
Haiwezekani watu kumpigia kura diwani, mbunge kisha wasimchague rais wa chama hicho hicho hata yule diwani au mbunge mwenyewe lazima kura yake itakuwepo kumchagua rais wa chama chake. Kuna mahala nasoma kura zero sijui moja hivi kweli hatadiwani, mbunge, mwenyekiti na viongozi wa chama hicho au wasimamizi wa chama kituoni hawakukichagua chama chao?. Pia sii rahisi mtu kumchagua rais wa chama fulani akamwacha diwani na mbunge wake pamoja na kwamba yawezekana na wapo wengi wamekusudia kufanya hivyo..
Kwa hiyo nilitegemea sana kuona watu wakichagua Madiwani naWabunge wa CCM lakini kura za Urais wakimpa Dr.Slaa lakini sii rahisi mtu kumchagua diwani wa chama hiki kisha mbunge wa chama kingine na rais wachama kingine tena..
Hizo hapo hesabu juu kidogo zinanipa shida ingawaje yawezekana lakini sii kwa mbumbumbu Wadanganyika.
Ni mtazamo wangu...