JK ameshatangaza kuwa mwaka huu ni mwaka wa siasa,na kama ndio hivyo tutegemee tusichokipenda hivi karibuni.Mimi nashangaa kashfa kibao hazijashughulikiwa yet bado mtu anaongoza kwa asilimia 70 we are not serious.
Hata kama sensization ya mambo ya siasa imefanyika matokeo haya yanaonyesha kuwa uelewa wa watanzania bado ni zero kwani hawajaweza kupambanua sifa dhabiti za kiongozi.
Kashfa ya ndege ya Rais, kashfa ya Rada, Meremeta, wizi wa BOT, Kagoda, Deep Green Finance, Richmond, IPTL, Kiwira, mabomu ya mbagala, ufujaji wa hela halmashauri, matumizi makubwa ya serikali inluding magari ya kifahari yanayotumika hivyo,bila kusahau safari za JK ambazo hazijaonyesha tija yoyote kwa Taifa nk.
Yaani yote hayo hapo juu hayajatolewa maelezo ya kina kwa wananchi kutosheleza kiu yao,isitoshe JK hajaonyesha uongozi wa dhati kukabiliana na mambo hayo yet anapata asimia 70 na chama kinaonekana kuwa karibu na wananchi,huu si usanii huu.
Haya ndiyo mambo yatakayoendelea kuanzia sasa mpaka wakati wa uchaguzi kuwabrain wash wadanganyika wasahau yale yote yaliyotokea huko nyuma.Kazi kubwa ipo kuwaelimisha wadanganyika walio wengi ili kuepukana na utapeli huu wa kisiasa ambao sasa umeanza kufanyiwa kazi.