Matokeo ya Utafiti: Kikwete, Freeman Mbowe, Zitto, Killango, Jerry Silaa na Dr Slaa

Jambo kubwa hapa ni kutumia vyombo vya Habari na pia wangejaribu kuuliza ni nani fisadi kati EL na RA maana tunachanganyikiwa na kuona ni chama gani kinkumbatia ufisadi katika Taifa nletu maana kuna kila dalili za kama yale ya mwaka 2005 kujirudia mwaka huu katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu
 

Si kila utafiti unapofanyika lazima ukubalike unaweza kufanya utafiti say laboratory ukaja na matokeo 100% lakini ukiyaweka kwenye real situation/practical utafiti huo una fail sasa kwa utafiti kama huu kwamba Kikwete ni kiongozi mzuri kwa 75% still wengi tunaona bado kuna mambo mengi ambayo yanasubiri utekelezaji lazima hata wewe mfanya utafiti u-doubt usipo query utafiti wako basi utakuwa mwenyewe una matatizo

au inawezekana unaujua ukweli kuwa it cant be possible lakini unalazimisha watu waukubali kwa maslahi fulani na hii ipo hata kwenye madawa watu wanafanyia utafiti nyani au panya kwa matumizi ya binadamu zinapotumika wakati mwingine huwa zina kuwa na side effects lakini wana force kwa ajili ya biashara zao.
 
Hongera Zitto, Hongera CHADEMA na watu wote makini katika taifa letu nyingi ndio mulifanya miaka yote siasa ziwe na changamoto kubwa sana. Karibuni wengine katika ulimwengu wa siasa
 
hayo ni maoni yako ukiwa kama kada wa ccm tuondolee uchafu wako kwenye jf , kiwete nani anmuhitaji kwenye taifa hili labda ccm wasiyo ona mbali kama wewe

Mkuu Kilewo haya si maoni ya mwanaJF anayejiita Habarindiyohiyo ni matokeo ya utafiti wa kampuni ya Synovate kwa hiyo unamwonea bure HNH badala yake ungempa thanks kwa kutuletea and then utoe comments zako kuhusiana na utafiti wenyewe
 
ndiyo hivyo mojwapo ya maswali ambayo wangetupa tuelewe ni kuwa ni wangapi wana jiconsider kuwa ni mashabiki au wanachama wa CCM..
...tena wangeuliza kama hao waulizwaji kama wanafahamu ni kitu gani kinachompa chati JK.

jamani huu ushabiki wa kinafiki unapaswa kukemewa kwa JINA la Yesu maana hawa SYNOVATE na REDET ni payee wa system ili kuwaweka sawa watawala kwamba wanapendwa kwa kuiweka nchi rehani.

Huwezi kufanya utafiti wa questionaire kwa watoto wa kindergarten wasiojua ABC za tafiti
 
Hivi ni lini Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi itakemea huu upuuzi na ujinga unaoendelezwa na shule za chekechea pamoja na za msingi na za sekondari kuwavika majoho na kofia watoto wanaomaliza shule hizo kwamba eti watoto hao ni "graduates"?

Watoto hao watakapomaliza vyuo vikuu wavalishwa nini? Nikumbuka wakati sisi tukiwa Chuo Kikuu, miaka ya 1960s, hata undergraduates hawakuwa wanavaa kofia!!!!!!!!!!!
 
Sijakuelewa mzee unaongelea kuhusu nini hapa na pia kuna nini kama watu wakivaa kofia hata kumi??
 

...technically, percentages could be significantly misleading if not associated with the degree of chance, thi 70% (p<=> 0.X) in accordance with their sampling. In the upshot, a significantly large sample, minus appropriate factors and a bit of talk about normal distribution (large population sample surveyed), Chebuyschev Central Limit might just apply. Otherwise, SYNOVATE and their figures ought to be discarded.
 
Baba
Unajua waandishi wetu ni kama wanafunzi wanaosemowa insha kisha haooo wanakimbilia newsroom. Hawana maswali yanayojijenga kichwani yenye mantiki. ndo maana tunawaita maripota njaa kali. kwa mwandishi makini hawezi akaitwa kwenye conference kisha akasomewa upuuzi kama huu wa SYNOVATE bila ya kuuliza maswali chechemizi yatakayosisimua ripoti hiyo.

Ni kama waliitwa kwenye hafla fupi wakasomewa risala kisha haooo wakawahi newsroom kupaste walichoambiwa
 
...sasa kama wananchi waliulizwa 90% walikuwa wanachama wa CCM, unategemea nini?
na idadi kubwa ya watanzania wanaipenda na kuitukuza CCM(hata kama sio wanachama).naunga mkono matokeo ya utafiti huu kwani yanaegemea kwenye ukweli ingawa ukweli unauma).
Utafiti huu ni janga kuu kwa watanzania wazalendo wa kweli kwani unathibitisha hofu yangu kuwa kuindoa CCM madarakani ni ndoto labda ichukue miaka mingine 1000.
Ujinga wa jamii yetu ndio mtaji wa CCM.Binafsi napendekeza MAPINDUZI ingawa wengine mtataka kunipiga mawe
 
tutasikia mengi mwaka huu na subiri lazima REDET watoe ripoti ya utafiti karibia kabisa na uchaguzi na wataonyesha kikwete na ccm yake eti wanapendwa kwa 110%
 
Hapa mseme tu mnataka Jerry Silaa asikike au ajulikane. Anakuwaje mbunge maarufu wakati wala si mbunge na bado hajatangaza anagombea na kama ametangaza ni kwenye forum ipi na hao watanzania 1000 wa nchi nzima wamepataje taarifa?
 
Yaani huu ni uhuni, wewe huwezi kuhoji watu 2000 kati ya watu milioni 40 halafu unaita ni utafiti. Naona hapa taaluma ya tafiti imemeingiliwa vibaya. Pia unaposema chama kilichopo karibu na wananchi ni kwenye nini? Ufisadi, Majengo pacha ya BOT, EPA, kushuka kwa elimu ya kidato cha nne, usofu wa waalimu, huduma mbovu hospitalini, barabara mbovu? Au ni kwenye kitu gani?
Pili mbunge kuongea kwa ukali haimfanyi kua bora, kuna waliofanya mambo mazito na wafuatiliaji wazuri wa kazi zao Mfano DR Magufuli, Dr. Mwakiyembe, Dr. Slaa, mbona hawa hamkuweka kwenye tafiti zenu mlizoandika?
Ili utafiti ukamilike na uweze kuutumia kufanyia maamuzi ni lazima huhoji watu wa kutosha na wenye uelewa wa hayo mbambo. Mtu ameishila la sana ni lazima atakwambia Rais anaongoza akimaanisha anaongoza nchi au safari za nje, wewe unaweka kama anaongoza kwa kufanya vizuri.
Huu utafit warudie na watuhoji tulioenda shule ili tutoke maoni. Hili taifa bwana, yaani hata wafaya tafit zimefisadiwa?

Utafit wao warudie kwani Hauna TBS, haujapitiwa na wasomi ili kujua kama kanuni za tafiti zilifuatwa. Pia ikumbukwe tafiti kama hizi wanatakiwa waseme walitumia Shs ngapi kukusanya data

Yaani mpaka wachina wametuingilia kwenye tafiti, Eee Mola tuepushe na balaa hili.
 
At the risk of sounding very Nigerian, NONSENSE!!

Haya madudu wanayofanya wanayajua wenyewe and the dudus inside their thieving minds.
 
...waislamu wana matatizo! mbona mkapa hakuwahi kufanyiwa kura za maoni???
propaganda za kippumbavu kabisa!!!
 
Kama wananchi wote wangekuwa na uwezo wa kusoma hapa JF basi ghafla CCM ingepoteza sifa mbele ya wananchi pasipo kujua nini hasa sababu ya msingi kama lililofanyika kwa mzee F. Sumaye. Tunashindwa kujadiri uhalisi wa mambo na badala yake tunaingiza hisia binafsi. Tutafika, lakini safari yetu si salama, imejaa makwazo makubwa sana!!!!!!!
 
Je huu utafiti ungefanyiwa JF ingekuaje? Huu utafiti na wasiwasi nao. Si ajabu ni propaganda na wizi mtupu!
 
Ni rubbish si utafiti wala ndugu yake utafiti. Ni ile wao wanaita propaganda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…