Matokeo ya Utafiti: Kikwete, Freeman Mbowe, Zitto, Killango, Jerry Silaa na Dr Slaa

Huu ni uchafu ambao CCM imekuwa ikiufanya siku zote, Rais kikwete tangu aingie madarakani hakuna hata alichokifanya zaidi ya kusuluhisha lowasa na sitta. kazi ya pili aliyoifanya ni kuchekacheka tu ikulu kwani huyu ni mtu asiyefahamu wajibu hata kazi yake. Mfano mzuri ni alipokuwa ufaransa , aliuzwa swali kuwa kwa nini tanzania pamoja na kuwa na mali asili nyingi ya kutosha bado ni maskini? kwa nguvu zote yeye alijibu hajui ni kwanini.Mwandishi wa habari alijaribu kumuuliza tena kuwa hata wewe raisi wa nchi hujui? akakili kuwa hajui kabisa .Huyu ni raisi ambaye hajui hata wananchi anawaongoza wana hali gani, na hajui wanchi wake ni maskini au laa, jamani huyu hakutakiwa kuliongoza taifa ila kwa kuwa wanchi bado tumelala basi ccm ndo inapopiga bao .ni noma babu.
 


Kwangu ni UPUPU MTUPU Hivi hao wananchi 2000 ni wakazi wa Ukonga au Kibondemaji, Gezaulole? Panga la mwingereza? maana nashindwa kuelewa mtu wa Geza ulole atamjua vipi? diwani wa Ukonga? naamini ata hao wa Ukonga wapo wasio mjua diwani wao Jerry.

Tuache jamani kula hela za wahisani na hivi vi NGO's visivyo na Tija.
 
sasa ndugu yangu waulize maswali kwa elimu gani waliyokuwa nayo??? unafahamu ujinga ni kitu kibaya sanakatika maisha ya binadamu, ukiwa mjinga wa kitu hata unakuwa huna ujasiri wa kusema/ kufanya lolote, 'waandishi' wetu wa habari wakishajua kushika kipaza sauti, notebook na kalamu baaasi, wanawahi kwenye press conf. wapate chai na pengine posho kidogo haooo hata hawaelewi walichoambiwa wanakibwaga kwa wananchi moja kwa moja, hawajifunzi kwa wenzetu angalia kwenye vyombo vya nje waandishi wa habari wanakuwa ni waliobobea kwenye fani fulani kwa hiyo wanahoji kitaalamu na kwa kutumia taaluma zao!
 
Mkombozi imenibidi nicheke kweli tunatakiwa tujiulize eti chama kilicho karibu zaidi na wananchi watuambie kwenye nini ufisadi ni kama kusema 70% ya watanzania tunajihusisha zaidi na ufisadi kwa namna moja ama nyingine kuliko mambo mengine haa ha ha
 
total knock out
hizi tafiti zitaleta kizaazaa siku moja.
ikifika 2015 hawa waganga njaa watakuja na findings wakisema wamehoji wanachi 2500 kuwakilisha taifa zima kuhusu kubadilisha katiba kumwongezea muungwana another chance kwa kuwa umaarufu wake uko juu na hakuna mwenye uwezo aliyesalia zaidi yake.
 
wanadhani watanzania wa leo ni wajinga wa mawazo kama enzi zile za kwanza za mawe!!! hii ni dunia nyingine kabisa watu wanajua mambo meeeengi kuliko wao wanavyofikiri tatizo ni kukosa nafasi ambazo zitawawezesha kutumia kile wanachokijua, wachache walilong'ang'ania nafasi hawana jipya wanalolijua na bado wapo tu? I wish kungetoa mageuzi ya kweli !!! halafu huyo mkuu wa hiyo NGO utasikia kesho kawa mjumbe wa NEC!!!!!! Kabla hajapewa ukuu wa wilaya hizi mpya mpya za kina misungwi etc....
 

Kweli tumeumia pamoja na ma Phd yote aliyonayo anashindwa kujibu hili swali?

si nasikia kasomea uchumi UDSM? sasa alipitapita vipi? au alikuwa anadesa? Kama tuna msomi wa uchumi kutoka UD na awezi kujibu hili swali basi walimu wake ni hasara Tufunge chuo unless mniambie alikuwa anadesa.

Angesingizia wakoloni basi maana si tunasoma Tokea primary kuwa wazungu ndio wametufanya hivi?
 

Inabidi watu waache kuwalalamikia hawa watafiti na matokeo yao. Uongozi wa CHADEMA ulitakiwa uwe tayari umeshafanya utafiti wao wenyewe na kujaribu kuu-skew kidogo towards CHADEMA, ili kujaribu kurubuni wale wanaofuata upepo.

Lakini kwa kwa vile uongozi ni wa kibinafsi, mawazo yao pia yanakuwa ya kibinafsi. Sasa wamewaachia wapambe wa JK kuendelea kuvutia watu kwake na kuogopesha wengineo wote wenye nia ya kumpinga.
 
Nashangaa kusiki jina la diwani asiyejulikana kafanya nini hadi kutajw ana wananchi 200 nchi nzima. Nahisi alichangia gharama za utafiti huo ili atajwe naye ajulikane kidogo. Pia haiwezekanai mama Kilango awe maarufu kuliko Slaa hata asitajwe ni uongo uliowazi na inaonyesha walioendesha utafiti huo walielekezwa cha kufanya na matokeo yalipangwa, haiwezekani wananchi 2000 wote wasimjue Dk Slaa wamtaje Zito na Kilango.
Mapungufu ya utafiti huo huenda yalikuwa dhaifi kwa sababu zifuatazo.

1.Maswali yalikuwa yanaelekeza majibu yawe hivyo
2.Walioanya walikusudia yawe hivyo.
3.Waliohojiwa ni wana CCM halisi au watu wa vijijini kule kigoma ambao wanamjua tu Zito na Kikwete.
4.Walifanya utafiti huo kuset agenja za mjadala wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu ili CCM wanaopinga wajue kuwa wananchi bado wanamkubali Jakaya na chama chao hivyo wasihamie Chadema.

Hayo ni maoni yangu wakuujapo mie mwanasiasa ambaye bado sijaamua chama gani niingie maana zote za kibabaishaji tu labda CCJ kama ni ya kweli.
 


Kumbe ni Kampuni?

Sawa wanataka nini sasa? ardhi au Mgodi?
 

Sio waandishi, ni maripota. Ndio maana kuna Wasanii na wanamuziki.
Na kwenye redio kuna Presenter na Dj.
 
Sasa labda waje na vitu vingine kufanya utafiti wao, Hotel, vyuo, Warembo, Magari, kila aina ya huduma na hospital
 
Sasa ni kweli ameongoza but wamemlinganisha na nani ambaye naye ametangaza kugombea??
 
Mkombozi umenena. Hawa jamaa walipata fedha za wafadhili sasa wamejitahidi ku-"justify" matumizi ya hizo fedha. Huu ni uhuni na ufisadi mtupu. Kama mtu anaamua kufanya utafiti basi uwe utafiti wa maana na siyo kuchezea watu.
 
Watanzania walitaka kuibadilikia CCM mwaka 1995. Mwalimu akaokoa jahazi. Ni lazima sasa apatikane mtu mwingine mwenye haiba na ushawishi kama aliokuwa nao Mrema wakati ule. Vinginevyo tafiti hizi zitabaki hivyo zilivyo.

Ah, wakati ule wala si kwa sababu walitaka kuigeuzia kibao CCM, ni ile excitement ya uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi.

Sasa hivi hamna tena hiyo, labda mtu achomoke CCM aweke mambo wazi kwa wananchi kwenye grass roots.

Bila hivyo kitadumu chama cha mapinduzi!
 

umenena mtu wangu,

Ushauri uliousema hapa wakiupata baadhi ya wanachadema damu lakini wenye ubongo wa kutokufikiri wataona kama unawatukana.

who is synovate? hivi vyama vya upinzani should conduct their own studies, that will be another way of evaluating themselves!

Hii kusubiri ulipwe deni lako , halafu uchikichie sio vizuri, ni vyema hivi vyama vikajua mapigano ya sasa yako too scientificaly. kukaa ofisini kusubiri kudra za mwenyezi sio vizuri.

Hao waliofanya study, wanaweza wakawa wamepika data, kesho wanaweza kusema Mbowe anaongoza! wakati sio. Hivi siku za hivi karibuni mwananchi wa kawaida huko vijijini anajua Mbowe anafanya nini? isn't this alone questionable? angalau Slaa watu wanasikia mara huku mara huku, Mbowe kwenye hiyo list kapandikizwa, halafu watabweteka. CCM hao....
 
Kumbe ni Kampuni?

Sawa wanataka nini sasa? ardhi au Mgodi?

Nafikiri kuna haja ya kuwafikishia hilo swali:

Synovate Tanzania
Aggrey Oriwo — Country Manager
Regent Estate
Mikocheni Street
Plot 161 P.O. Box 106253
Dar-Es Salaam
Tanzania
Telephone: +255 22 277 5851 / 2037
Fax: +255 22 270 1606
Send an email


SYNOVATE: REINVENTING RESEARCH
We help our clients meet the commercial challenges of the information age by constantly creating innovative ways of gathering facts, and turning that data into strategic business insights. If there's no existing method of finding out what you need to know, we'll invent it.
Nimeuzimia huo mkakati wao kwenye nyekundu hapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…