Matokeo ya VPL: Simba SC wameibuka na ushindi wa mabao mawili kwa moja dhidi ya Dodoma Jiji FC

Chamaaaa ameingia kwenye box kwake Bwalyaaaaa anakosa loooooo

Daaaaaah ilikuwa hatari sana
 
Watanzania hawapendi mchezo wa mpira bali wanapenda timu. Ndio maana hata uwanja ulikuwa haujai kwenye Simba Cup.
 
Bwalya anapiga shutiiiiii loooooo njeee

Hatari sana huyu kijana, ilikuwa hatari lango la Dodoma Jiji
 
89' Ametoka Rally Bwalya na ameingia Ajibu upande wa Simba SC

Dodoma Jiji FC 1-2 Simba SC
 
90+3'

Kuelekea kumalizika kwa mchezo huu wa VPL, uwanja wa Jamhuri Dodoma

Hoza anapiga mbele, mabeki wa Simba wanazuia mpira unatoka nje, wanarusha kuleee, ni faulo kuelekea Simba

Dodoma wanapata Free Kick, inapigwaaaa, Manula anachumpa na anadaka bila wasiwasi, ilikuwa hatari lango la Simba, dah almanusura wasawazishe...

Naaaam mpira umekwishaaaa ambapo Simba wameibuka na ushindi mabao mawili kwa moja, mabao ya Kagere, Morrisoon na huku Mkandala akifunga upande wa Dodoma Jiji FC

VPL' FT: Dodoma Jiji FC 1-2 Simba SC

Ghazwat
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…