EMT
Platinum Member
- Jan 13, 2010
- 14,477
- 15,357
Wana ChitChat,
Matokeo ya awali ya Wachaga walioenda kwao kuhesabiwa yameanza kutolewa. Habari za ambazo zimetua kwenye dawati langu hivi punde na kudhibitishwa zinasema kuwa hadi hivi sasa, Kibosho inaongoza kwa asilimia 90!
Nafasi ya pili inashikiliwa na Marangu ambayo imejipatia asilimia 70.5, huku ikichuana vikali sana na Machame ambayo imepata asilimia 69.6 na kushika nafasi ya tatu. Rombo inashikilia nafasi ya nne kwa asilimia 65.8 ikifuatiwa na Old Moshi kwenye nafasi ya tano kwa kupata asilimia 50. Mgawanyo wa matokeo ya awali ni kama ifuatavyo.
Waliongoza kwa kula mbuzi na kunywa mbege.
Kibosho: Tayari mbuzi 400,000 wameshapoteza maisha huku debe 600,000 za mbege zikiwa zimeshanyweka! Ukoo unaongoza ni ule wa Mushi.
Marangu: Jumla ya mbuzi 300,310 wamechinjwa. Debe za mbege zilizonyweka had hivi sasa ni 513,000. Ukoo unaongoza ni ule wa Mosha.
Machame: Mbuzi 300,001 tayari zimeshachinjwa na debe 420,000 za mbege ziko tupu! Ukoo wa Kweka unaongoza kwa kunywa debe nyingi za mbege, huku mbuzi zaidi wakipoteza maisha kwenye ukoo wa Kwayu. Habari za chini chini zinasema kuwa Wamachame walikuwa wametarajia kushinda kwa kishindo mpambano huu kama Mh. Mbowe angetangaza nia ya kuogombea Urais, lakini kujitoa kwake kugombea Urais mwaka 2015 kumefanya baadhi ya Wamachame kurudi Dar Es Salaam fasta kabla ya mwaka mpya ili kuendelea na shughuli zao
Rombo: Jumla ya mbuzi 20,020 wamepoteza maisha, huku debe 26,092 za mbege zikiwa zimenyweka hadi jana. Koo za Kavishe na Swai zinaongoza lakini mchuano bado ni mkali. Warombo wengi waliamini wangeshinda mwaka huu hasa baada ya ile barabara ya lami kukamilika kwa vile ingewafanya Warombo wengi zaidi waende kuhesabiwa.
Hata hivyo, habari ambazo nimezipata hivi punde zinasema kuwa mbuzi wameisha kabisa huko Rombo na sasa wameamua kwenda kununua mbuzi mpakani na Kenya. Tayari Ben Saanane na Mkuu rombo wameonekana maeneo ya mpakani na Kenya wakifuatilia mbuzi. Pia kuna uwezekano Warombo kuaanza ku-import mbege kutoka Mwika kwa ajili ya kusherekea mwaka mpya!
Old Moshi: Jumla ya mbuzi 25,951 zimechinjwa. Wachaga wa Old Moshi pia wamefanikiwa kunywa debe 24,911 za mbege hadi hivi sasa. Ukoo unaongoza ni ule wa Shayo.
Tutaendelea kuwapa updates za mpambano huu mkali mara tuu tuzipatazo. Pia kama kuna Wana ChitChat walioko kwenye maeneo ya tukio tafadhali tupeni live updates.
UPDATES
Habari ambazo zimenifikia hivi punde lakini bado hazijathibishwa ni kwamba kuna Mwana ChitChat mmoja kutoka Marangu alikuwa amepanga kwenda Tanga kwa ajili ya kukutana na WanaJF kutoka Wing ya Kaskazini, lakini akaamua kukatisha safari ghafla na kurudi Marangu kuokoa jahazi.
Meza yangu imejaribu kuwasiliana na kiongozi wa masafara PakaJimmy lakini amekataa katakata kulizungumzia jambo hilo. Aidha meza yangu imejaribu pia kuwasiliana Preta kwa simu yake ya mkonomi lakini alipoulizwa juu ya Mwana Chit Chat huyo alikata simu. Tulijaribu kumpigia tena simu lakini iliita tuu bila kujibiwa. Baadae tulijaribu kumtumia SMS kumwuliza kama huyo Mwana ChitChat anaweza kuwa ni Asprin lakini hatukujibiwa.
Pia nilijaribu kuwasiliana na watu8, Madame B, Filipo, marejesho, Lily Flower, Blaki Womani, werawera na Smile lakini simu zao za mkononi zilikuwa zimezimwa. Arushaone alijibu simu yake lakini akasema kuwa yuko barabarani akiendesha kutokea Tanga kwenda Arusha kwa hiyo tumpigie baadae. Nilipomwuliza kama kuna mwana ChitChat mwingine kwenye gari ambaye ningeweza kuzungunza nae alikata simu!
Bado tunajaribu kuwasiliana na Dark City, KOKUTONA, Arabela, YNNAH na Mwanyasi kupata udhibitisho wa hii habari na kumjua huyu Mwana ChitChat aliyeamua kukatisha safari na kurudi Marangu kuokoa jahazi.
NAWATAKIA WANA CHITCHAT HERI YA MWAKA MPYA.