Shida yako Nguzo1 unapenda mambo hayo yakutokee kama yalivyokutokea katika miezi mitatu ila sasa wewe unapenda kuchanganya Mungu na mambo machafu vitu hivi havichanganyani kuwa upande mmoja kama wampenda Mungu acha pombe na zinaa au tafuta mwanamke mmoja oa kabisa Mungu anakupenda sana nguzo1 na anamengi ya kukutendea katika maisha fanya vile Mungu atakavyo kukutendea kuna mengi mazuri yanakuja mbeleni baada ya kujikabidhi mikononi mwa Mungu.
Huu ni ushauri wangu ukitaka ufanikiwe zaidi ufuate ukitaka kumkumbatia zaidi shetani endelea kumshikilia maisha haya ni mafupi na duniani tunapita!!!
Asante kwa kunisikiliza Nguzo1 maamuzi ni kwako mwenyewe!!!
Hakika mkuu sikujua kwamba ule uwezo niliupata kwa kujitenga na maovu ndani ya hiyo miezi mitatu ningelijua hilo wala nisingefanya mapenzi na kutumia kilevi ila sasa ndiyo nimedhamiria kuacha hizo dhambi na nikifikia uwezo nikiokuwa nao basi mimi na pombe basi na hata mapenzi nitajitenga nayo kabisa na nikizidiwa nitachukua uamuzi wa kuoa.
Nitajitahidi sana kutoshiriki ngono. Wakati nikiwa katika hiyo hali ya ufunuo kuna kipindi nilikuwa nimepumzika sehemu ya uwazi mida ya mchana nilikaa hapo kwa utulivu mkubwa mno baada ya lisaa limoja nikawaona mtu na mpenzi wake wanatembea huku wameshikana viuno kwa mahaba (tuwaite Jack na James) wakakaa meza iliyopo mebele yangu nikaanza kuwawazia (ikaja picha/screen kwenye paji la uso wangu nikaanza kuona jinsi watakavyoagiza chakula na vinywaji nikaona jinsi james atakavyoinuka na kwenda kuongea na mhudumu wa pale wakinongonezana akarudi kukaa na mwenza wake.
Ile screen ikaendelea kunionyesha picha jioni watakavyo kwenda room na kuanza kufanya mapenzi na wakati wanafanya mapenzi kuna watu wengi watakuwa wanawaangalia pembezoni mwa kitanda wakiwa kimya sura zao sikuziona na ni kama mashabiki wa mpira walikuwa wanaangalia penalt inavyopigwa uwanjani huku wakijiandaa kushangilia goli kama penalt ingepenya golini.
jack na james walipofika kileleni nikasikia sauti nyingi za watoto wachanga wakilia kana kwamba wamezaliwa na nikawaona wakianza kuzagaa mle chumbani wakitokea kitandani alikolala jack&james wale watu waliokuwa wanawaangalia pembezoni mwa kitanda waliposikia sauti za watoto wakashangilia na kuanza kuwakamata na kuwatafua kama kumbikumbi na watoto wengine wakawekwa kwenye cage/kitu kama box lilitengenzwa kwa nyavu kisha wakatoweka. Wale viumbe walivyotoweka basi jack alianza kuinuka kitandani kwa taabu sana huku akiwa amebadilika na kukonda sana kama mtu ambae hajapata chakula kwa muda mrefu james yeye aliendelea kulala. Gafla nikaona kama ninapaa hadi juu ya paa la ile hoteli nikapaa juu zaidi nikaanza kuona nyumba za jirani nikapaa juu zaidi kiasi cha kuliona jiji lote la dar es salaam nikiwa angani nikaanza kusikia zile sauti za watoto wachanga zikilia kila kona ya jiji na ile mijitu ikishangilia kwa nguvu zidi nikaanza kutua na kurudi nilipokaa nannikawaona jack na james bado wapo pale mezani nitakata kujua kujua kile nilichokiona ni ndoto au kweli basi nikajisemea kama ni ndoto ngoja nishtuke kutoka usingizini nikafanya kama kukohoa/kusafisha koo kidogo kama vile najiandaa kuongea na sikuona utofauti wa mazingira zaidi ya ile screen kupotea baada ya kukohoa hiyo sikuwa usingizini.
Wakati natafakari mara akaja mhudumu akawaletea chakula jack na james kumbe kweli waliagiza chakula sasa cha kushangaza ni jinsi mhudumu alivyokuwa anawanawisha mikono ni vilevile nivyoona kwenye ile screen muda mchache uliopita yule mhudumu alimwagia maji bahati mbaya james kwenye kiatu na kule kwenye screen niliona hivyo hivyo asee nilistuka sana nikagundua kumbe nilichokiona kwenye screen ndicho kinachokwenda kutokea nikazidi kuogopa haswa nilivyokumbuka kwenye scree niliona wale viumbe wa ajabu wakila wale watoto wachanga moyoni nikajisema ngoja niondoke nisije pata balaa.
Nikamwita mhudumu amwite mhudumu aliyenihudumia ila alichelewa kuja baada ya kama dakika 20 nikalipa bill yangu ila nikasubiria chenchi...chenchi nayo ilichelewa kuja na wakati ananiletea chenchi jack & james walikuwa wamemaliza kula tayari. Ile nataka kuondoka simu yangu ikaita kunagalia simu nikajua aliyenipigia lazima atakuwa na maongezi marefu na mimi hivyo nikakaa mezani ili nikimaliza kuongea na simu ndiyo niondoke. Niliongea na simu kwa muda kama dakika 45 na nilipokata nikaona James amenuka na kwenda Conter kuongea na mhudumu asee huwezi amini jamaa alivyonyanyuka kuelekea counter ni vile vile nilivyoona kwenye screen alivyotembea hatua mbili alirudi mezani na kuchukua simu yake na akaelekea hadi counter.
Hapa nikapata ujasiri wa ajabu nikasema siondoki ngoja nishuhudi. Alivyokuwa conter sikumuona vizuri aliporudi mezani alipomwacha jack kuna kitu alimwambia jack halafu wote wakacheka na jack akampiga kofi la mahaba begani huku wakiendelea kucheka Asee hapa nusu nipagawe tena maana ni kama nilikuwa naangalia movie ya marudio yani alivyompiga kofi begani na walivyocheka ni vilevile nilivyoona kwenye screen nikajisemea hapana hapa siko ndotoni hii ni kweli na nikambuka kwenye screen kuna muda nilipaa juu na kuliona jiji lote la dar nikaingia woga nikasema siko tayari kuendelea kukaa ile sehemu nikaondoka huku nikiwa na maswali mengi sana kichwani.
Wakuu yani hili tukio dogo tu ambalo lilitokea kati ya masaa mawili au matatu kwa kifupi nina mengi ya kuandika na kiukweli naitamani sana hii hali initokee tena.