Matokeo yote ya Watani wa Jadi Simba na Yanga

Makoye Matale

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2011
Posts
6,491
Reaction score
2,104
Salaam kwenu WanaJF.

Zimesalia siku chache kufikia mpambano mwingine wa watani wa jadi Simba na Yanga. Yapo mabishano mengi yanayojitokeza hasa katika kipindi hiki, kila upande ukijinasibu kuwa ni bora kuliko upande mwingine. Hata hivyo matokeo ya uwanjani huwa hayafuati mapenzi au hata majigambo ya kila upande, matokeo hutokea kulingana na uwezo wa kila timu.

Nimejaribu kupitia wavuti na blogu mbalimbali, sikufanikiwa kupata matokeo ya watani hawa wa jadi isipokuwa katika blogu ya BIN ZUBEIRY, nimefanikiwa kupata matokeo yote ya watani hawa tangu waanze kuingia katika mapambano ya ligi daraja la kwanza (sasa Ligi Kuu), kombe la Muungano na mapambano mengine mfano CECAFA, TUSKER n. k. Nimeandaa muhtasari wa matokeo hayo katika format ya pdf. Naomba sasa nitoe dondoo chache zitokanazo na matokeo hayo.

1. Yanga ndiyo timu ya kwanza kuifunga Simba hapo tarehe 07/06/1965 pale ipoibugiza Simba bao 1-0 mfungaji akiwa ni Mawazo Shomvi katika dakika ya 15 ya mchezo.

2. Yanga ndiyo timu ya kwanza kuibamiza Simba kichapo cha paka mwizi cha 5-0 hapo tarehe 01/06/1968. Kwa kipindi cha takribani miaka 9 hivi Simba ilikuwa ikijipanga kulipa kisasi hicho na ilipofika tarehe 19/07/1977 iliibamiza Yanga kipigo kikali zaidi cha 6-0.

3. Abdallah Kibadeni wa Simba ndiye mchezaji pekee aliyeweza kupiga bao 3 (hat trick) katika mapambano ya watani siku ya kifo cha karne cha Yanga cha bao 6-0 siku ya tarehe 19/07/1977. Kipigo hiki hakijalipwa na Yanga hadi leo.

4. Simba kwa mara nyingine tena iliibamiza Yanga kipigo kikali cha bao 5-0 siku ya tarehe 06/05/2012. Kipigo hiki ni malipo kwa Yanga kwa kipigo kama hicho cha tarehe 01/06/1968.

5. Hadi sasa watani Simba na Yanga wamecheza mapambano 109. Mapambano 30 yaliisha kwa sare au suluhu bila kutambiana. Yanga imefanikiwa kushinda mapambano 43 huku Simba ikitamba katika mapambano 36. Hadi sasa Simba inadaiwa na Yanga mapambano 7 ya kushinda.

6. Hadi sasa Yanga imefanikiwa kuifunga Simba mabao 140 huku Simba ikizifumania nyavu za Yanga mara 132. Simba inadaiwa na Yanga mabao 8.

7. Takwimu katika vipengele 5 & 6 hapo juu zinaungwa mkono na mataji ya ubingwa wa ligi kuu ambapo Yanga imefanikiwa kuchukua ubingwa mara 24 huku Simba ikishinda mataji mara 18.

Taarifa ndani ya jedwali ni nyingi, naomba niishie hapa ili kutoa nafasi kwa wachangiaji wengine kuzichambua.

Chanzo: BIN ZUBEIRY - MAPAMBANO YOOOOTE YA WATANI WA JADI, SIMBA NA YANGA KABLA YA PAMBANO LA KESHO | BIN ZUBEIRY

DISCLAIMER: Makoye Matale hatahusika kwa njia moja ama nyingine na madhara yoyote yatakayompata shabiki au msomaji yeyote wa post hii kwa mfano msongo, shinikizo la damu, kiharusi, kifo cha ghafla, kifafa, kizunguzungu, kuhara na kuhara damu n.k. yatokayo na kuujua ukweli huu.
 
Attachments

Last edited by a moderator:
Salaam kwenu WanaJF.

Zimesalia siku chache kufikia mpambano mwingine wa watani wa jadi Simba
na Yanga. Yapo mabishano mengi yanayojitokeza hasa katika kipindi hiki,
kila upande ukijinasibu kuwa ni bora kuliko upande mwingine. Hata hivyo
matokeo ya uwanjani huwa hayafuati mapenzi au hata majigambo ya kila
upande, matokeo hutokea kulingana na uwezo wa kila timu.

Nimejaribu kupitia wavuti na blogu mbalimbali, sikufanikiwa kupata
matokeo ya watani hawa wa jadi isipokuwa katika blogu ya BIN ZUBEIRY,
nimefanikiwa kupata matokeo yote ya watani hawa tangu waanze kuingia
katika mapambano ya ligi daraja la kwanza (sasa Ligi Kuu), kombe la
Muungano na mapambano mengine mfano CECAFA, TUSKER n. k. Nimeandaa
muhtasari wa matokeo hayo katika format ya pdf. Naomba sasa nitoe dondoo
chache zitokanazo na matokeo hayo.

1. Yanga ndiyo timu ya kwanza kuifunga Simba hapo tarehe 07/06/1965 pale
ipoibugiza Simba bao 1-0 mfungaji akiwa ni Mawazo Shomvi katika dakika
ya 15 ya mchezo.

2. Yanga ndiyo timu ya kwanza kuibamiza Simba kichapo cha paka mwizi cha
5-0 hapo tarehe 01/06/1968. Kwa kipindi cha takribani miaka 9 hivi
Simba ilikuwa ikijipanga kulipa kisasi hicho na ilipofika tarehe
19/07/1977 iliibamiza Yanga kipigo kikali zaidi cha 6-0.

3. Abdallah Kibadeni wa Simba ndiye mchezaji pekee aliyeweza kupiga bao 3
(hat trick) katika mapambano ya watani siku ya kifo cha karne cha Yanga
cha bao 6-0 siku ya tarehe 19/07/1977. Kipigo hiki hakijalipwa na Yanga
hadi leo.

4. Simba kwa mara nyingine tena iliibamiza Yanga kipigo kikali cha bao
5-0 siku ya tarehe 06/05/2012. Kipigo hiki ni malipo kwa Yanga kwa
kipigo kama hicho cha tarehe 01/06/1968.

5. Hadi sasa watani Simba na Yanga wamecheza mapambano 109. Mapambano 30
yaliisha kwa sare au suluhu bila kutambiana. Yanga imefanikiwa kushinda
mapambano 43 huku Simba ikitamba katika mapambano 36. Hadi sasa Simba
inadaiwa na Yanga mapambano 7 ya kushinda.

6. Hadi sasa Yanga imefanikiwa kuifunga Simba mabao 140 huku Simba
ikizifumania nyavu za Yanga mara 132. Simba inadaiwa na Yanga mabao 8.

7. Takwimu katika vipengele 5 & 6 hapo juu zinaungwa mkono na mataji
ya ubingwa wa ligi kuu ambapo Yanga imefanikiwa kuchukua ubingwa mara
24 huku Simba ikishinda mataji mara 18.

Taarifa ndani ya jedwali ni nyingi, naomba niishie hapa ili kutoa nafasi
kwa wachangiaji wengine kuzichambua.

Chanzo: BIN ZUBEIRY -
MAPAMBANO
YOOOOTE YA WATANI WA JADI, SIMBA NA YANGA KABLA YA PAMBANO LA KESHO |
BIN ZUBEIRY

DISCLAIMER: Makoye Matale hatahusika kwa
njia moja ama nyingine na madhara yoyote yatakayompata shabiki au
msomaji yeyote wa post hii kwa mfano msongo, shinikizo la damu,
kiharusi, kifo cha ghafla, kifafa, kizunguzungu, kuhara na kuhara damu
n.k. yatokayo na kuujua ukweli huu.

pamoja mkuu, hao watakaoumwa ghafla, j2 ndio watakufa kabisa!
 
Last edited by a moderator:
pamoja mkuu, hao watakaoumwa ghafla, j2 ndio watakufa kabisa!

Baada ya kuuanika hadharani ukweli huu, wazee wa Msongamanoni wamenywea na kuwa wadogo kama piriton. CC. Masuke and Company.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu umejitahidi lakini kuna baadhi ya mechi umeziacha, mfano ile iliyoisha kwa sare ya moja moja Simba akifunga Amri Kiemba na Yanga wakifunga kwa penati kupitia kwa Said Bahanuzi, na kuna nyingine mzee Hamis Kilomoni alifunga magoli manne peke yake ila sijui Yanga walipata mangapi.
 
Mkuu orodha ni ndefu, njoo na ushahidi wa rejea, nita ammend ili kuweka kumbukumbu sawa.
 
Mkuu hata ile ya mwaka jana nayo unataka ushahidi? Natumia simu nitakuja na information zote kuanzia kesho.
 
Duh.!!
Kumbe Simba Ana madeni kibao kwenye timu ya wananchi, ngoja jumapili tuongeze deni lingine.!!
 
Mkuu hata ile ya mwaka jana nayo unataka ushahidi? Natumia simu nitakuja na information zote kuanzia kesho.

Ile ya Kiemba na Bahanuzi ilifanyika 3/10/2012 haihitaji ushahidi, nakiri kutoijumuisha kwa bahati mbaya. Ile ya Hamis Kilomoni kufunga bao 4 peke yake ndiyo inahitaji 'concrete evidence'. Hata hivyo sare ya Oktoba 3 haina madhara kwa madai ya timu zote mbili. Asante Mkuu kwa comment yako murua.
 
Hiyo mechi ilichezwa mwaka 1964, na matokeo yalikuwa 4-0, kwa sababu umeamua kuanzia 1965 basi hiyo haina umuhimu sana, itabidi tuanzie pale mashindano yalipoitwa ligi kuu na sio daraja la kwanza.
 
kuanzia mwaka gani tena..
 
kwa hiyo bado wanadeni la tano duuu...:faint2:

Kwa sababu ukiangalia vilabu vilianzishwa miaka ya 1935 na 1936 na yeye kashindwa kuanzia 1936 na kuamua kuanzia 1965, ambayo ligi daraja la kwanza ilianza sasa kwa nini asianze ilipokuwa ligi kuu ambayo ni mwaka 1997?
 
Wewe anzia popote unapotaka lakini ukumbuke kuwa Yanga ni bora kuliko Simba, takwimu zinaongea zenyewe hazihitaji ufafanuzi wa kina.
 
Mkuu Masuke nimeonesha ugumu wa kupata data hizi, pongezi kwa BIN ZUBEIRY kwa kutupatia hata hizi data kuanzia 1965. Sina shaka na Yanga ya kuanzia 1935, ilikuwa moto, ilipoa miaka ya 2000 kwa sababu ya Yanga Kampuni na Asili (rejea takwimu). Kama una data za kuanzia 1936 ziweke hapa nami nitaziunganisha na kuzitoa mutatis mutandis.
 
Last edited by a moderator:
simba sikio la kufa tu,wimbo wetu uleee ahhh' simba makopo! Simba makopo! YANGA IMARA! YANGA IMARA!
 
Salaam kwenu WanaJF.

Zimesalia siku chache kufikia mpambano mwingine wa watani wa jadi Simba na Yanga. Yapo mabishano mengi yanayojitokeza hasa katika kipindi hiki, kila upande ukijinasibu kuwa ni bora kuliko upande mwingine. Hata hivyo matokeo ya uwanjani huwa hayafuati mapenzi au hata majigambo ya kila upande, matokeo hutokea kulingana na uwezo wa kila timu.

Nimejaribu kupitia wavuti na blogu mbalimbali, sikufanikiwa kupata matokeo ya watani hawa wa jadi isipokuwa katika blogu ya BIN ZUBEIRY, nimefanikiwa kupata matokeo yote ya watani hawa tangu waanze kuingia katika mapambano ya ligi daraja la kwanza (sasa Ligi Kuu), kombe la Muungano na mapambano mengine mfano CECAFA, TUSKER n. k. Nimeandaa muhtasari wa matokeo hayo katika format ya pdf. Naomba sasa nitoe dondoo chache zitokanazo na matokeo hayo.

1. Yanga ndiyo timu ya kwanza kuifunga Simba hapo tarehe 07/06/1965 pale ipoibugiza Simba bao 1-0 mfungaji akiwa ni Mawazo Shomvi katika dakika ya 15 ya mchezo.

2. Yanga ndiyo timu ya kwanza kuibamiza Simba kichapo cha paka mwizi cha 5-0 hapo tarehe 01/06/1968. Kwa kipindi cha takribani miaka 9 hivi Simba ilikuwa ikijipanga kulipa kisasi hicho na ilipofika tarehe 19/07/1977 iliibamiza Yanga kipigo kikali zaidi cha 6-0.

3. Abdallah Kibadeni wa Simba ndiye mchezaji pekee aliyeweza kupiga bao 3 (hat trick) katika mapambano ya watani siku ya kifo cha karne cha Yanga cha bao 6-0 siku ya tarehe 19/07/1977. Kipigo hiki hakijalipwa na Yanga hadi leo.

4. Simba kwa mara nyingine tena iliibamiza Yanga kipigo kikali cha bao 5-0 siku ya tarehe 06/05/2012. Kipigo hiki ni malipo kwa Yanga kwa kipigo kama hicho cha tarehe 01/06/1968.

5. Hadi sasa watani Simba na Yanga wamecheza mapambano 109. Mapambano 30 yaliisha kwa sare au suluhu bila kutambiana. Yanga imefanikiwa kushinda mapambano 43 huku Simba ikitamba katika mapambano 36. Hadi sasa Simba inadaiwa na Yanga mapambano 7 ya kushinda.

6. Hadi sasa Yanga imefanikiwa kuifunga Simba mabao 140 huku Simba ikizifumania nyavu za Yanga mara 132. Simba inadaiwa na Yanga mabao 8.

7. Takwimu katika vipengele 5 & 6 hapo juu zinaungwa mkono na mataji ya ubingwa wa ligi kuu ambapo Yanga imefanikiwa kuchukua ubingwa mara 24 huku Simba ikishinda mataji mara 18.

Taarifa ndani ya jedwali ni nyingi, naomba niishie hapa ili kutoa nafasi kwa wachangiaji wengine kuzichambua.

Chanzo: BIN ZUBEIRY - MAPAMBANO YOOOOTE YA WATANI WA JADI, SIMBA NA YANGA KABLA YA PAMBANO LA KESHO | BIN ZUBEIRY

DISCLAIMER: Makoye Matale hatahusika kwa njia moja ama nyingine na madhara yoyote yatakayompata shabiki au msomaji yeyote wa post hii kwa mfano msongo, shinikizo la damu, kiharusi, kifo cha ghafla, kifafa, kizunguzungu, kuhara na kuhara damu n.k. yatokayo na kuujua ukweli huu.
Jiwe hili sijui karushiwa nani?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom