Mwimbaji wa Tanzania Matonya ameachiwa huru kutoka gereza la Shimo La Tewa lililopo Mombasa, ambako alikuwa akishikiliwa kwa takriban siku 20 kufuatia tuhuma za ubakaji.
Msanii huyo, ambaye amekanusha vikali tuhuma hizo, amepewa dhamana baada ya kutimiza masharti ya bondi ya shilingi 500,000 za Kenya, bila chaguo la kulipa fedha taslimu kama dhamana mbadala.
Aidha, ameagizwa kuwasilisha pasipoti yake mahakamani, huku pia ikitolewa taarifa ya tahadhari (red alert) kwa idara ya uhamiaji ili kuzuia asitoroke nchini bila kibali.
Matonya anadaiwa kutenda kosa hilo la ubakaji Aprili 7, 2026, katika fleti moja iliyopo Nyali, Kaunti ya Mombasa.
Inaelezwa kuwa wakati wa tukio hilo, msanii huyo alikuwa katika fleti hiyo akiwa na wanawake wawili—mmoja anayemfahamu vizuri, na mwingine akiwa rafiki wa rafiki yake.
Kwa mujibu wa ripoti ya polisi, mtuhumiwa pamoja na rafiki yake walilala chumbani, huku mwanamke wa pili akilala kwenye kochi sebuleni.
Polisi wanasema kuwa Matonya alitoka chumbani kwake na kwenda sebuleni, ambako anadaiwa kumbaka mlalamikaji, kisha kumshambulia kimwili alipojaribu kupiga kelele kuomba msaada.
Tukio hilo lilisababisha kukamatwa kwa msanii huyo na kufikishwa mahakamani. Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa awali (pre-trial) Aprili 30.
Soma pia Mwanamuziki Matonya ashtakiwa kwa ubakaji nchini Kenya