Matonya alivunja katiba ya bongo flava, hakushitakiwa

Matonya mpaka kawa mzee matonya yule marehemu ombaomba ila mzee matonya japo alijenga
 
Akwelina, hii nyimbo Matonya alitoa kuhusu dada anayejihusisha na mapenzi ya jinsia moja
 
Tunda Man wa Manzese ndio alikuwa mwandishi wa nyimbo za Matonya na watu wote waliokuwa wanashinda mbele ya Kitega Uchumi kwenye ofisi za Clouds wanalijua hilo. Kilichomsukuma Tunda kushika microphone mwenyewe ni hicho. Alikuwa anampa mwana mistari yenye vina lakini hapewi credit yoyote na mambo ya mitonyo mchizi anamruka viunzi.
Bagumashi ni sababu nyingine inayozorotesha nyanja nyingi za maendeleo Bongo yetu.
Hii ni kweli kabisa. Baada ya hii conflict kutokea ndio ikawa kama Tonya ameshuka kimuziki. Pia Tonya ana skendo skendo za kukosa uaminifu kwenye maokoto!
 
Alivyokorofishana na Tunda, Tonya alipotea mpaka alivyokuja kubebwa na Lady JayDee Kwenye Anita.
Kwenye mambo ya pesa wabongo wengi ni konakona tu. Na hii ndio sababu ya kuzorota kwa maendeleo Kwenye nyanja nyingi.
We mtu akikufanyia kazi mlipe vizuri afurahie jasho lake kisha angalia atakavyojituma.
 
Masterplan ya Tanga kuitawala Bongo Flava, ilianza kwa kutambulisha silaha yao ya maangamizi "Matonya", ambaye kinyonge, alilia “Uaminifu” akimshirikisha Bwana Misosi.

Jamhuri yote ya Bongo Flava ilisaluti talanta ya Matonya. Halafu akapotea masikioni mwa watu. Tanga ikachekwa kuwa ilitambulisha silaha ya one hit wonder yani Ngoma moja, pumzi kwisha.

Hesabu 2004, nenda 2005, weka kituo 2006. Matonya akarudi kwa ujio ulioacha historia ya dude baada ya dude, mawe juu ya mawe.

“Siamini” ilikuwa chereko. Janki wa Kitanga aliopoa manzi mwenye mahaba ya kibaikoko na kidumbaki, hakuamini kuchukua mtoto mkali. Halafu huyo manzi, kawatosa matajiri wenye mzigo.

Ujio wa pili, Matonya hakutaka mazoea. Hapo bado "Siamini" haijapoa, akaifanya Afrika Mashariki ilie kwa “Dunia Mapito.” Zikafuata tambo za kumpata “Vailet”. Sijui nani alichonga Tonya asingempata Vai wake!

Ngoja nikusimulie mshikaji wangu, Vailet ni mkwaju uliokaa kileleni kitambo kirefu bila kushuka wala kuchoka. Taifa likashudia ma-Vailet wengi. Walijitokeza kwenye vyombo vya habari, wakisema ni wao walioimbwa. Ni Bongo Flava na drama zake.

Wanamuziki wanadumu na mapenzi basi? Ilipofika mwaka 2008, Matonya alikwenda mpaka kwa mganga kumsaka “Anita”. Kazi ya Ambrose Dunga. Mom In Chief wa Bongo Flava, Lady Jaydee, aliweka sauti.

Ni Matonya aliyemfanya Irene Uwoya aitwe “Taxi Bubu” kwa kolabo na Fid Q, halafu akampigia magoti Aunty Ezekiel, ili tu amkubalie kuwa “Spare Tyre” mbele ya njemba yake, Mpoki.

Katiba ya Bongo Flava inatambua muhula wa utawala kimuziki ni mwaka mmoja bila nyongeza. Mwaka 2006, Matonya alipokaa on top, alivunja Katiba, akabaki madarakani 2007, 2008 hadi 2009. Raia walichekelea Tonya kuvunja Katiba.

Wengi hamjui how good the good old days, Matonya akiitawala Bongo Flava kama mali yake binafsi. Mapromota waliteseka kumpata. Bookings zimefunga mwaka mzima. Hakuna upenyo. Kila siku ziarani.

Nini nyumba na magari? Matonya alijenga mpaka hoteli. Unashangaa? Kwani ule u-busy, mwaka mzima anapiga show bila kupumzika, alikuwa anaingiza mawe?

Respect kwa Tonya mbili
Baadae akaamua kuuza ngada
 
Kweli kila zama za fursa zake kwa namna vile zile nyimbo zilihit, kwa dunia ya sasa ya social media na pesa za mtandaoni, Matonya, Mr Nice, Rose Muhando, Ferouz na Saida Karoli wangekuwa mabilionea

Muziki wanaudai hela nyingi sana sema ndio hivyo tena zile zama za kule mapromota na huku mdosi anachukua chake

Basi ndio hivyo tena
Huku ruge akikununuia ndo kwisha habari yako
Mziki ulikuwa umekamatwa na deep state wa kipindi hicho wakiongozwa na ruge
 
Sema unaonekana humjui vizuri matonya maana hit yake Kali ya Kwanza ilikua... NAMTAFUTA MREMBO
Wote hammjui,uaminifu ndio wimbo wa kwanza kumtoa,akapewa zawadi ya pikipiki na Bozinia,Matonya akaacha kuwinda njiwa kwa manati barabara za namba
 
Masterplan ya Tanga kuitawala Bongo Flava, ilianza kwa kutambulisha silaha yao ya maangamizi "Matonya", ambaye kinyonge, alilia “Uaminifu” akimshirikisha Bwana Misosi.

Jamhuri yote ya Bongo Flava ilisaluti talanta ya Matonya. Halafu akapotea masikioni mwa watu. Tanga ikachekwa kuwa ilitambulisha silaha ya one hit wonder yani Ngoma moja, pumzi kwisha.

Hesabu 2004, nenda 2005, weka kituo 2006. Matonya akarudi kwa ujio ulioacha historia ya dude baada ya dude, mawe juu ya mawe.

“Siamini” ilikuwa chereko. Janki wa Kitanga aliopoa manzi mwenye mahaba ya kibaikoko na kidumbaki, hakuamini kuchukua mtoto mkali. Halafu huyo manzi, kawatosa matajiri wenye mzigo.

Ujio wa pili, Matonya hakutaka mazoea. Hapo bado "Siamini" haijapoa, akaifanya Afrika Mashariki ilie kwa “Dunia Mapito.” Zikafuata tambo za kumpata “Vailet”. Sijui nani alichonga Tonya asingempata Vai wake!

Ngoja nikusimulie mshikaji wangu, Vailet ni mkwaju uliokaa kileleni kitambo kirefu bila kushuka wala kuchoka. Taifa likashudia ma-Vailet wengi. Walijitokeza kwenye vyombo vya habari, wakisema ni wao walioimbwa. Ni Bongo Flava na drama zake.

Wanamuziki wanadumu na mapenzi basi? Ilipofika mwaka 2008, Matonya alikwenda mpaka kwa mganga kumsaka “Anita”. Kazi ya Ambrose Dunga. Mom In Chief wa Bongo Flava, Lady Jaydee, aliweka sauti.

Ni Matonya aliyemfanya Irene Uwoya aitwe “Taxi Bubu” kwa kolabo na Fid Q, halafu akampigia magoti Aunty Ezekiel, ili tu amkubalie kuwa “Spare Tyre” mbele ya njemba yake, Mpoki.

Katiba ya Bongo Flava inatambua muhula wa utawala kimuziki ni mwaka mmoja bila nyongeza. Mwaka 2006, Matonya alipokaa on top, alivunja Katiba, akabaki madarakani 2007, 2008 hadi 2009. Raia walichekelea Tonya kuvunja Katiba.

Wengi hamjui how good the good old days, Matonya akiitawala Bongo Flava kama mali yake binafsi. Mapromota waliteseka kumpata. Bookings zimefunga mwaka mzima. Hakuna upenyo. Kila siku ziarani.

Nini nyumba na magari? Matonya alijenga mpaka hoteli. Unashangaa? Kwani ule u-busy, mwaka mzima anapiga show bila kupumzika, alikuwa anaingiza mawe?

Respect kwa Tonya mbili
Ukiacha yote binafsi nimependa uwasilishaji wako
 
Kipindi anakimbiza miaka hiyo yote MB Doggy alikuwa wapi? Is MB DOGGY JOKE TO YOU?![emoji16][emoji16]
 
Back
Top Bottom