Matrafiki kukaa Barabarani kunasababisha maradhi ya Moyo na msongo wa mawazo kwa Madereva

Matrafiki kukaa Barabarani kunasababisha maradhi ya Moyo na msongo wa mawazo kwa Madereva

Jeshi la Polisi Tanzania Lina utaratibu la kuwapa vitendea kazi trafki yaani askari wa usalama barabarani vikiwemo Mashine ya Risiti na Tochi ya kukamatia waozidi mwendo wa 50 jambo ambalo ni tofauti na nchi za wenzetu ambapo trafiki wao hupewa Silaha, gari na nyenzo nyingine muhimu.

Jambo hili limeondoa maana ya askari kufanya shughuli takwa na inaonekana lengo kubwa kwao ni kukusanya fedha ,na huwa wamejipanga barabarani sehemu ambayo imejengwa kwa Kodi Ili raia wapite kwa usalama na bila hofu.

Kitendo cha Trafki kusimama barabarani na Mashine ya Risiti na Tochi kinaleta hofu kubwa sana kwa Madereva , na hivyo kuwaletea Msongo mkubwa wa mawazo na kuwasababishia magonjwa ya Moyo, presha na sukari. Hakuna jambo baya barabarani Kama kusimamishwa na Trafki akiwa na vitendea kazi vyake.

Kila dereva akiingia barabarani jambo la kwanza kuwaza ni Trafki, na wahanga wakubwa ni Madereva wa Mafuso ya mchanga, virikuu, pickup, malori ya mizigo, watu Hawa wamekuwa wakisumbuliwa na magonjwa ya Msongo ikiwemo presha sababu ya kukutana na stress za Trafki kila siku.

Jambo jingine kitendo Cha Trafki kuwa barabarani ni kitendo Cha mambo ya Rushwa, Polisi wanafundisha raia kutenda makosa ya Rushwa, Polisi huko barabarani wamewafundisha watu kuwa Rushwa ndo tiba ya matatizo yako,

Hali iliyopelekea na Madereva nao huko mtaani wanakoenda wanaeneza elimu ya Rushwa waliofundishwa barabarani na hivyo kupelekea nchi nzima kunuka Rushwa.

Itafutwe namna nyingine nzuri ya kudeal na usalama kuliko hao jamaa wenye nguo nyeupe na kofia nyeupe, ukiwaona tu moyo unastuka
Nikiwa barabarani kwenda kwetu Ipinda sijawahi fikiria trafiki ilimradi nifuate sheria na taratibu ila huwa naeka buku2 na buku pembeni ili kuokoa muda
 
Naungana na huyo jamaa u anaemcrash hapo, kama gari yako imekamilika na huna mapungufu yoyote wewe mwenyewe na gari yako hofu ya Nini? Yani utamuogopaje trafik, kwa lipi?
Hata hao wanaotoa rushwa kwa trafik je huwa hawakutwi na makosa kweli? Utatoaje Kama gari imekamilika?
Nina chombo pia
Mkuu, inawezekana ukawa na chombo lakini ukawa hujawahi kukutana na maswahibu ya hawa wakubwa - labda hutumii chombo chako kwa safari za masafa marefu katika barabara kuu (highways). Lakini kama unaweza fanya utafiti mdogo kama majaribio utakuja kubali kuwa hawa askari wa barabarani ni shida. Atakuambia umeovateki mahali ambapo mstari hauruhusu (hapo chombo chako ni kizima na kila kila stika), utamwambia hapana hujaovateki pasiporuhusu au umeovateki lakini palikuwa panaruhusu - mnaanza kubishana. Unamwambia basi akufikishe mahakamani ili akathibitishe kosa hilo maana utawala wa sheria ni kuwa hakuna aliye juu ya sheria, anakataa na kukuandikia faini kwa kosa ambalo hujakubali kulitenda - ameshajigeuza mahakama, yaani mkamataji yeye na mahakama yeye mwenyewe.
 
Naungana na huyo jamaa u anaemcrash hapo, kama gari yako imekamilika na huna mapungufu yoyote wewe mwenyewe na gari yako hofu ya Nini? Yani utamuogopaje trafik, kwa lipi?
Hata hao wanaotoa rushwa kwa trafik je huwa hawakutwi na makosa kweli? Utatoaje Kama gari imekamilika?
Nina chombo pia
Jeshi la polisi ndilo linalotoa Stika ya Nenda kwa Usalama Barabarani. Wanazalisha stika chache kuliko idadi ya magari, zinanunuliwa zote na kuadimika, magari mengine yanakosa stika ilhali watumiaji wanataka kununua. Hapohapo, jeshi la polisi linaanzisha operesheni KAMATA MAGARI YASIYO NA STIKA YA USALAMA BARABARANI. Unakamatwa na unajitetea kuwa ulikwenda kituoni kununua ukaambiwa zimekwisha, anakwambia kwa nini hukununua mapema, sasa hata ningenunua mapema si kuna mwingine bado angekosa tu!! Anakupiga umeme, FAINI - unamwambia haya niuzie stika ili nibandike kwenye gari, anakujibu kuwa zimeisha na jeshi halijazalisha STIKA nyingine
 
Wakati wangu naendesha gari huwa siwafikiri matrafiki kabisa

Ova
 
Kuna mzee mmoja alizimia kabisa kisa kiwewe Cha tilafiki
 
Na cha ajabu hawa askari hawajali kabisa kuhusu saikolojia ya dereva na usalama wa watumiaje wengine wa barabara. Anamsimamisha dereva na kumbambikia kosa na kumtwanga faini, dereva anabishana na askari kupinga ubambikwaji anatishiwa kuwekwa selo au anajibiwa shombo na kuamriwa kuondoka eneo la tukio ama sivyo atashtakiwa kwa kumzuia askari kufanya kazi yake.

Sasa, askari wa usalama barabarani, hivi mnategemea huyu dereva aliegadhibishwa hivyo ataendesha gari sawasawa? Usalama wa kwake mwenyewe, abiria aliowabeba na watumiaji wengine wa barabara anaopishana nao unakuaje? Imajini madereva wawili waliobambikwa makosa na faini wanapishana, yaani wanaendesha magari huku wana mawazo ya kwa nini wameonewa, nini kinatokea?? Hamjui kuwa dereva anapoendesha huku ana hasira na saikolojia haijakaa sawa ni hatari maana anahatarisha usalama wake mwenyewe na wa watumiaji wengine wa barabara??

Maaskari wa barabarani, Badilikeni - boresheni usalama barabarani badala ya kuchochea hatari barabarani kwa kuharibu utulivu wa akili za madereva wawapo barabarani wakiendesha vyombo vya moto.
Hiki kitu umekieleza hapa ni ukweli kabisa, mimi nimeshawahi kubambikiwa speed isiyokuwa yangu na uzuri nafahamu hilo eneo niliingia nikiwa speed ngapi.
Lakini kilichotekea ni yule askari aliyeniandikia kwanza kabisa nilivyofika kaniambia anaomba akague leseni yangu nikampatia baada ya muda akazunguka gari na kurudi ananieleza nimezidisha speed hivyo ananiandikia fine nitajaribu kumueleza ni eneo gani ambalo nimezidisha akakataa kulitaja ila.nikaomba basi anipe picha niione akanionesha na ukweli speed radar haikuwa sawa na gari yangu na hii najua target ingekuwa vipi ili nikubali kama ni mimi.

Kifatia hivyo niliomba kuongea na.aliyenipiga hiyo picha nashukuru alinielewa ila bw**g**e aliyechukua leseni aliandika hiyo fine sababu alikuwa na details zangu pembeni. Baadae nakuja kuangalia nakuta nimeandikiwa fine ilinivurugia sana mood ya safari na safari ilikuwa ni ndefu hivyo askari wanachangia sana kuharibu saikolojia ya madereva barabarani.
Wanajiona sana wakivaa hizo uniform utadhani maisha wameyapatia na wao ndio wenye haki siku zote.
 
Back
Top Bottom