Matrafiki kukaa Barabarani kunasababisha maradhi ya Moyo na msongo wa mawazo kwa Madereva

Nikiwa barabarani kwenda kwetu Ipinda sijawahi fikiria trafiki ilimradi nifuate sheria na taratibu ila huwa naeka buku2 na buku pembeni ili kuokoa muda
 
Mkuu, inawezekana ukawa na chombo lakini ukawa hujawahi kukutana na maswahibu ya hawa wakubwa - labda hutumii chombo chako kwa safari za masafa marefu katika barabara kuu (highways). Lakini kama unaweza fanya utafiti mdogo kama majaribio utakuja kubali kuwa hawa askari wa barabarani ni shida. Atakuambia umeovateki mahali ambapo mstari hauruhusu (hapo chombo chako ni kizima na kila kila stika), utamwambia hapana hujaovateki pasiporuhusu au umeovateki lakini palikuwa panaruhusu - mnaanza kubishana. Unamwambia basi akufikishe mahakamani ili akathibitishe kosa hilo maana utawala wa sheria ni kuwa hakuna aliye juu ya sheria, anakataa na kukuandikia faini kwa kosa ambalo hujakubali kulitenda - ameshajigeuza mahakama, yaani mkamataji yeye na mahakama yeye mwenyewe.
 
Jeshi la polisi ndilo linalotoa Stika ya Nenda kwa Usalama Barabarani. Wanazalisha stika chache kuliko idadi ya magari, zinanunuliwa zote na kuadimika, magari mengine yanakosa stika ilhali watumiaji wanataka kununua. Hapohapo, jeshi la polisi linaanzisha operesheni KAMATA MAGARI YASIYO NA STIKA YA USALAMA BARABARANI. Unakamatwa na unajitetea kuwa ulikwenda kituoni kununua ukaambiwa zimekwisha, anakwambia kwa nini hukununua mapema, sasa hata ningenunua mapema si kuna mwingine bado angekosa tu!! Anakupiga umeme, FAINI - unamwambia haya niuzie stika ili nibandike kwenye gari, anakujibu kuwa zimeisha na jeshi halijazalisha STIKA nyingine
 
Wakati wangu naendesha gari huwa siwafikiri matrafiki kabisa

Ova
 
Kuna mzee mmoja alizimia kabisa kisa kiwewe Cha tilafiki
 
Hiki kitu umekieleza hapa ni ukweli kabisa, mimi nimeshawahi kubambikiwa speed isiyokuwa yangu na uzuri nafahamu hilo eneo niliingia nikiwa speed ngapi.
Lakini kilichotekea ni yule askari aliyeniandikia kwanza kabisa nilivyofika kaniambia anaomba akague leseni yangu nikampatia baada ya muda akazunguka gari na kurudi ananieleza nimezidisha speed hivyo ananiandikia fine nitajaribu kumueleza ni eneo gani ambalo nimezidisha akakataa kulitaja ila.nikaomba basi anipe picha niione akanionesha na ukweli speed radar haikuwa sawa na gari yangu na hii najua target ingekuwa vipi ili nikubali kama ni mimi.

Kifatia hivyo niliomba kuongea na.aliyenipiga hiyo picha nashukuru alinielewa ila bw**g**e aliyechukua leseni aliandika hiyo fine sababu alikuwa na details zangu pembeni. Baadae nakuja kuangalia nakuta nimeandikiwa fine ilinivurugia sana mood ya safari na safari ilikuwa ni ndefu hivyo askari wanachangia sana kuharibu saikolojia ya madereva barabarani.
Wanajiona sana wakivaa hizo uniform utadhani maisha wameyapatia na wao ndio wenye haki siku zote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…