Mayu
JF-Expert Member
- May 11, 2010
- 7,621
- 12,505
Umetumia kigezo gani kuona imani zingine ni POTOFU na imani zingine ni SAHIHI?Unachotaka kufanya wewe ni kuondoa uhuru wa imani au kuamini ambao ni haki iliyo kisheria, imani potofu zinapingwa na watu wanaelimishwa hivyo usitake kuondoa uhuru wa imani kisa kuna baadhi ya imani ni potofu dawa ni kuelimisha watu sio kuwafanya kuwa atheists hiyo haitosaidia kutokuwa na imani potofu au kutotenda uhalifu.
Kila siku tunasikia matukio ya kinyama watu hufanya kwa sababu za kisiasa au unakuta kisa ni wivu tu wa mapenzi, watu wanaacha kufanya kazi na kukesha kubeti n.k hivyo mtu anaweza kufanya lolote kwa kutumia lolote.
Imani ni Imani..... usiweke double standard mkuu
Kwa muktadha wa hoja yako ni kwamba kumzuia mmasai asiuwe mtoto wake kilema ni kumuingilia uhuru wake wa kuamini?