Mlinzi Shujaa_
Member
- Mar 30, 2020
- 68
- 106
Tarehe ( 30 / 12 / 2024 ) majira ya saa nne asubuhi katika eneo la majohe relini jijini dar es salaam tanzania, mlinzi shujaa alivamiwa na wauaji wawili ambao walikuwa na bajaji hawakuitaji chochote kutoka kwake, bali walishuka katika bajaji nakuanza kumshambulia na magongo makubwa ambayo yalikua yamefanyika mpaka leo. Bahati nzuri mlinzi alikuwa anauwezo mzuri wa kujihami, hivyo alikabiliana nao vilivyo, kufa kupona , akawapiga hadi wakakimbia katika bajaji yao na kutoweka kabisa katika eneo la tukio. Mlinzi shujas baada ya tukio hilo alienda katika kituo cha polisi cha gongola mboto kilichokuwepo katika eneo la sokoni wakati huo kabla hakijavunjwa wakati wa vurugu za uchaguzi mkuu wa 9 desemba.
Alipo fika kituoni akatoa taarifa jinsi alivyo vamiwa hadi alivyokabiliana nao, polisi wakampa karatasi wakamwambia aende hospitali akapate vipimo kisha arudi polisi ili polisi wafuatilie kesi hiyo, mlinzi akawaambia mimi nipo salama kabisa, sijaumia hata kidogo, ila nimekuja kutoa taarifa hii ili jeshi la polisi liwe na taarifa kwamba majohe kuna vijana wdngi sana wanavuta bangi na kutumia madawa ya kulevya mwende mkachunguze ikibidi muwakamate na muwawajibishe kwa makosa ya kuvamia watu na kuwaliga bila sababu au kupora mali za watu, polisi wakasema sisi hatuendi mpaka uje na majibu ya hospitali, mlinzi shujaa akarudi zake nyumbani, alipo fika nyumbani akaielezea familia yake kila kitu kilicho mkuta, kisha familia yake ikafurahi sana baba yao kurudi nyumbani salama.
TUKIO LA PILI
litaendelea