Elections 2015 Matukio na Matokeo toka maeneo mbalimbali ya Tanzania - Uchaguzi Mkuu 2015


Unaonaje Ukituwekea Pia Na Ya CCM Tena Ukianzia Na Ya Urais Hadi Ktk Mtiririko Wako Huo?
 

Hee Urais katangazwa nani mkuu? me nipo shamba huku sijasikia.
 
Kuna tv channels ambazo kila kwenye vurugu ndizo huchangamkia na kutoa TAARIFA utadhani wanafurahia.wala hawakemei mambo ya vurugu.waache
 
Kwani si walisha bandika vituoni na mawakala wamesign? Ondoa shaka watatangaza tu!
 
Kwa mara ya kwanza tangu kupata uhuru nchi yetu imeonekana kwenye vyombo vya kimataifa,kwa mara ya kwanza Afrika na Dunia imeongea kuhusu Tanzania
Baba kazi uliyofanya kwa kujitolea ni kubwa kuliko hata ya Urais,japo bado tunasubiri matokeo lakini hata kama ukishindwa umefanya kazi kubwa sana ya kutangaza mchi yetu kwa mara ya kwanza tangu uhuru,
mimi nimefarijika baada ya kuona vyombo vya kimataifa kama CNN wakisema ni uchaguzi wa century haujawahi kutokea
umeongeza ushawishi na ari kubwa ya kupiga kura na kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu tumejitokeza 77% ukilinganisha na 33% iliyojitokeza 2010
Baba tunakupenda na kazi uliyofanya tutaiheshimu milele hata kama hatutashinda!
 
Baada ya magwiji wa siasa za upinzania Augustino Mrema na Momose Cheyo kushinda kurudi bungeni, nafasi zao sasa zitachukuliwa rasmi na Zitto Zuberi Kabwe.
 
Wanavuta "attention" kwenye matokeo ya Udiwani na Ubunge; wapinzani wakibaki kukodolea macho ubunge na udiwani, wanaweka sasa namba za Uraisi. Wabunge wa Arumeru wamekuwa wajanja, matokeo ya Uraisi kwanza kabla ya Ubunge. Laiti wote wangesimamia hilo hata kama wameshindwa....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…