Hakika Mwaka 2004 ulioongoza kwa vipindi vingi vya kutoa elimu ya uelimishaji rika juu masuala ya ngono salama, ngono zembe, athari za ngono zembe, faida za ngono salama, visababishi vya Ukimwi na virusi vya ukimwi, jinsi na namna ya kujikinga na kuwakinga wengine na virusi vya ukimwi na ukimwi.
PSI Tanzania waliendesha kampeni kabambe katika kutekeleza hilo kwa kuja na matangazo mbalimbali ya kwenye vipindi vya redio na luninga (televisheni) vilivyotoa elimu mahususi ya ukimwi na virusi vya ukimwi ikiwa na kaulimbiu mbalimbali zikiwemo :
View attachment 3131518
‘’Kama Kweli Unampenda Utamlinda’’
View attachment 3131513
‘’Salama Chaguo la Kweli’’
View attachment 3131512
"Michepuko Sio Dili" na "Kuwa Original, Tumia Original’’.
View attachment 3131508
Haya matangazo yote yalikua yanalenga matumizi ya kondomu sana sana 'Salama' kondomu.
Bila kusahau mwaka huo huo 2004 kulikua na michezo mbalimbali ya Maigizo kupitia televisheni channel ya ITV na vikundi mbalimbali vilitoa michezo ya maigizo inayotoa elimu kuhusu ukimwi na virusi vya ukimwi, kwa mfano kundi la Nyota Academia km sijakosea walitoa mchezo wa maigizo, ambapo siku hizi nyinyi mnaita tamthiliya ila kipindi hicho sisi tulikua tunaita
maigizo au
igizo na televisheni ilikua inasema
igizo linalofuata, mchezo huo wa maigizo pia uliokua ukitoa elimu kuhusu ukimwi na virusi vya ukimwi na km sijakosea mhusika mkuu aliigiza km muathirika kweli wa virusi vya ukimwi, kwenye igizo hilo muhusika mkuu aliigiza kua ana kikohozi fulani hivi kikavu sana na jinsi alivyokua anajiweka kiugonjwa ugonjwa km mgonjwa kweli wa ukimwi ilipelekea kila mtu alikua anaogopa kupata ngwengwe kipindi hicho.
Kipindi hicho ndio kulikua na makundi mengi ya maigizo yaliyochuana vilivyo kupitia redio na televisheni km vile Kaole Sanaa Group, Mambo Hayo, Kidedea, Kidedea Original, Nyota Academia na mengine sijayataja