Matukio ya kukumbukwa mwaka 2004

Vitoto vingi sana humu aisee 🤣.

Unakuta ka mtu hiyo 2004 hata ungo hakajavunja bado.
 
Halafu tunategemea nchi isonge mbele Kama jitu linakumbuka pop star tu

Ndinalioooooo 🥹🥹
 
Kisiasa 2004 uchaguzi wa serikali za mitaa ulikua hautiliwi maanani na upinzani, kwa kiasi chake chadema ilikua inaanza kusikika kishindo chake, mbowe, lipumba ,maalim Seifu, zito ,slaa, walikuwa wakisikika sana.
Kule ccm joto la uchaguzi mkuu lilikuwa linaanza kujitokeza.
 
Ukimwi wa zamani ulikuaga balaa umemmaliza wengi.

Yale aliyo yaimba ferouz mrisho kwenye starehe..

Mtu mwenye ukimwi akikohoa tu mnaogopa..
 
Nilikuwa mdogo lakini nachokumbuka 2004 matangazo ya kujikinga na ukimwi yalikuwa mengi sana, NGO's za ukimwi zilikuwa nyingi sana na wasanii wengi walikuwa wakishindana kutoa ngoma kali juu ya elimu ya ukimwi.



Guess what! sasa ukimwi ni kama mafua tu, hakuna mtu anauogopa na ARVs zilifanya kazi yake vyema na bado zinafanya kazi yake.
 
Hakika Mwaka 2004 ulioongoza kwa vipindi vingi vya kutoa elimu ya uelimishaji rika juu masuala ya ngono salama, ngono zembe, athari za ngono zembe, faida za ngono salama, visababishi vya Ukimwi na virusi vya ukimwi, jinsi na namna ya kujikinga na kuwakinga wengine na virusi vya ukimwi na ukimwi.

PSI Tanzania waliendesha kampeni kabambe katika kutekeleza hilo kwa kuja na matangazo mbalimbali ya kwenye vipindi vya redio na luninga (televisheni) vilivyotoa elimu mahususi ya ukimwi na virusi vya ukimwi ikiwa na kaulimbiu mbalimbali zikiwemo :

‘’Kama Kweli Unampenda Utamlinda’’

‘’Salama Chaguo la Kweli’’

"Michepuko Sio Dili" na "Kuwa Original, Tumia Original’’.


Haya matangazo yote yalikua yanalenga matumizi ya kondomu sana sana 'Salama' kondomu.

Bila kusahau mwaka huo huo 2004 kulikua na michezo mbalimbali ya Maigizo kupitia televisheni channel ya ITV na vikundi mbalimbali vilitoa michezo ya maigizo inayotoa elimu kuhusu ukimwi na virusi vya ukimwi, kwa mfano kundi la Nyota Academia km sijakosea walitoa mchezo wa maigizo, ambapo siku hizi nyinyi mnaita tamthiliya ila kipindi hicho sisi tulikua tunaita maigizo au igizo na televisheni ilikua inasema igizo linalofuata, mchezo huo wa maigizo pia uliokua ukitoa elimu kuhusu ukimwi na virusi vya ukimwi na km sijakosea mhusika mkuu aliigiza km muathirika kweli wa virusi vya ukimwi, kwenye igizo hilo muhusika mkuu aliigiza kua ana kikohozi fulani hivi kikavu sana na jinsi alivyokua anajiweka kiugonjwa ugonjwa km mgonjwa kweli wa ukimwi ilipelekea kila mtu alikua anaogopa kupata ngwengwe kipindi hicho.

Kipindi hicho ndio kulikua na makundi mengi ya maigizo yaliyochuana vilivyo kupitia redio na televisheni km vile Kaole Sanaa Group, Mambo Hayo, Kidedea, Kidedea Original, Nyota Academia na mengine sijayataja
 
Duh sasa nimekumbuka kitu maana kuna hio siku niliingia na yule binti kigoli ghetto kwangu ila kabla hatujafanya kitu chochote mara ghafla likapigwa tangazo la kondomu kwenye redio ndio hapo binti akaniuliza 'una kinga?' ilibidi niwahi dukani kwa mangi chapu nikachukue dhana na hio ndio ikawa mara yangu ya kwanza kuvaa Salama kondomu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…