Matukio ya kukumbukwa mwaka 2004

Lydia, Amabilis na Josh wote wapo zao majuu huko duniani, kitambo sana! Dahh! Umenikumbusha mbali sana!
 
Jarida la FEMA limeanza kutolewa mwaka 2000
Wimbo umetoka mwaka 2004, ni vipi wimbo ufanye hilo jarida lianze kutoka ikiwa lilishakua linatoka four years back
 
Umenikumbusha mbali sana enzi hizo nipo bukoba mjini nafanya kazi Na icap , maeneo ya zamzam tulikuwa Na project yetu ya" Ishi" ya kuwakusanya vijana pamoja
 
Ili tangazo linanikumbusha ofisini kwa Baba yangu miaka inakimbia sana
 
Dah! Nachokumbuka ni mwaka ambao naanza kujifunza kuandika na kusoma. Haswa stori za chibwaye mchoyo, kunguru nipe jino lingine halafu eti niko nasari. naweza kusema ndio mwaka nilio fall in love na vitabu. Pia nakumbuka ndio kipindi nilisikia ngoma za ray. C kwa wingi sana. Na za mwanamuziki toni braxton dah! Nostalgic memories
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…