kinyesi.
Wakuu,
1. JK amekabidhiwa nchi ikiwa na amani kabisa, lakini Mheshimiwa huyu amekuwa ni mtu anayejificha kwenye matukio mbali mbali UDHAIFU wake usijulikane!
2. Alianza na Richmond ambayo ilitusumbua sana, hatimaye alivunja Baraza zima la Mawaziri, mambo yakatulia kidogo!
3. Hatujakaa vizuri tukasikia "Zanzibar sio nchi!" Hili nalo lilitusumbua sana hadi kupelekea Mabadiliko ya 10 ya Katiba ya Zanzibar, 1984 ili kuitambua Zanzibar kama "nchi!" Baadaye mambo yakatulia!
4. Tulishuhudia mgomo wa Madaktari na kuteswa kwa ULIMBOKA, lilisumbua sana akili za watu. Matukio mengine yaliyofanana na hayo: Kuuawa kwa wafuasi wa CHADEMA, waandishi wa Habari, Gesi ya Mtwara, nk. Yote hayo yalitufanya tu-concentrate na matukio menyewe zaidi kuliko ku-concentrate na mambo ya maendeleo!
5. Hili la ESCROW sihitaji hata kulielezea maana bado linaendelea kusumbuma akili za watu.
6. Hili la Katiba Mpya nalo limeleta kizaa zaa, ni kama vile limeletwa makusudi ili tugangamane nalo ili Mzee amalize ungwe yake ya Awamu ya Nne!
7. Hili la Mahakama ya Kadhi ndio funga kazi. JK anajua kabisa litatugawanya na litagawanya nchi vipande vipande! Kwa kuwa yeye ni mzee wa matukio yanayo-draw attention kwenye tukio lenyewe badala ya yeye mwenyewe basi tutakomaa nalo wakati yeye anaendelea kumalizia safari zake kwenye nchi ambazo alikuwa bado hajazitembelea! Hana shida na mshikamano na mustakabali wa nchi hii!
8. Bill Clinton alipoona issue yake na Monica Lewinsky imepamba moto, alihamisha attention kwa kuishambulia Iraq. JK naye akishaona kwamba kuna tukio ambalo linamlenga yeye na Serikali yake moja kwa moja analeta tukio jingine. Hili la Katiba lilifunikwa na ESCROW, hili tukio la ESCROW halijaisha tumeshaletewa mambo ya Mahakama za Kadhi.
Tunakorogwa sana kwa kweli! Nikimtafakari JK nashindwa kummaliza! Hapa sijagusia Mgogoro wa Malawi na Rwanda na baadaye na Kenya, Rwanda na Uganda kwa umoja wao! Yaani ni tatizo juu ya tatizo!
Karibuni kwa mjadala zaidi!!