Historia imethibitisha majeshi hayajawahi kuwashinda binadamu hata siku moja.
Napoleone Bonaparte na jeshi lake lenye nguvu alipoivaimia Urusi aliondoka kwa aibu baada ya warusi kuchoma nyumba zao na baridi kali likamfanya Napoleo atoke nduki.
Alipotekwa Mo Dewji tulimsikia rais JPM akisema watanzania sio wajinga, hawawezi kuaminishwa uongo wa kitoto kama alioutoa Rpc Mambosasa. Cctv footage kuonekana kama picha ya kupigwa.
Leo tena IGP amekuja na habari ambazo ukipita kila kijiwe ni maswali ya kujiuliza tu. Askari apotee tar 26 Oktoba, polisi mje kutoa taarifa November 19? Hii baada ya manugu'niko ya watu juu ya kuwepo taarifa za watu kupigwa risasi hovyo na hakuna hatua stahiki zinazochukuliwa
Achana na ukatili huko Pemba maana mnaweza kujustify matumizi ya nguvu kwa sababu mnadai kunawatu walivamia maofisa wa Zec. Je huku bara, mbona watu wanabambikiwa kesi kila kukicha? Mbona watu wanapigwa na kuuwawa bila makosa? Matukio ya polisi kunyanyasa na kutesa raia ni mengi sana. Mfano kuna mama mmoja kule Moshi, aliwahi kuomba msaaada kwa rais JPM maana mtoto wake alinyongwa ndani ya kituo cha polisi.>>> https://www.jamiiforums.com/threads...ujinyonga-kwenye-chumba-cha-mahabusu.1487355/
Namaaliza kwa kusema ipo siku watanzania na upole wao watanyanyuka na kudai haki zao. Maana watanzania sio wajinga bali huwa wanauchuna tu sababu mnadhania ni wajinga.