BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 706
- 1,716
“Tulibebeshwa miili ya marehemu waliopigwa risasi… hali hii imetuathiri kisaikolojia, tusaidiwe.”
Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 29, 2025 umeripotiwa kuambatana na matukio mengi ambayo kwa raia wengi yalikuwa mapya na ya kutisha. Simulizi kwenye mitandao ya kijamii na mitaani zimeacha huzuni, mshangao na makovu ya kisaikolojia ambayo wahanga wanadai ni vigumu kuyasahau.
Katika pitapita zangu, nimekutana na watu kadhaa wanaodai vichwa vyao vimebeba kumbukumbu ngumu ambazo zimegoma kufutika.
Kijana mmoja (28) mkazi wa Dar es Salaam anaeleza kuwa siku ya uchaguzi aliamka mapema na kuelekea kazini maeneo ya Kinondoni. Baada ya kufika ofisini, walichukua gari la ofisi na kuelekea kutekeleza majukumu yao ya kila siku.
“Tulipofika maeneo ya Magomeni, tulisimamishwa na watu tuliowakuta barabarani bila kuwafahamu. Walitulazimisha kubeba miili miwili ya marehemu na kuipeleka hospitali (anaitaja). Tukio hili lilituumiza sana mimi na dereva, mpaka sasa halijatoka kichwani.”
Mkasa kama huo unaelezwa na mwananchi mwingine aliyekuwa akipita eneo la Buguruni na gari lake binafsi. Anadai alitishiwa na kulazimishwa kubeba miili ya marehemu na kuipeleka hospitali jijini Dar es Salaam. Anasema tukio hilo limebaki kuwa kovu lisilofutika katika maisha yake.
Pia soma ~ Tume yasema waathirika wa Oktoba 29 watapatiwa huduma ya Kisaikolojia
Sambamba na hao, mkazi mmoja wa Mbezi anasimulia kuwa siku moja baada ya uchaguzi, akiwa anaenda dukani, alikamatwa pamoja na mwenzake na kupakiwa kwenye gari la watu wasiojulikana waliokuwa na silaha. Waliambiwa waende nao kukusanya miili ya watu waliouawa kwa kupigwa risasi kutoka Kimara hadi Mbezi.
“Tulipelekwa mpaka Kimara na tukaambiwa tutapakia miili kwenye gari lao. Wakatuonya kwamba yeyote atakayesita atapigwa risasi. Kwa hofu, tulikusanya miili kwa takribani saa nne. Baadaye walituacha njiani mmoja mmoja. Mimi nilishushwa nikiwa mtu wa tatu. Mpaka sasa akili yangu haipo sawa nikikumbuka kilichotokea.”anaeleza
Taarifa kutoka kwenye jamii zinadai kuwa baadhi ya watu walipigwa risasi mbele ya ndugu na jamaa zao, wengine wakiwa majumbani kwao, tukio linalodaiwa kuacha majeraha makubwa ya kisaikolojia.
Katika uchunguzi wa video iliyochapishwa na CNN, inaonekana mama mjamzito akipigwa risasi mgongoni mbele ya ndugu zake. Video hiyo imeibua mjadala mkali mtandaoni, watu wakijiuliza hali ya kisaikolojia ya waliokuwa mashuhuda.
Kwa wiki mbili tangu kuruhusiwa kwa intaneti, mitandao ya kijamii imefurika video zinazodaiwa kuonesha matukio yaliyotokea kipindi cha uchaguzi: watu wakipigwa risasi, miili ya marehemu mitaani na hospitalini, pamoja na picha za majeruhi.
Baadhi ya video zimekanushwa na mamlaka zinazodai zimetengenezwa kwa nia ovu. Hata hivyo, athari za kisaikolojia kwa watumiaji wa mitandao ikiwemo watoto zimeendelea kutabiliwa kuonekana.
Mwanasaikolojia anasema nini?
Baada ya kutafakari matukio hayo, nilizungumza na mtaalamu wa masuala ya saikolojia ambaye anaeleza kuwa athari zilizoachwa ni kubwa kuliko inavyoonekana.
“Wengi hawakutarajia mambo kama haya kutokea. Hata baadhi ya viongozi huenda hawakuyatarajia. Hilo peke yake linaweza kuacha kovu la kisaikolojia. Sasa fikiria waliowaona ndugu zao wakiuawa au kujeruhiwa. Ninaliona hili kama tatizo litakalozidi kuwa kubwa endapo watu hawa hawatasaidiwa."
Anaendelea: Nilijizuia kuingia mtandaoni kwa muda
“Mara baada ya mtandao kurudi, nilijihisi kuzidiwa na maudhui ya kutisha na nilijizuia kuingia mtandaoni kwa wiki nzima. Hata mke wangu nilimshauri afanye hivyo. Ubongo wa binadamu unapokutana na tukio jipya lenye sura mbaya, hupata tabu kulihifadhi na kuelewa uzito wake. Hapo ndipo mara nyingi matatizo ya kisaikolojia huchipukia.” anaeleza
Mtaalamu huyo anashauri mamlaka zichukue hatua za haraka kuwatumia wataalamu kutoa msaada wa kisaikolojia kwa waathirika. Anaonya kuwa kovu la matukio hayo likiachwa bila kutibiwa, linaweza kuathiri hisia za uzalendo na kusababisha visasi vya muda mrefu.