BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
Nimekaa nikatafakari kuhusu matukio ya utekaji yanayoendelea Nchini, sisi Wananchi tumekuwa tukiumia kadiri siku zinavyoenda, matukio ya utekaji yanaendelea, imani yetu kwa vyombo vya Ulinzi inaanza kupotea.
Mawazo hayo yamekuja baada ya kuona tukio la Mfanyabiashara Deogratius Tarimo alivyonusurika kutekwa na Watu ambao hawajulikani lakini angalau sura zao tumeanza kuziona.
Tukio hilo limeanza kutupa hofu Wananchi wengi wa kujiona hatupo salama, kama matukio yanafanyika mchana kweupe, sura za Watu zinaonekana huku Vyombo vya Usalama vikiishia kusema uchunguzi unafanyika baada ya hapo tunasahau tunasubiri tukio lingine, naona sio sawa.
Pia soma - Inasemekana tukio hili la utekaji limetokea Kiluvya, kutokana na uzito wa jamaa walishindwa kumchukua. Hakuna aliyetoka kumsaidia
Pia soma - Polisi watoa tamko tukio la jaribio la utekaji Kiluvya, wasema uchunguzi umeanza toka aliporipoti Novemba 11, 2024
Inawezekana Watu hawasemi lakini haya mambo yanayofanyika hivi, mdogomdogo yanazidi kuwaaminisha Wananchi kuwa hatupo salama. Serikali inatakiwa kufanya maamuzi magumu kuhusu hao "Watekaji" au ambao "Hawajulikani", tutaishi kwa hofu hivi hadi lini?
Miaka ya nyuma ilikuwa utekaji unafanyika kwa kificho, kama imefikia hatua mambo yanafanyika hadharani basi tunaelekea kubaya.
Hii ni mifano michache tu ya matukio ya hivi karibuni ya Mwaka 2024, achana na yale ya kina Roma na kina Mo Dewji na wengine wengi, haya machache ni ya mwaka huu, mnaweza kunikumbusha mengine pia:
Juni 2024: Edger Mwakalebela “Sativa” alitekwa akiwa Dar es Salaam akapatikana Katavi akiwa amejeruhiwa vibaya, Jeshi la Polisi likasema linafanya uchunguzi.
SATIVA: Nilitekwa nikapelekwa Karakana ya Polisi Oysterbay kabla ya kusafirishwa sehemu nyingine na nimepigwa risasi ya kichwa
Septemba 2024: Mwanachama wa CHADEMA, Ally Mohamed Kibao alichukuliwa na Watu wasiojulikana ndani ya basi, mwili wake ukapatikana baadaye akiwa ameuawa. Jeshi la Polisi likasema linafanya uchunguzi.
Kuelekea 2025 - Polisi: Tunachunguza kubaini chanzo na watu waliohusika kumchukua Ali Kibao
Novemba 2024: Mkurugenzi wa Dar24 Media, Maclean Mwaijonga alipotea kwa siku mbili akiwa hajulikani alipo, Taasisi yake ikatoa taarifa kwa umma, akapatikana Kigamboni na kueleza kuwa alikuwa na Watu anaofanyanao biashara, akanywa juisi ambayo anaamini ilimfanya akapoteza fahamu.
Mkurugenzi wa Dar 24 apatikana Kigamboni
Agosti 2024: Kijana Shadrack Chaula (24) alichukuliwa na Watu wasiojulikana Mkoani Mbeya, Wazazi wake wakajitokeza kuomba msaada wa kumtafuta kijana wao, Jeshi la Polisi likasema linachunguza na kumtafuta mhusika.
Sakata la kijana aliyechoma picha ya Rais kutoweka lawaibua polisi
Novemba 2024: Vijana wawili walipoteza maisha kwa kupigwa risasi, wengine wawili walijeruhiwa vibaya ikidaiwa walikuwa wakiwakimbia Askari Polisi, chanzo kikidaiwa ni kesi ya uchimbaji mchanga, Jeshi la Polisi likasema linafanya uchunguzi.
Zanzibar: Vijana wawili wauawa na wengine 2 kuumizwa vibaya. ACT yataka Jeshi na Polisi kufanyiwa mabadiliko Kimuundo na Kiutendaji
Julai 2024: Mwanachama wa CHADEMA - Tanga, Kombo Mbwana alipotea kwa siku 29, Jeshi la Polisi likatangaza kuwa lilikuwa likimshikilia, akikabiliwa na kesi ya Jinai.
Tanga: Mahakama kutoa uamuzi kuhusu Polisi kuendelea kumshikilia Kombo Mbwana
Unadhani matukio kama haya yanatoa picha gani kuhusu hali ya usalama wetu Wananchi? Ni kweli watu kama hawa hawajuliani?