Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Nimesoma kwamba katibu wa CCM wa wilaya ya Kilolo ameshambuliwa na kuuwawa kwa risasi na watu wasiojulikana. Hivi karibuni huko Songwe kulikuwa na tukio jingine la katibu wa CCM kuvamiwa wa watu wasiojulikana na kuvunjwa miguu.
Songwe: Katibu wa CCM avamiwa na watu wasiojulikana na kuvunjwa miguu yote miwili
Sasa, watu wenye akili walijua kwamba hili lilikuwa ni suala la wakati tu kabla ya kuanza kutokea, kwamba kuna wakati haya matokio dhidi ya viongozi wa CCM yangeanza kutokea, na kuna uwezekano mkubwa yataendelea sana.
Sababu ni kwamba, kwa muda mrefu sana, watu walioonekana kuwa wako vyama vya upinzani ndio walifanyiwa utekeaji na hata kuuwawa. Kila watu walipolalamika, serikali ya CCM haikutaka kuchukua hatua. Katika hali ambayo watu waliouwawa mara zote walikuwa walioonekana kuikosoa au kuikashifu CCM na serikali yake, uongozi wa CCM ulionekana "kufaidika" na kutekwa au kuuwawa kwao, ndio maana kukawa na hisia kuwa vyombo vya dola vilihusika na matukio ya utekaji na uuaji wa hawa watu.
KIla mtu anajua kwamba uongozi wa serikali haikulishinikiza jeshi la polisi kufanya uchunguzi juu ya matukio ya uuaji na utekaji.
Sasa uonevu huu wa muda mrefu wa watu wa upinzani ni wazi ulitoa muda wa kutosha kwa upande wa waliotekwa na kuuwawa kujipanga na kuanza kufanya yale ambayo waliona kuwa wakifanyiwa, bila serikali kuchukua hatua. Matokeo ndio haya tunayaona Kilolo, Songwe, na sijui waapi kwingineko tutarajie.
CCM na serikali yake wanapaswa kulaumiwa kwa haya matukio yanayohusu utekaji uuaji nchini, iwe yanafanywa na kwa sababu za kisiasa au kijambazi, dhidi ya wapinzani au CCM. Mmelilea jambo hili, mliamua kukaa kimya badala ya kulizuia na hatimae wale waliokuwa wakionewa kwa muda mrefu ni wazi walifikia muafaka kwamba njia pekee ni kuwapa radha ya dawa mliyoitengeneza wenyewe dhidi ya wapinzani na wakosoaji wa serikali.
Ni wazi kwamba hawa wanaofanya matukio haya dhidi ya viongozi wa CCM wameandaliwa kwa muda mrefu, na wana ujuzi wa kufanya kile ambacho waliona mnawafanyia wao.
Mliona mkuki kwa nguruwe ni mzuri sana, na sasa mtaona uchungu wa mkuki kwa binadamu, kwa sababu nyie mlijiona ni binadamu na watu wa upinzani waliokuwa wakitekwa na kuuwawa ni nguruwe na hivyo hamkupaswa kufanya chochote. What goes around comes around.