Matukio ya viongozi wa CCM kuanza kushambuliwa na kuuawa wa kulaumiwa ni CCM na serikali yake, wameyalea kwa muda mrefu na sasa yanawageukia

Kuna jumuia kubwa tu ya Watanzania wakisikia askari polisi au kiongozi wa CCM amekufa wanafanya sherehe. Nani anatutoa katika ubinadamu kiasi hiki? Si kuna wakati Watanzania wote tuliitana ndugu?
Ni matunda ya ukaburu wa CCM kuwabagua wapinzani na kuwaona kama ni wahaini wasiostahili kuwepo Tanzania licha ya kuwa Katiba ya Tanzania inatamka wazi kuwa Tanzania ni nchi ya vyama vingi.

Mifano hai ni jinsi wagombea wa upinzani walivyoenguluwa katika mchakato unaoendelea wa uchaguzi wa serikali za mitaa.

Mfano hai mwingine ni jinsi viongozi wa upinzani wanavyotekwa,wanavyoteswa,wanavyo funguliwa kesi za uongo na wengine kupotezwa na kuuwawa kikatili na vyombo vya dola. Mambo haya yamepelekea chuki inayojionyesha sasa na huu ni mwanzo tu kinachofuata ni uhasama na uadui ambao utaishia kwenye vita ya wenyewe kwa wenyewe,hakuna mtu mwenye akili timamu anayeombea tufike huko lakini viongozi wa sasa wa CCM na Serikali yake wanatuelekeza huko.
 
Hii ni michezo yao wenyewe
 
Ni muhimu sana kutenganisha watu kutolewa kafara na vijana kuchukuliwa misukule kichawi na watu wa chama chao, kwasabb tu ya uongozi ndani ya chama, na mtu kupigwa risasi wazi wazi kabisa suala ambalo ni specific πŸ’
Lisu alipigwa risasi pia, nalo ni hiyo specific?
 
πŸ€”πŸ€”πŸ€”
 
Gentleman, acha upotoshaji wa kishirikiana πŸ’
Ni zamu yenu sasa kuweka mahema ya matanga.
Hatufurahii kifo cha mtanzania yeyote. Lakini muuaji anapokuwa anapunguzwa nguvu tunapata haueni.

Kifo ni kifo tu
 
Hawa jamaa wa CCM na serikali yao wanetuharibia sana nchi yetu.Na kosa lao kubwa ni kuhisi wanahati miliki ya hii nchi. Wameparalyse mifumo ya haki, polisi, usalama, majeshi hadi bungeni - tunawatu wanainterest na CCM kuliko taifa lao...Kama taifa tunahutaji ukombozi wa pili - hakuna accountability - ni kama hakuna viongozi - Cha ajabu tunakutana na ving'ora na misafara ya ajabu ajabu..unajiuliza hivi hawa watu wanajua wajibu wao kweli??
Wali- initiate kutekana na mambo ya risasi - tangu kwa Lissu..tukafikiri bahati mbaya - tukamsema Magufulu - kumbe tayari ni kama system imekaa kabisa....watu wakaendelea kupotea na serikali hiyohiyo inachukua kodi zetu inashindwa kutoa majibu - Polisi hawasemi chochote ni kama dhamira zinawasuta..
Haya sasa haya mambo ni lazima yataenda out of control....mama wa watu kala chuma ---mwanaccm huyo...Na hii hali wakiendelea kuifumbia mambo wataanza kuuwana sana.....Dhambi ya usaliti kwa watanzania itawatafuna tu....
NA TUNASEMA IWATAFUNE NYOTE..MVURUGANE..MTWANGANE MPAKA AKILI ZIWAKAE SAWA
 
Matukio ya viongozi wa CCM kushambuliwa na kuuawa yanapaswa kulaumiwa kwa CCM na serikali yake, kwa sababu wameyalea kwa muda mrefu na sasa yanawageukia.

Je, hii ni laana ya Magufuli? Na Samia amekaa kimya!

Kwanini yeye, kama mwenyekiti wa chama, hatoi maelezo?
 
Magufuli alikuwa kinara wa huu uhalifu wa watu kutekwa, kupigwa risasi na kuuwawa bila hatua kuchukuliwa.
 
Na yote haya yanafanywa na Mtanzania dhidi ya Mtanzania mwenzake, sometimes watu wa kabila moja, dini moja? Unajua sometimes nauelewa uhasama wa Rwanda kati ya Watusi na Wahutu, lakini sio huu wa Tanzania kati ya CCM na vyama vingine. Ni wa ajabu sana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…