Matukio ya watu kupotea na kutekwa na 'watu wasiojulikana' kuendelea kuzua hofu kwa wananchi, nini sababu ya matukio haya?

Matukio ya watu kupotea na kutekwa na 'watu wasiojulikana' kuendelea kuzua hofu kwa wananchi, nini sababu ya matukio haya?

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Joined
Aug 7, 2018
Posts
685
Reaction score
1,124
utekaji.jpg

Matukio ya Watu Kupotea katika mazingira ya kutatanisha, Kutekwa na wanaoitwa 'Watu Wasiojulikana', na wengine Kuuawa yameendelea kuzua hofu miongoni mwa Wananchi. Je, ni nini sababu ya Matukio haya?

Ungana nasi katika mjadala maalum kupitia X Spaces ya JamiiForums kujadili matukio haya na kutafuta suluhisho leo Ijumaa, Novemba 15, 2024, Saa 12:00 Jioni hadi Saa 2:00 Usiku

Kushiriki mjadala kupitia XSpaces ya JamiiForums ingia hapa

Tukio lililotokea hivi karibuni soma hapa: Inasemekana tukio hili la utekaji limetokea Kiluvya, kutokana na uzito wa jamaa walishindwa kumchukua. Hakuna aliyetoka kumsaidia

Kwa matukio mengine ya utekaji yaliyowahi kutokea nchini ingia hapa: Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana

========================================

MAONI YA WACHANGIAJI WALIOPO KWENYE MJADALA

Fulgence Massawe - Mkurugenzi na Maboresho LHRC Alisema Yafuatayo:

"Kwanza nianze kwa kuzungumzia kwa kurejea Kifungu cha 13 cha Mwenendo wa Makosa ya Jinai Sura Namba 20, kilichofanyiwa maboresho Mwaka 2019 / 2020Hakuna kosa ambalo mtu anakwenda kukamatwa bila kuwa na Arrest Warrant (Hati ya Kukamatwa) lakini Askari anaweza kumkamata Mtu bila hati hii kama inapotokea ameshuhudia mtu akifanya kosa mbele yake au anapozuia Askari kufanya kazi yake au anapoona ana kitu ambacho ni hatarishi. Pia, kuna makosa ya zamani kama vile uzururaji"

"Kuundwa kwa Tume ya Haki Jinai ni dalili ya kuonesha kuwa Serikali inatambua juu ya uwepo wa matukio ambayo yanahitaji kuwa na Mamlaka hiyo"

"Kama Polisi wenyewe wanaendesha Magari ambayo hayatambuliki, hayana namba na mambo mengine kama hayo, fursa kama hiyo inaweza kutumiwa na Watu wenye nia mbaya pia kufanya uhalifu Mitaani na wasijulikane kwa kuwa Jeshi la Polisi limekuwa likionesha ni jambo la kawaida"

"Inapotokea hivyo Askari anakuwa hana muda wa kutafuta au kwenda kuchukua Arrest WarrantKwenye Nchi ambazo zina Mfumo wa Utawala wa Sheria, Watu wanaoongoza kuzingatia mfumo huo ni Vyombo vya Usalama"

"Inapotokea Polisi wanafanya majukumu yao ikiwemo kukamata bila kuzingatia misingi ya Kisheri, mfano kuwa na Sare au Vitambulisho, ni rahisi Watu ambao hawapo katika majukumu ya Jeshi la Polisi nao wakaingia na kufanya hivyo pia"

"Kuna matukio mengi yametokea Tanzania ambayo mengine yalifanyika hadharani ikiwemo lile la Nape Nnauye, Ali Kibao na mengine mengi, lakini mpaka leo wahusika hawakuchukuliwa hatua licha ya kuwa matukio mengine Serikali ilijitokeza na kuahidi kuchukua hatua"

"Siyo kila Mtu anayekamatwa anatakiwa kufungwa pingu, bastola kupigwa juu, sio kila tukio linatakiwa kutumia nguvu kumkamata mtuhumiwaKuna Watu ambao walijipeleka wenyewe Vituo vya Polisi lakini walipofika walivyopokelewa nguvu zilitumika"

"Tulipendekeza kuundwa kwa Chombo Huru (Police Oversight Board) ambacho kinaweza kupokea malalamiko dhidi ya Jeshi la Polisi, tulionesha hadi mfano wa jinsi chombo hicho kinavyoweza kufanya kaziChombo kama hicho kiliundwa Afrika Kusini ambapo kulikuwa na changamoto awali kuhusu Jeshi la Polisi na kikawasaidia sana, kuna umuhimu wa sisi Tanzania kuwa na chombo kama hicho"

Mohamed Kibao - Muathirika Wa Matukio Ya Utekaji Alisema Yafuatayo:
"
Kuna umuhimu wa Wananchi kufahamu Haki zao za Kisheria, wengi wetu hatujui hata wapi pa kuanzia inapotokea kuna jambo limetukuta"

" Tuna mashaka kama Haki itatendeka kuhusu tukio la kifo cha Ali Kibao, kama hisia zetu sio sahihi basi tupo tayari kukosolewa katika hilo Inawezekana ni jambo ambalo linaweza kupotea kimya kimya kama ambavyo imetokea katika matukio mengine kadhaa"

"Hatuhisi kama haki itatendeka lakini tutaendelea kupigania. Sisi Familia tunaendelea kupambania lakini hatuna ImaniUkosefu wa Imani kwa Vyombo vya Usalama umeongezeka kwetu, kuna wakati Mtu akikupigia simu anataka kuja kusalimia Familia, tunaanza kujiuliza sisi wenyewe kuwa anayekuja au wanaokuja ni Watu salama kwetu, tunaanza kujiuliza kuhusu usalama wetu"

"Unaweza usiione hiyo hali kama hujafikwa, mfano Septemba 6 (2024) tulipoambiwa mzee wetu amechukuliwa kwenye basi hatukujua nini cha kufanya kwa kuwa hatukujua nini kinatakiwa kufanyikaNdio maana napenda uwepo wa mijadala inayoweza kusaidia ufahamu kama hii kwa kuwa kuna mambo au kuna vitu vya kujifunza kwa Watu wote"

"Pia, kuna hali ya Watu kukata tamaa kuhusu matukio ya utekaji, wanasema ‘tayari imeshatokea’, hivyo hakuna cha kufanya, sijui hali hiyo tutaiweka sawa vipi lakini nadhani jambo la kwanza muhimu ni kutambua Haki zetu"

"Mimi nilikuwa mmoja kati ya Watu ambao walikuwa wanaona matukio ya utekaji yanatokea na kuripotiwa katika Vyombo vya Habari lakini sikuwa nafuatilia kwa kuwa sikujua kama siku moja linaweza kunikuta
Sikuwa mmoja kati ya Watu waliokuwa wakipiga kelele au kusema chochote juu ya matukio ya utekaji, nasema hilo ili wengine wajifunze na watambue nami nilikuwa katika njia ipi"

"Mila na Desturi za Utendaji kazi wa Idara zetu za Vyombo vya Dola vipo chini ya Ibara ya 9 ya Katiba, inawezekana Katiba yetu ikawa na changamoto lakini wanaosimamia Katiba hiyo wakawa na ubaya zaidi'

"Tutaendelea kupigania Haki na kuhakikisha inapatikana kuhusu kifo cha mzee wetu (Ali Kibao) hata kama itachukua muda mrefuTulipewa ushauri wa kushirikiana na wanaotetea au wanaopambania masuala ya Haki ili haya yaliyotukuta yasiwakute wengine ambao hayajawakuta"
"Viongozi wenye dhamana wakiwemo Waziri wa Mambo ya Ndani, IGP na wengineo, kuchelewa kwao kufanya maamuzi ya uchunguzi kunawafanya nao waonekana kuwa ni sehemu ya mfumo mbovuNafasi bado ipo wanaweza kufanya mabadiliko ikiwemo kuunda Tume za kuchunguza masuala hayoLeo tunalia sisi, huwezi jua kesho Mtawala atakuwa nani, inawezekana kesho ikawa wao ndio wapo upande wa pili wanalia"

Boniphace Mwakubusi - Rais Wa TLS alisema yafuatayo:

"Sisi TLS tulianza kuwaonesha Watanzania kuwa huu sio wakati wa kufanya utani, tunatakiwa kupata majibu ya nani anafanya matukio ya UtekajiTLS ilikusanya Wadau kuanza kujadili matukio kama hayo, hata hiki kinachofanywa na JamiiForums ni kitu cha kupongeza. Haiwezekani Mtu au Watu wanapotea na Serikali inaendelea kuwa kimya tu"

"Tuna changamoto katika Mfumo wa Haki Jinai, tuna changamoto ya kutothamini uhai, kuna Watanzania wanaona uhai wa Mtu ni kitu cha kawaida kama vile kudondosha Tsh. 500"

" Ifike hatua tunapozungumzia Maisha tutambue kuwa hakuna aliyeyatengeneza zaidi ya MunguTunapofika hatua tumeshindwa kupata utatuzi basi tuombe msaada. Serikali inaonesha inafanya kazi lakini kama hicho wanachokifanya hakiendani na uhalisia"

"Nitoe mfano hata lile tukio lililotokea hivi karibuni, majibu ya yule aliyekuwa anatarajiwa kufanyiwa utekaji nayo yanatia shaka, ningekuwa mimi ningewaambia hata Polisi nao wamuhoji muathirika"

"Nitoe mfano hata lile tukio lililotokea hivi karibuni, majibu ya yule aliyekuwa anatarajiwa kufanyiwa utekaji nayo yanatia shaka, ningekuwa mimi ningewaambia hata Polisi nao wamuhoji muathirika"

"Tunatakiwa kuwa na mfumo thabiti wa Ulinzi kwa raia, Mahakama nazo zitimize majukumu yake inavyotakiwa kuliko kuishia kusema Polisi inafanya upelelezi kisha inaishia hivyo hivyoMaisha ni zawadi pekee tuliyopewa na Mungu, uhai haukupigiwa kura, hivyo ni suala linalotakiwa kuheshimiwa"

"Polisi wanalaumiwa kuhusu matukio ya utekaji kutokana na kigugumizi chao, wamekuwa wakifanya uchunguzi ambao haumalizi kwa Miaka mingi Kuna matukio kadhaa ambayo yalitokea na Jeshi la Polisi likafanya kazi kwa weledi wa kiwango cha juu, siamini kama Polisi hawawezi kufanya kazi kwa weledi"

Boniface Jacob - Mwenyekiti wa CHADEMA kanda ya Pwani alisema yafuatayo:

"Taifa Makini linatakiwa kujiuliza kwanini kuna matukio ya utekaji na Watu kupotea, kunapokuwa na nadharia hizo inamaanisha kuna tatizo

Uzoefu wangu unaonesha kuwa taarifa za kupotea nyingi ziliendana na matukio yanayoendana labda na uhalifu, mfano kuna mtu alinunua 'simu used' ambayo ilikuwa na tatizo ikafuatiliwa inabainika ni yeye, hivyo wanaweza kuhisi mtu huyo anaweza kuwa sehemu ya tatizo la uhalifu"

"Nadharia ya pili kuhusu matukio ya Watu kupotea yanaendana na wale Watu wajanja wajanja ambao hawana kazi ya kueleweka, inaweza kutokea kachukuliwa, anapotea"

"Nadharia nyingine ni kuwa wapo wanaodai kuna watu ndani ya Serikali au Vyombo vya Dola wanakuwa na sababu zao binafsi, labda wanapishana au wanaweza kuamua kufanya uhalifu ili Serikali ichafukeHapo pia kuna nadharia kuwa kuna matukio ya aina hiyo yanayofanywa na Kikosi Kazi. Kikosi kama hicho kinaweza kwenda kukamata mtu au Watu na kuwapeleka sehemu ambazo hazijulikani"

"Pia, imeelezwa kuwa Usalama wa Taifa nao wanaruhusiwa kukamata, zamani mtu yeyote alikuwa akikamatwa basi mchakato huo unafanywa na Jeshi la Polisi, sasa hivi hali imekuwa tofauti, kuna Mamlaka nyingine nazo zinajihusisha kukamata Watu"

"Polisi wanalaumiwa kuhusu matukio ya utekaji kutokana na kigugumizi chao, wamekuwa wakifanya uchunguzi ambao haumalizi kwa Miaka mingi Kuna matukio kadhaa ambayo yalitokea na Jeshi la Polisi likafanya kazi kwa weledi wa kiwango cha juu, siamini kama Polisi hawawezi kufanya kazi kwa weledi"

"Kuna matukio ambayo Watu walikuja wakanieleza, nikawaeleza kuwa kwa suala hilo mnaweza kumuona Waziri, lakini ikafikia hatua hata Waziri mwenyewe anamwambia Mtu aliyeenda kuwasilisha suala lake kwake kuwa “huogopi?

”Kama Waziri mwenyewe anamwambia raia kuwa haogopi katika suala la kupotea kwa Mwanaye akiamini wanaohusika wana nguvu zaidi yake yeye, unadhani nini kinaendelea hapo?"

"Nadharia nyingine ya masuala ya Utekaji ni kuwa kuna vikundi vya uhalifu ambavyo vinapatikana ndani ya Vyombo vya Usalama, havijatumwa wala kupewa maelekezo na Viongozi wao, wanafanya hivyo kwa maslahi yao binafsi Mifano ya matukio kama hayo ipo imekuwa ikitajwa, mfano kuna kesi ilitokea kule Kagera na Askari wakabainika kujiuhusisha na matukio ya uhalifu"

"Nipongeze Jeshi la Polisi kwa kiasi fulani kuwa siku hizi Wakuu wa Vituo nao wamekuwa waoga kupokea Watu wanaokamatwa au kufikishwa vituoni kwao na Vikosi Kazi, kwa kuwa wanajua ni hatari kwao huyo mtu au Watu wakipoteza Maisha mkononi mwakeHali hiyo imesababisha pia kuwepo na vituo kadhaa vinavyotengeneza mazingira ya Vikosi Kazi kuanzisha vituo vyao vya kutesa Watu"

HAPPINE (Mdau):

"Haki ya Binadamu ni Haki ya Binadamu, tujiulize kwanini Watu wanashindwa kuingilia wanapoona Mtu anakamatwa kinyama?Utekaji unatokea pia hata kwa Watu wenye uwezo wa Kiuchumi, ilitokea hivyo kwa Mo Dewji, yupo vizuri kiuchumi lakini alitekwa, yametokea mauaji ya Kiongozi wa CCM wa Iringa, hili sio suala la Uchama, tunatakiwa kulipinga"

NICKODEM SIMCHIMBA (Mdau):

"Kuna Watu wanaona haya mambo ya utekaji hayawahusu, hao ni wale ambao labda wapo kwenye Utawala au wapo kwenye nafasi nyingine Kundi la pili ni wale ambao wanajiona wapo hatarini kutekwa au kufanyiwa matukio mabaya"

"Sisi kama Taifa tumekuwa na ubinafsi, hatujali Maisha ya Watu wengine, kwanini tumefika huko? Kwanini tusiwe mstari wa mbele kupigania uhai wa wenzetu?
Tunatakiwa kuwa kitu kimoja ili kulinda uhai wa wenzetu, tunatakiwa kutambua kuwa sisi ni ndugu"
 
👉 Udicteta wa serikali kuamini kila anayetoa maoni ni mpinzani wao hivyo kumfanyia njama za utekaji

👉 Roho mbaya na tamaa ya uongozi kwa wanasiasa kusalitiana wao kwa wao na kuishia kutoana roho.

👉 Matukio ya visasi kwa raia ambao wanahusishwa na kutembea/kuchepuka na mme/mke wa mtu, hivyo kufanyiana njama za utekaji/mauaji na matokeo yake kutokana na trend hii ya utekaji mzigo wote wanaubeba wanasiasa/serikali/CCM kuwa wamehusika hata kwa matendo wasiyohusiana nayo.

Serikali ikiendelea kuchekeleq hii tabia ipo siku tutaongea lugha moja.
 
Sababu kuu ni Watu kushindwa kujibu hoja za wengine, sasa ili kuzima mijadala hiyo inaelekezwa kuua wadadisi, hii nchi inataka watu wawe wajinga wasioweza kuhoji ili walio madarakani waendelee kufanya watakavyo

Unaweza kuhoji jambo dogo tu linalohitaji ufafanuzi wa kawaida kabisa lakini ukatishwa au ukatekwa kabisa na kupotezwa

Kwa Nchi kama Tanzania ya sasa kuhoji jambo lolote ni sawa na Uhaini
 
Tawala zinazoelekea mwishoni hufanya sana haya mambo aidha kwa kuchanganyikiwa ama kwa hofu
 
Matukio ya Watu Kupotea katika mazingira ya kutatanisha, Kutekwa na wanaoitwa 'Watu Wasiojulikana', na wengine Kuuawa yameendelea kuzua hofu miongoni mwa Wananchi. Je, ni nini sababu ya Matukio haya?

Ungana nasi katika mjadala maalum kupitia X Spaces ya JamiiForums kujadili matukio haya na kutafuta suluhisho leo Ijumaa, Novemba 15, 2024, Saa 12:00 Jioni hadi Saa 2:00 Usiku

Kushiriki mjadala kupitia XSpaces ya JamiiForums ingia hapa

Tukio lililotokea hivi karibuni soma hapa: Inasemekana tukio hili la utekaji limetokea Kiluvya, kutokana na uzito wa jamaa walishindwa kumchukua. Hakuna aliyetoka kumsaidia

Kwa matukio mengine ya utekaji yaliyowahi kutokea nchini ingia hapa: Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana

========================================

MAONI YA WACHANGIAJI WALIOPO KWENYE MJADALA

Fulgence Massawe - Mkurugenzi na Maboresho LHRC Alisema Yafuatayo:

"Kwanza nianze kwa kuzungumzia kwa kurejea Kifungu cha 13 cha Mwenendo wa Makosa ya Jinai Sura Namba 20, kilichofanyiwa maboresho Mwaka 2019 / 2020Hakuna kosa ambalo mtu anakwenda kukamatwa bila kuwa na Arrest Warrant (Hati ya Kukamatwa) lakini Askari anaweza kumkamata Mtu bila hati hii kama inapotokea ameshuhudia mtu akifanya kosa mbele yake au anapozuia Askari kufanya kazi yake au anapoona ana kitu ambacho ni hatarishi. Pia, kuna makosa ya zamani kama vile uzururaji"

"Kuundwa kwa Tume ya Haki Jinai ni dalili ya kuonesha kuwa Serikali inatambua juu ya uwepo wa matukio ambayo yanahitaji kuwa na Mamlaka hiyo"

"Kama Polisi wenyewe wanaendesha Magari ambayo hayatambuliki, hayana namba na mambo mengine kama hayo, fursa kama hiyo inaweza kutumiwa na Watu wenye nia mbaya pia kufanya uhalifu Mitaani na wasijulikane kwa kuwa Jeshi la Polisi limekuwa likionesha ni jambo la kawaida"

"Inapotokea hivyo Askari anakuwa hana muda wa kutafuta au kwenda kuchukua Arrest WarrantKwenye Nchi ambazo zina Mfumo wa Utawala wa Sheria, Watu wanaoongoza kuzingatia mfumo huo ni Vyombo vya Usalama"

"Inapotokea Polisi wanafanya majukumu yao ikiwemo kukamata bila kuzingatia misingi ya Kisheri, mfano kuwa na Sare au Vitambulisho, ni rahisi Watu ambao hawapo katika majukumu ya Jeshi la Polisi nao wakaingia na kufanya hivyo pia"

"Kuna matukio mengi yametokea Tanzania ambayo mengine yalifanyika hadharani ikiwemo lile la Nape Nnauye, Ali Kibao na mengine mengi, lakini mpaka leo wahusika hawakuchukuliwa hatua licha ya kuwa matukio mengine Serikali ilijitokeza na kuahidi kuchukua hatua"

"Siyo kila Mtu anayekamatwa anatakiwa kufungwa pingu, bastola kupigwa juu, sio kila tukio linatakiwa kutumia nguvu kumkamata mtuhumiwaKuna Watu ambao walijipeleka wenyewe Vituo vya Polisi lakini walipofika walivyopokelewa nguvu zilitumika"

"Tulipendekeza kuundwa kwa Chombo Huru (Police Oversight Board) ambacho kinaweza kupokea malalamiko dhidi ya Jeshi la Polisi, tulionesha hadi mfano wa jinsi chombo hicho kinavyoweza kufanya kaziChombo kama hicho kiliundwa Afrika Kusini ambapo kulikuwa na changamoto awali kuhusu Jeshi la Polisi na kikawasaidia sana, kuna umuhimu wa sisi Tanzania kuwa na chombo kama hicho"

"
Ni vile tu na nyie JFs mnataka kujadili lakini wahusika wanajulikana.

Kutekwa ni kutekwa tu.
 
Uoga wa watanzania ndio immunity ya watekaji.

Level hii ya uoga sijui inasababishwa na nini?

Kwanini tufikie kiwango hiki cha kuona sawa mtu kutekwa mbele yetu bila sisi kuzuia?

Kuna faida gani ya kusema tunaishi maisha kijamii kama hatuwezi kutetea maisha ya wengine?

Hii kitu mpaka saizi bado inanifikirisha.
 
Sababu kuu ni pale CCM inapoamini kwamba, nchi na wananchi ni mali yao waliyopewa na Mungu, na hivyo kuamini kwamba, wanaweza kuwashurutisha kukubaliana nao tu hata kwa mambo maovu, na wakati mwingine, ccm ni kama wanaamini kuwa, Mungu amewapa Watanzania wote kuwalinda na kuwachunga hata kwa fimbo ya chuma, na ndiyo maana utakuta, watu wakihoji kwa nguvu kuhusu rasilimali za nchi, katiba na mambo ya msingi katika nchi, wanapofanya tathimini, wao huona ni kama wananyang'anywa tonge mdomoni, wao huchukua jukumu la kuanza kuwapoteza watu hao

Mauwaji na utekaji ulioendelea sana nchini, kwa nchi yenye viongozi wenye kuthamini uhai wa watu, hili lisingeendelea kama ilivyo sasa!
 
tukitaka kupambana na hili kwanza tufute fikra kuhusisha matukio ya aina hii na siasa

imani yangu ipo kwa vyombo vya ulinzi kikubwa ni kulisaidia jeshi
 
Uoga wa watanzania ndio immunity ya watekaji.

Level hii ya uoga sijui inasababishwa na nini?

Kwanini tufikie kiwango hiki cha kuona sawa mtu kutekwa mbele yetu bila sisi kuzuia?

Kuna faida gani ya kusema tunaishi maisha kijamii kama hatuwezi kutetea maisha ya wengine?

Hii kitu mpaka saizi bado inanifikirisha.
Uoga unatokana na kwamba ukionekana na kaujasiri hata kidogo tu unafumuliwa ubongo wazi wazi ili na wengine wakome.

Ktk.mazingira kama.haya wasiojulikana wamepata mbinu konki ya kutulemaza
 
Back
Top Bottom