Mkurya mweupe
JF-Expert Member
- Aug 10, 2023
- 239
- 817
Ndugu Wana JF,
Nataka tushirikishane kuhusu matukio ambayo yaliwahi kutokea yakafanya niamini uwepo wa Mwenyezi Mungu. Mimi binafsi, kama muumini wa dini ya RC, kuna kipindi mdogo wangu aliwahi kusumbuliwa sana na ushirikina. Kwa kuwa imani yangu ilikuwa 50 kwa 50, nilikuwa nampeleka mpaka kwa waganga kupambania afya yake. Kipindi hicho alikuwa mwanafunzi; nadiriki kusema advance alisoma mwaka mmoja tu kutokana na kusumbuliwa na magonjwa ya kishirikina. Alipokuwa shuleni, alikuwa akiugua sana hadi kupoteza fahamu, lakini akiruhusiwa kurudi nyumbani, anapona kabisa na haumwi chochote. Mnakuwa naye wiki nyumbani, lakini akirudi shule tu, ugonjwa unarudi.
Mdogo wangu alikuwa vizuri kiimani ukizingatia alisomea shule za seminari. Muda wote alikuwa anakaa na kitabu cha "Nguvu ya Sala na Mawaridi" kila umuonapo, na hakosi kuhudhuria ibada kila siku licha ya hayo majanga. Baada ya kuona kwamba mdogo wangu anasumbuka hivyo, nikampeleka kwa mtaalamu akamuangalia. Nadiriki kusema pia nguvu za huyo mtaalamu zilikuwa nzuri kweli, aliweza kumuangilizia matatizo yake yote tokea yalipoanzia, yaani live kwenye screen, na alimpatia dawa za kutumia. Tukakaa naye nyumbani akawa vizuri kabisa, akaenda shule akawa anasoma, walau akawa anamaliza hata miezi mitatu bila kuugua. Baada ya hapo alianza kusali kama kawaida, tukaacha kwenda kwa mtaalamu.
Siku moja akiwa anasali Novena ya Mtakatifu Yuda Thadei kwa Roman Catholic kwa watu waliokabiliwa na matatizo makubwa, mdogo wangu alitema hirizi. Nikaifungua nikakuta imefungwa tu kwa uziuzi. Kesho yake tulienda kusali kanisani kabisa nikiwa naye maana alinambia kuwa kipindi anasali usiku, ameambiwa akaabudu ekarist takatifu kanisani. Nikaenda naye, kipindi tunasali yeye alipitiwa usingizi sana. Baada ya hapo alitapika hirizi hapo hapo kanisani, nikaichukua nikaiweka mfukoni. Nilipofika nyumbani niliifungua, nikakuta ina maandishi ikieleza vitu vibaya ambavyo vitamtokea mdogo wangu.
Mdogo wangu alianza kunielezea kuwa kipindi akiwa kanisani ametokewa na Mtakatifu Yuda Thadei akimuonesha vitu ambavyo anapaswa kufanya, ikiwemo kusali rozari ya huruma kila saa tisa usiku, kusali Zaburi 28 na 61, na novena ya Mtakatifu Ritha wa Kashia. Aliendelea kusali sana kwa imani na akawa anapewa maelezo kwamba apitie njia hii na hii, akisali hizo sala ili kupona na maadui zake. Alifanikiwa kupona na Mungu akawa amemshinda shetani. Hadi sasa, akiwa anasali huwa anapokea maono hata yanayotuhusu sisi ndugu zake. Anaweza kukupigia simu na kukuambia, "Leo nimeelekezwa ukasali labda novena fulani," na inakuwa kweli. Kisa hiki kilifanya niamini uwepo wa Mwenyezi Mungu. Licha ya kwamba huwa nasali kama yeye, sijawahi kubahatika kuona, lakini naendelea kusali. Yeye na dada yangu wanaposali huwa wanaongea na Mwenyezi Mungu moja kwa moja na kupewa maelekezo. Hii ni true story. Ebu share na mimi kisa kilichokufanya wewe uamini uwepo wa Mungu. Samahani kwa kuandika kwa haraka.