Matukio yanayoonesha uongo kwenye vitabu vya dini

Huna jipya wewe.......
 
1. Mungu hakumuumba Shetani, bali Lucifer, ambaye baada ya kuasi aliitwa Shetani au Ibilisi. Mungu aliumba viumbe sio kama "robot". Kila mara kwenye Biblia kuna sehemu za majdailiano. Sehemu hizo zinachangia kuona kwamba Mungu anataka awasiliane na viumbe wake. Malaika Lucifer kakuumbwa mbaya bali alikuwa malaika wa kuongoza sifa mbele zake. Uamuzi wa kuasi sio Mungu alimsukuma moyoni aufanye, hata kama inawezakana aliujua. Mfano Kaini na Habili. Kaini alipokusudia kutenda baya Mungu alimwonya lakini Kaini hakutii. Mungu mara nyingi anatuonya tusijiingize kwenye mabaya. Naamini pia Lucifer kabla hajaamua kuasi alionywa, lakini hakutii, ndio anaitwa mwasi.
Kuna wajibu ambao tunatarajiwa kuufanya, Naamini pia Shetani alijua anachofanya sio sahihi, pia Adamu alijua anachofanya sio sahii, kwa kuwa alipewa tahadhari.
Mungu kujua yote haina maana kwamba analazimisha kila afanye kile anachotaka, ingawa ndio shauku na nia yake, ila pia tuna hiari ya kufuata yale ya Kwake na tusipofuata wa kulaumiwa si Mungu ni mimi na wewe ambao tumepewa utashi wa kusikiliza, na kutii au kukataa. Kwa sababu hiyo Biblia inamwonesha Mungu hafurahii watu watendao kinyume naye. Anapenda sana atusaidie tuishi kwa ushindi kupitia njia ya upendo alioionesha. Yesu Kristo aliifia dhambi ili sisi ambao hatuna nguvu ya kutii sheria zote tupate nguvu ya kuishi ndani ya sheria za Mungu ambazo zinakuwa ndani yetu, tunapomwamini na kumpokea kuwa Bwana na Mwokozi. Tunafanyika wana wa Mungu.. Kwa Bwana aliyeishi bila dhambi (kushinda dhambi) ni mmoja tu ambaye ni Yesu. Nguvu ya kuishi maisha ya ushindi iko ndani Yake. Ukiwa Naye atakuwezesha kwa neema kwa njia ya imani.
Ukipata nafasi soma Biblia kwa utulivu utapata majibu yote ya maswali yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…