Maana ukiingia huko mjini twitter kila kona watu kwenye kila tukio lazima usikie wanataka katiba mpya. Je, Katiba mpya itakuwa ni suluhisho la haya matatizo?
Ndio, katiba mpya (na bora) ni suluhisho. Katiba inaendesha nchi na inaamua mfumo uendeshaji nchi, ndani yake ikitatua matatizo mengi.
Tukiwa na katiba bora itatusaidia kuweka mfumo mzuri wa kiuongozi unaowajibika kwa wananchi na kutatua matatizo ya kijamii.
Mfumo mbovu tulio nao sasa unaiweka serikali mbali na wananchi na kukwepa majukumu yake, huku ikijaribu kutupa mzigo wa majukumu hayo kwa wananchi.
Juzi nimemsikia mama Rais Samia akisema (baada ya kusikia kelele nyingi za wananchi wakiinyooshea vidole serikali juu ya kukithiri kwa ushoga) kuwa kazi ya kudhibiti ushoga ni jukumu la wazazi la kimalezi. Akasisitiza kuwa akiachiwa 'yeye peke yake' hatoweza. Anasema peke yake' kwasababu mfumo wetu mbovu unaibinafsisha serikali kwa mtu mmoja, means ikilaumiwa serkali kalaumiwa yeye rais pekee, wasaidizi hawana habari wanasubiri kusikia rais anasemaje ndo wafuate!
Lakini mfumo mzuri unaoongoza nchi kitaasisi unatambua kuwa mtatuzi mkuu wa matatizo ya kijamii ni serikali. Mama alitakiwa asimame na kusema sasa tayari kuna sheria imetungwa/inatungwa ili kudhibiti jambo hilo, halafu ndipo awatake wazazi nao kutimiza wajibu wao wa kimalezi. Ama katika mfumo mzuri zaidi jambo hilo lingeshashughulikiwa na mamlaka zingine bila kumtegemea rais.
Nilimsikia mchungaji mmoja akisema vema kuwa serikali kusisitiza viongozi wa dini wakemee ushoga kwenye nyumba za ibada ili kupambana na janga hilo ni kukwepa jukumu lake la msingi na kutumia njia ngumu kwani dhambi nyingi watu huonywa kuzifanya lakini bado zinatendeka, njia rahisi sana ni serikali kutunga sheria na kusimamia basi! Hayo mengine yanakuwa ziada. Lakini kwakuwa tuna serikali isiyotambua wajibu wake ama inajizima data na katiba inailinda hata matatizo madogo yanafutuka na kuwa makubwa.
Tupate katiba, si mpya pekee, bali iwe bora pia.